Je, Hatuna Wanawake wa kutosha kukidhi 50/50 au kuna kosa?

Marekani mpaka sasa hawajaweza kufikia 50/50 pamoja na kuwa na uzoefu wa miaka chumgu mzima kwenye mfumo wao wa utawala.

Great Britain kwa miaka yote wamekuwa na PM Margaret Thatcher ambae alichaguliwa na Thereza May ambae alirithi serikali toka kwa Cameron.

Nadhani tujipe muda, wapo wanawake wenye uwezo na ni sawia kabisa kuwa sehemu ya utawala/uongozi.

Ila itakuwa makosa kumpa mti nafasi kwa kuwa ni mwanamke.
Nadhani ni sawa kumpa mtu nafasi kwa kuwa ana uwezo wa kitimiza majukumu ya kuwatumikia Watanzania na kumsaidia Mhe. Rais ambae ni mamlaka ya uteuzi.

Kwetu sisi ambao tuna watoto wa kike, dada, au wake zetu; tuendelee kuwajengea uwezo kwa kupata elimu na wakipata majukumu kwenye maeneo yao watakuza skills za uongozi.

Viongozi wanazaliwa na kutengenezwa (leaders are born and also made) how, tuwape fursa ya majukumu eventually watakuza skills zao za uongozi.

Madam President kufika hapo juu alianzia mahali kwa kutimiza majukumu with time ata-gain skills.

Kila la heri kwa viongozi wote waliopata uteuzi wakiwemo wanawake, ila tusikimbilie kwenye 50/50 bila kuwa na maandalizi ya viongozi kwa kuwapa majukumu ili wakue kiungozi.
 
Kwa vile saa hizi Mama tayari yuko kwa msusi akifumuliwa nywele tayari kwa kusuka upya, kama tunao wa kutosha, tumshauri Mama aanze na 50/50 kwenye teuzi mpya, mfano kama yeye alivyoweka historia ya kuwa Mwanamke wa kwanza kuwa VP na baadaye akaupata urais by default, lakini na yeye ametuteulia Waziri wa kwanza wa ulinzi mwanamke. Sasa katika hii suka mpya, kama kuna mwanamke mwenye uwezo wa kuwa PM, apewe, hata kama kuna mwenye uwezo wa kuwa JM ampe, Spika najua atakuwa. Najua kutatokea maneno haiwezekani Rais mwanamke, Waziri Mkuu mwanamke, Spika mwanamke, JM , mwanamke!, yaani wakuu wote wa mihimili ni wanawake!. Kama ni kweli, wanaume tuko sawa na wanawake, mbona walipokuwepo wanaume tuu, hakuna aliyeshangaa?.
Kama wapo wanawake wa kukidhi 50/50, Rais wetu Samia, nenda na 50/50, utengeneze historia ya kweli ya ukombozi wa mwanamke, maana huwezi kujua, kwa nini Mungu alimtwaa JPM akakuleta wewe, usikute amekuleta ili kuwakomboa wanawake, kama wapo wenye sifa, wateue tuu.
p
 
Ukiandika kitu ukashauri jambo fulani, halafu jambo uliloshauri likaja kutekelezwa, huna budi kupongeza utekelezaji wa jambo hilo.

Ushauri wa bandiko hili umeanza kutekelezwa safari ya kuelekea kwenye 50/50 ya gender balance kwenye uteuzi imeanza na uteuzi mpya wa majaji 22, majaji 11 wanawake na 11 wanaume. Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?

Hongera sana Rais Mama Samia, hii trend tuendelee nayo katika teuzi zote zinazofuata, na mwaka 2025 tukamilishe kwa uteuzi wa wagombea ubunge, tukifanikisha 50/50 tufutilie mbali viti maalum.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…