Je, Hatuna Wanawake wa kutosha kukidhi 50/50 au kuna kosa?

Je, Hatuna Wanawake wa kutosha kukidhi 50/50 au kuna kosa?

Marekani mpaka sasa hawajaweza kufikia 50/50 pamoja na kuwa na uzoefu wa miaka chumgu mzima kwenye mfumo wao wa utawala.

Great Britain kwa miaka yote wamekuwa na PM Margaret Thatcher ambae alichaguliwa na Thereza May ambae alirithi serikali toka kwa Cameron.

Nadhani tujipe muda, wapo wanawake wenye uwezo na ni sawia kabisa kuwa sehemu ya utawala/uongozi.

Ila itakuwa makosa kumpa mti nafasi kwa kuwa ni mwanamke.
Nadhani ni sawa kumpa mtu nafasi kwa kuwa ana uwezo wa kitimiza majukumu ya kuwatumikia Watanzania na kumsaidia Mhe. Rais ambae ni mamlaka ya uteuzi.

Kwetu sisi ambao tuna watoto wa kike, dada, au wake zetu; tuendelee kuwajengea uwezo kwa kupata elimu na wakipata majukumu kwenye maeneo yao watakuza skills za uongozi.

Viongozi wanazaliwa na kutengenezwa (leaders are born and also made) how, tuwape fursa ya majukumu eventually watakuza skills zao za uongozi.

Madam President kufika hapo juu alianzia mahali kwa kutimiza majukumu with time ata-gain skills.

Kila la heri kwa viongozi wote waliopata uteuzi wakiwemo wanawake, ila tusikimbilie kwenye 50/50 bila kuwa na maandalizi ya viongozi kwa kuwapa majukumu ili wakue kiungozi.
 
Wanabodi,

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kila nipatapo fursa, huwa naendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zina lengo la kukuza uzalendo na kulisaidia taifa letu, kusaidia nchi yetu, kusaidia serikali yetu na kusaidia viongozi wetu waweze kutuongoza vizuri kwa kuangazia maeneo yenye changamoto ili zitatuliwe. Makala ya leo ni hoja na swali.

Hoja ni "Kufanya Kosa Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa", hoja hii inakuja kwasababu hatuongozwi na malaika, tunaongozwa na binadamu, katika kuongoza huko, huweza kufanyika makosa ya hapa na pale. Hivyo hata kukifanyika makosa, kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa.

Nisimalize bila kumpongeza Mama Samia kwanza kwa ku heal the nation kwa kutenda haki, na pili ni pongezi kwa kuyaishi maneno yake ya kuteua yoyote hata kutoka upinzani.

Tanzania ni yetu sote,
Mungu mbariki Mama Samia.
Mungu ibariki Tanzania.

Paskali
Kwa vile saa hizi Mama tayari yuko kwa msusi akifumuliwa nywele tayari kwa kusuka upya, kama tunao wa kutosha, tumshauri Mama aanze na 50/50 kwenye teuzi mpya, mfano kama yeye alivyoweka historia ya kuwa Mwanamke wa kwanza kuwa VP na baadaye akaupata urais by default, lakini na yeye ametuteulia Waziri wa kwanza wa ulinzi mwanamke. Sasa katika hii suka mpya, kama kuna mwanamke mwenye uwezo wa kuwa PM, apewe, hata kama kuna mwenye uwezo wa kuwa JM ampe, Spika najua atakuwa. Najua kutatokea maneno haiwezekani Rais mwanamke, Waziri Mkuu mwanamke, Spika mwanamke, JM , mwanamke!, yaani wakuu wote wa mihimili ni wanawake!. Kama ni kweli, wanaume tuko sawa na wanawake, mbona walipokuwepo wanaume tuu, hakuna aliyeshangaa?.
Kama wapo wanawake wa kukidhi 50/50, Rais wetu Samia, nenda na 50/50, utengeneze historia ya kweli ya ukombozi wa mwanamke, maana huwezi kujua, kwa nini Mungu alimtwaa JPM akakuleta wewe, usikute amekuleta ili kuwakomboa wanawake, kama wapo wenye sifa, wateue tuu.
p
 
Wanabodi,

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kila nipatapo fursa, huwa naendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zina lengo la kukuza uzalendo na kulisaidia taifa letu, kusaidia nchi yetu, kusaidia serikali yetu na kusaidia viongozi wetu waweze kutuongoza vizuri kwa kuangazia maeneo yenye changamoto ili zitatuliwe. Makala ya leo ni hoja na swali.

Hoja ni "Kufanya Kosa Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa", hoja hii inakuja kwasababu hatuongozwi na malaika, tunaongozwa na binadamu, katika kuongoza huko, huweza kufanyika makosa ya hapa na pale. Hivyo hata kukifanyika makosa, kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa.

Hoja hii inakuja kwa tangu rais Samia ashike usukani, juzi ndio amefanya uteuzi wake mkubwa wa kwanza wa viongozi wengi kwa mpigo. Kwenye uteuzi huu, kuna idadi ndogo ya wanawake, na ndipo kwenye swali, "Jee ni kweli Tanzania hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa za uongozi kustahili uteuzi?. Kwa maoni yangu japo uteuzi huu una walakin ya idadi ndogo ya wanawake, yaani gender imbalance, Rais Samia hajafanya kosa, bali akirudia idadi ndogo hivi kwa ma DC, RAS, DED na ma DAS, then, litakuwa ni kosa!.

Lazima tukubali, tukatae, kwenye gender balance kule nyuma, kuna makosa yalifanyika. Sasa ni jukumu letu sisi tuliobahatika kuyaona makosa hayo ya nyuma, ambayo Rais Samia ameyarithi, tumsaidie, rais Samia, kwa kuyaangazia makosa hayo, ili rais Samia asiyarudie makosa ya nyuma kwa spirit ile ile ya kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa

Kabla haujasoma hoja za bandiko hili, naomba nikupe homework ndogo ya kusoma bandiko langu hili

Kwenye bandiko hilo nilisema

Kwa vile Mama Samia amejitanabaisha wazi yeye ni kama JPM, kwenye upande wa uteuzi wa JPM, we had gender problem, Mama Samia, asiiendeleze.

Uteuzi wa JPM, Kwa mfano idadi ya mawaziri wanawake ni 4 tu kati ya 19, hii ni asilimia 21%. wanaume ni asilimia 79%. Kwenye Baraza la Mawaziri la Samia, lina mawaziri 25, wanawake ni 6 ambao ni asilimia 24% wanaume 19 ambao ni asilimia 76%. Hivyo hapa gender imbalance imeendelezwa!.

Kwenye uteuzi wa Wakuu wa Mikoa, kati ya wakuu wa mikoa 26 wa Magufuli, wanawake ni 4 tu ambao ni asilimia 15% wakati wanaume ni 21 ambao ni asilimia 85%!. Sasa rais Samia anapita mule mule, alikopita JPM kwenye uteuzi wa wakuu wa mikoa wa Samia ameteuwa ma RC wanawake 4 tu kati ya ma RC 25, hii ni asilimia 16% ndio wanawake na wakati wanaume ni 21 ambao wanafanya asilimia 84%!.

Kwenye wakuu wa wilaya, kati ya wakuu wa wilaya 134 wa Magufuli, wanawake ni 25 tu ambao ni asilimia 18%, wakati wanaume ni 109 ambao ni asilimia 82%. Na kwa upande wa Wakurugenzi, kati ya wakurugenzi

Katika safari ya kuelekea gender balance ya 50/50 katika uongozi, mimi siamini kuwa Tanzania hatuna wanawake wa kutosha hadi uteuzi wa wanawake uwe that low!.

Kwa maoni yangu, naamini uteuzi huu wa ma RC ni mama Samia, ameendelea kubeba some luggages na baggages za mtangulizi wake. Hilo ni kosa!. Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa!. JPM alifanya kosa kwenye gender balance.

Gender balance kwenye baraza la mawaziri hatuwezi kulaumu, kwasababu ili mtu uwe waziri ni lazima kwanza uwe mbunge, ikitokea hakuna wanawake wa kutosha kujaza nafasi za kufikia kiwango cha 50/50, hili litaeleweka, kwasababu Mama Samia, ameingia na kuwakuta wabunge tayari wapo, ikitokea wabunge wote hadi wa viti maalum, hawana sifa za uwaziri, hatuwezi kulaumu, kwasababu sio kosa lake. Huwezi tuu kujiteulia watu hawana sifa ili tuu kutimiza gender balance. Lakini kwenye ma RC, ma DC , ma RAS, ma DAS ns na DED, yaani Wakurugenzi, haiwezekani Tanzania ndani ya hii milioni 60, wakakosekana wanawake wenye sifa.

Tanzania ni yetu sote,
Mungu mbariki Mama Samia.
Mungu ibariki Tanzania.

Paskali
Update
Hoja za bandiko hili, zimejibiwa jana na Rais, Mama Samia wakati akiapisha majaji, amesema ataongeza nafasi za wanawake kwenye teuzi zote zijazo

Hii ni habari njema, hivyo mabandiko kama haya, yanasaidia.

P
Ukiandika kitu ukashauri jambo fulani, halafu jambo uliloshauri likaja kutekelezwa, huna budi kupongeza utekelezaji wa jambo hilo.

Ushauri wa bandiko hili umeanza kutekelezwa safari ya kuelekea kwenye 50/50 ya gender balance kwenye uteuzi imeanza na uteuzi mpya wa majaji 22, majaji 11 wanawake na 11 wanaume. Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?

Hongera sana Rais Mama Samia, hii trend tuendelee nayo katika teuzi zote zinazofuata, na mwaka 2025 tukamilishe kwa uteuzi wa wagombea ubunge, tukifanikisha 50/50 tufutilie mbali viti maalum.
P
 
Back
Top Bottom