Uchaguzi 2020 Je, hii ndiyo sababu ya NEC kutochapisha fomu za wagombea Urais kwa "Alphabetical order"?

Kutakuwa na wakala wa CCM anayewatolea macho wapiga kura ambao ni wanachama wa CCM. Ukimchagua Lissu lazima utaonekana tu unavyomtafuta kule chini. Hivyo mwanaccm itambidi apige tu pale juu kama akishindwa kujilipua.

Nahisi washaambiwa OLE WAO. ...
 
Tupe sababu moja kuu ya kutofuata mpangilio wa alfabeti kama ilivyo kawaida.
 
Uxuri mgombea wangu wa chauma nimeona alipo nikifika sina cha kukawia

sent from HUAWEI
Una undugu na "delicious" au Elton John!?
Hii "uxuri" ndio nini?
Halafu wewe ndio unakuwa wa kwanza kuandika/kusema, "ooh Chadema wanasapoti ushoga"!
 
Nape alikuwa sahihi alipodukuliwa simu yake alikuwa akisema tuna Rais mshamba.
Huu ni ushamba wa hali ya juu sana kudhani CCM wakikaa pale juu basi watu hawataona wengine au? Ushamba tuu.
Tuko kwenye kizazi ambacho wasiojua kusoma na kuandika wamebaki wachache sana kama siyo kuisha kabisa.
Sasa hivi mtu anaenda kupiga kura akijua anaenda kuchinja, hata kama wageuzie karatasi Lissu awe ukurasa wa pili tutamtafuta tuu
 
na sisi tunasema usihangaike we check jina la mwisho tu. Wamempiga chura teke.
ila haya mambo ya sijui wepesi wa kuonekana yanafanya waTz tuonekane akili zetu sio,hivi kabisa umesikiliza sera,umefanya maamuzi,halafu unaenda pale unatiki Jiwe katili kwa sababu ya uvivu wa kumtafuta Lissu. Duuh
 
Kama ni kweli nia ilikuwa kumpoteza Lissu basi huyo aliyetoa wazo hilo hana kazi, angemuweka katikati hapo ingewapa shida mtu kutafuta na macho yenyewe haya ya siku hizi unaona kama huoni ingekuwa shida ila hii ya mwisho unaambiwa yule wa mwisho ndio mwenyewe, rahisi sana. kawaida mtu ukimpa karatasi anataka kuona wa juu halafu sababu wa Tz tunapenda umbea tunapenda kuona nani wa mwisho huku..
 
Na kwa masikitiko makubwa nchi hii bado inao watu wengi wajinga kabisa wanaosikiliza upuuzi kama huo na kufanya walivyoelekezwa.

Halafu tunasema kama taifa tunaendelea bado tukiwa na watu wajinga wengi kiasi hicho!
 
Mbinu za ushindi bwashee
 
Wamekosea sana kumuweka JPM pamoja na hawa wasio hata na chembe ya uzalendo. Wamekosea sana

Sijui unawezaje kupima uzalendo wa mtu usiyemjua vizuri. Wote wawili Lissu na JPM huwajui zaidi ya kuwasikia tu jinsi wanavojieleza au kuelezwa!! Ninyi ndio pia hupima imani au dhambi za watu kwa maneno na matendo yao - huku hamjui mioyo yao. Uzalendo ni jambo lisilopimika!! Uhalifu ndio hupimika. Ingekuwa bora ukataja uhalifu wa Lissu na kumuita ni mhalifu.

Nchi hii ina tatizo la ujinga zaidi kuliko njaa na maradhi!! Wewe ni kielelezo cha ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…