Je, Hatuna Wanawake wa kutosha kukidhi 50/50 au kuna kosa?

Mzee Mayala wakati mwingine huwa unakurupuka sana ...sijui ni umri na ugumu wa maisha? Gender balancing kwenye teuzi sidhani kama ipo kwenye criteria ...na ni kosa sana kumwacha mtu fulani kushika nafasi fulani kwa kisingizio cha usawa wa kijinsia. Mzee Mayala tafakari.
 
Mkuu Pascal, Mama kakujibu kwenye hotuba yake baada ya kuapisha majaji. Kumbe anatusoma.

Hi ni fursa kwetu wana JF tusio weza kuonana live na Rais kutumia vizuri mtandao huu kumfikishia maoni/ushauri.
 
Wakuu wa mikoa style ni "KUNYOFOA NA KUNYOFEKA "

NYOFOA HAPA NYOFEKA KULE, NYOFOA KULE NYOFEKA PALE.....🤣🤣🤣🤣🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️
 
Kwenye uteuzi huu, kuna idadi ndogo ya wanawake, na ndipo kwenye swali, "Jee ni kweli Tanzania hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa za uongozi kustahili uteuzi?
Na yeye analitambua si kwamba hajui, ila nadhani kuna kitu bado anachekecha, fikiria akiteua wenye elements za wale kumi na kenda waliowasaliti wenzao kule ng'ambo ya mto, si wanaweza kumsaliti hata yeye mwenyewe siku za usoni?
 
Katiba mpya ingemaliza haya yote
Hata katiba ikiwa mpya mentality ya watu tunaowapa madaraka ni shida, kwani ile tuliyonayo hawaijui kama ni katiba? Hivi uliwahi kufikiri mtu mtu mwenye akili timamu, msomi anaweza kuitumia kuchamba?
 
Mkuu hii ni process.Kwa mfano Sweden mojawapo ya Nchi zilizo na mafanikio makubwa kwenye gender equality bado haijafanikiwa kuwa na mishahara sawa kati ya wanaume na wanawake . Wanaume wana mishahara mikubwa zaidi kwa wastani.
Baraza la mawaziri Sweden lina wanaume 11 na wanawake 11.Vyama vya siasa vipo 8.Vitano vinaongozwa na wanawake.Bado tuna safari ndefu sana kwenye gender equality.
Muhimu sana kwa sasa ni wanawake waweze kurithi wanaume zao wakifariki bila vikwazo vya mila na sheria potofu.
 
Hawa wanawake wa Tanzania waajabu sana. Kwenye nafasi za ajira na uongozi wanataka 50/50 lakini ukija kuwaambia kwenye majukumu ya kutunza familia utasikia hayo ni majukumu ya mwanaume alipewa na Mungu.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tukijifunza kutoka Sweden, nadhani ipo haja ya kuandaa mfumo maalumu wa kuwajengea uwezo wa kujiamini wanawake kwenye masuala ya uongozi, nilichojifunza, wapo wanawake wenye uwezo mzuri kiuongozi, lakini wanakosa confidence.

SIjajua ni kwanini Sweden wana underpay wanawake, nilipata kuuliza hili pia sikupatiwa jibu, labda nasi tukilijua hilo linaweza kuna mahala pazuli pa kujengea mfumo wetu ili Sweden waje wajifunze kwetu.
 
Hawa wanawake wa Tanzania waajabu sana. Kwenye nafasi za ajira na uongozi wanataka 50/50 lakini ukija kuwaambia kwenye majukumu ya kutunza familia utasikia hayo ni majukumu ya mwanaume alipewa na Mungu.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
😂 👩‍❤️‍💋‍👨Kuna ndoa ya rafiki yangu inayumba kwasababu kama hii, mume na mke ni watumishi wa serikali, na wote wana package nzuri kabisa, ila linapokuja suala la kununua chakula, kununua mavazi ya watoto na kuwalipia ada, mama anamwambia mumewe wewe ndiyo baba wa familia ndiyo mwenye jukumu la kuilisha, kuivisha na kuisomesha, kipato chake ananunulia 💄 🤣
 
hii issue ya 50/50 sioni faida yake....kwani nafasi za kazi ni upendeleo au weledi......hata ikitokea wanawake wae 70% then wanaume 30% sawa tu...ilimradi walio kwenye nafasi wana weledi......
 
Update
Hoja za bandiko hili, zimejibiwa jana na Rais, Mama Samia wakati akiapisha majaji, amesema ataongeza nafasi za wanawake kwenye teuzi zote zijazo

Hii ni habari njema, hivyo mabandiko kama haya, yanasaidia.

P
 
nilipita mtaa fulani vile nikakuta kikao cha wanawake na hoja yao ilikuwa kwamba wao wanapendezwa sana kuhudumiwa na wanamme kuliko wanawake hivyo wangependa kuona wanaumme wanakuwa wengi.labda waulizwe wanawake kwa nn wanapenda kuhudumiwa na wanaume na shida iko wapi?nadhani ukiweza kupata maoni yao si wanawake wanasiasa bali wale wa kawaida kabisa ambao niliowakuta mm basi njoo na huo ushauri.
 
Hawa underpay kwa makusudi.Kazi za huduma kama waalimu,manesi,Försäkringskassan(bima ya huduma kwa jamii) kazi za maofisini ,maduka, Apotek (pharmacies),usafi ni kazi ambazo majority ni wanawake na mishahara ya kazi hizi ni ya chini kulinganisha na wanaume wanaofanya kazi zingine. Hivyo kufanya wastani wa mishahara ya wanawake kuwa chini kuliko ya wanaume.Wanapofanya kazi za aina moja mishahara huwa sawa.
 
Hivyo kufanya wastani wa mishahara ya wanawake kuwa chini kuliko ya wanaume.
Lakini kuna wengine wanafanya kazi sawa kabisa na qualifications ni sawa kabisa na wanakuwa wamesoma shule na vyuo sawa kabisa
 
Sweden wana sheria "samma lön för samma arbete" (mshahara sawa kwa kazi zilizo sawa) na hiyo inalindwa na sheria ya kazi inayoitwa kollektivavtal.
Muajiri anaweza kutoa mshahara wa juu zaidi kwa mojawapo ya hizi jinsia lakini ni lazima abainishe kisheria kwanini amefanya hivyo.Sababu mojawapo inaweza ikawa mmojawapo ana wajibu wa ziada kwenye hiyo kazi.Bila hivyo atashtakiwa na kulipa kiasi kilichopungua kwenye mshahara anaostahili mtu aliyeajiriwa.
 

 
Mkuu Tui, which is which?.
Mimi nimefanya kazi FCO (Foreign Commonweath Office) ya UK. Hii ni equal opportunity employer, mishahara inalingana kwa kazi za aina moja, ila kwenye allowances kuna tofauti, spouse allowance inatolewa kwa wanaume tuu, under the presumption mke yuko nyumbani kwa kazi ya kulea. Child child support pia inatolewa kwa wanaume tuu. Mke hata kama una mume, hulipwi spouse alowances wala child support, unless kama ni single mother!. Ili mke ulipwe spouse alowance, kwenye gender uonyeshe wewe ni trans gender, na wewe ndio mume na umeoa kwenye same sex marriage na mkeo yuko home, utalipwa!.
P
 
Bwana mdogo Tanzania hakuna chama cha upinzani bali ni matawi ya CCM
 
Mkuu P
Kwa mfumo wa Sweden kuna pesa unapewa kama mzazi kwa watoto wako kila mwezi kronor 1050 kwa mtoto mpaka atimize miaka 16.Ukiwa na watoto 2 kuendelea licha kupata 1050 kronor kila mtoto pia unaongezewa kiasi kingine cha pesa kutegemeana na watoto ulionao.(Flerbarn tillägg).Pesa hizi wanapewa wazazi wote bila kujali kipato.
Pia kuna pesa za kukusaidia kulipa kodi (bostadsbidrag) hizi zinatolewa kutegemeana na kipato.Ukiwa na kipato kikubwa hupewi.
Kuna allowance ya uzazi kwa wazazi wote wawili.Mnapewa siku 480 maternity allowance mgawane siku 240 kila mzazi.Ila kila mzazi ana uhuru wa kumpa mzazi mwenzake siku 60 kati ya hizo.Allowance inategemea kipato chako lakini cha chini kabisa ni kronor 4800(kama milioni na laki mbili za Tanzania).Baba au mama mmojawapo anaendelea na kazi na mwingine anabaki nyumbani kulea.
Kodi ni asilimia 30-32 ya kipato chako.Shule ni bure including chakula mpaka level ya sekondari.
Chuo kikuu masomo ni bure lakini unakopeshwa kulipia chakula na malazi.
Hospitali ni bure ,madaktari wa meno ni bure kwa watoto na vijana mpaka umri wa miaka 21.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…