Abu Ubaidah Commando
JF-Expert Member
- Sep 8, 2016
- 7,591
- 6,946
Adam na Hawa Walikuwa warabu,wazungu,wahindi,wachina,waafrika ? Kama walikuwa wazungu wachina walitoka wapi? Waafrika walitoka wapi?
Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asili) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao..." (4:1)
Hapa Mwenyezi Mungu anatufahamisha kuwa baada ya Adam (as) kuumbwa kisha akaumbwa mkewe ambaye ni Hawwa (a.s.) ndipo tukaenea wanaume kwa wanawake wengi duniani kutoka katika wawili hao.
Pia katika Qur'an 49:13 Allah (s.w.) anatufahamisha:
"Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanaume (mmoja, Adamu) na yule yule) mwanamke (mmoja Hawaa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbalimbali) ili mjuane (tu basi, siyo mkejeliane). Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule ambaye mcha Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote)". (49:13).