Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Kisa Kinachosambaa sasa nchini Misri..
Vyombo vya habari nchini Misri vimesambaza kisa cha kusikitisha cha daktari mmoja aliyetumia zaidi ya miaka 30 akifanya kazi nje ya nchi yake, akiwa nchini Saudi Arabia, akipambana kujenga mustakabali wake na wanawe.
Katika kipindi cha miaka 16 pekee, daktari huyo aliwatumia wanawe kiasi kinachozidi pauni milioni 50 za Kimisri (takriban zaidi ya dola 1058922.70 sawa na shilingi 2,659,484,361.05 na zaidi kwa rate ya sasa).
Na akawapa wanawe mamlaka yote ya kusimamia majengo na mali zake, akiamini kuwa wao ndio "usalama" wake wa baadaye.
Lakini cha ajabu alipostaafu na kurejea nyumbani..
Alistushwa kukuta fedha zote zimeyayuka, na majengo yote yameuzwa au kuandikwa kwa majina ya watu wengine, na hakuachiwa hata senti moja.
Daktari huyo alieleza kuwa alijenga maghorofa matatu makubwa nchini Misri, lakini alishangaa kukuta yamechukuliwa na maeneo yake kuuzwa na mwanawe mkubwa bila yeye kujua, jambo lililozima ndoto yake ya kuwa na maisha mazuri uzeeni.
Maumivu ya kupoteza mali zake hayo yalimsababishia matatizo ya kiafya kwani baadae kidogo alipatwa na tatizo la kuvuja damu kwenye ubongo kutokana na shinikizo kubwa la kisaikolojia baada ya kugundua usaliti huo kutoka kwa watu wake wa karibu aliyekuwa akiwaamini.
Leo hii, daktari huyu anaomba dua na maombi, baada ya kupoteza miaka ya maisha yake ugenini na kubaki akihangaika na uzee wake akiwa peke yake, bila nyumba wala mali.
Chanzo: Tazama Comment.
Kisa hiki kinatufundisha kutowaamini watu kupita kiasi kwasababu tu ni jamaa zetu.
Mwenyezi Mungu amsaidie mzee wetu.