Ni Chlorine tu hiyo. Ni kemikali salama kimtindo, na maji yenye taswira hiyo ni salama zaidi kiafya (hayana vimelea) japokuwa ubora wa uhalisia (rangi na ladha) wa maji huonekana kuwa tofauti.
Ni kemikali inayotumika kutakatisha maji dhidi ya vimelea wengi wa bacteria. Ikiwekwa kwenye maji, PH ya maji hubadilika na kuwa alkalinity zaidi, na vimelea hufa. Ni sawa tu na ile waterguard ambayo ilikuwa ikiuzwa madukani ili kwenda kutakatikasha maji.
Mamlaka za maji nyingi ambazo hazina mifumo bora ya kisasa ya kuchuja (filter), kuhifadhi (sedimentary storage) hukimbilia moja kwa moja tu kuweka Chlorine nyingi kwenye chamber ya kusukuma maji kwenda kwa wateja ilimradi tu wateja wasife kwa magonjwa ya vimelea vilivyopo kwenye maji.
Maji yenye taswira hiyo ni ngumu mnoo kwa watumiaji wake kupata kipindupindu, Typhoid, Amoeba, na magonjwa mengi ya kuharisha.
Kitaalamu, inashauriwa, maji yakiwa namna hiyo (yana chlorine nyingi na mbichi) ni vyema yakachotwa na kuwekwa yakatulia at least nusu saa ili kemikali ipoe, isambaratike na imalize kazi ya kuua vijidudu.