Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Bila hata kusoma sheria, kanuni za bunge, kitu kimoja ni wazi kwa mantiki ndogo tu.
Ikiwa katiba ya nchi inasema wananchi wana haki ya kutoa na kupewa habari muhimu kuhusu nchi yao inavyoendeshwa, na Mpina amewatimizia haki hii wananchi kwa kuweka wazi madai yake ili kila mwananchi ayajue, basi ni dhahiri kwamba alichofanya Mpina, bila kujali kuwa maoni yake ni sawa au si sawa, ni kutimiza haki yake ya kikatiba, na kutimiza haki ya Watanzania ya kikatiba.
Kitendo hicho, bila kujali kanuni za bunge zinasema nini, ni haki ya kikatiba, sheria au kanuni yoyote itakayotungwa kuvunja haki hiyo itakuwa kinyume na katiba na hivyo batili.
Katiba ndiyo sheria mama. Kwingine kote huko inabidi kufuata katiba.
Wananchi ndiyo wanawakilishwa na bunge, wana haki zote za kujua bunge linaendaje na mashauri yaliyo bungeni yana habari gani, kwa undani.
Mpina kaonewa tu.