Wewe ungekuwa makini swali la post namba 218 usingefika post ya 314 ndio uje utoe majibu. Kitendo cha kuacha swali nililokuuliza ni pengine hukua makini au pengine haukuwa na majibu.
Umesema kuwa mtu anaweza kufikia ukamilifu kwa kutumia nyenzo na ala alizopewa.
Nikakwambia nitajie watu waliofikia hilo daraja la ukamilifu. Ukanitajia mitume na manabii kwamba walikuwa wakamilifu.
Nakuuliza swali:
Unapimaje Huo ukamilifu wa hao manabii na mitume je wakati wakiishi duniani au baada ya kufa?
Kama wakati wanaishi duniani, je hao manabii na mitume hawajawahi kufanya makosa ya kibinadamu hapa duniani?
Hao uliosema wamebashiriwa pepo hao hatuwezi kuwazungumzia hapa kwasababu Mimi nahitaji kujua waliopo Sasa au kipindi Cha nyuma.