Je, hii ni sawa kwa media kutoa maoni ya kukandamiza timu za nyumbani?

KJ07

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2021
Posts
2,370
Reaction score
5,381
Salaam wakuu.

Hivi sasa tunaona serikali na wadau mbalimbali wakitoa support kwa timu za mpira za simba na yanga kuelekea michezo yao ya robo fainali klabu bingwa barani afrika.

Inatokea media yenye waandishi wa mchongo na kupost maneno yenye ukakasi yasiyo na chembe ya kutia moyo timu za nyumbani licha ya hali halisi.

Hii sio sawa kwa media kubwa kama EAST AFRICA RADIO/TV KUPUBLISH UJINGA HUU.

Haijakaa kitaalamu
1711013134929.jpg
 
Asante moderators kwa kurekebisha kichwa cha thread.
 
Yanga ikikamilika haoa kwa mkapa mamelodi hachomoki, waombee kina aucho, yao yao na pacome wawe wodi ya mwaisela la sivyo wataipata pata.
Hawa wote wageni ushindi wao haoa ni sare, wakipata sare wakafanye sherehe kwao huko.
 
Ni kuhamasisha na kuleta tention ya match husika, mkianza kusifiwa na kila mtu match itapoteza utamu
 
Salaam wakuu.

Hivi sasa tunaona serikali na wadau mbalimbali wakitoa support kwa timu za mpira za simba na yanga kuelekea michezo yao ya robo fainali klabu bingwa barani afrika.

Inatokea media yenye waandishi wa mchongo na kupost maneno yenye ukakasi yasiyo na chembe ya kutia moyo timu za nyumbani licha ya hali halisi.

Hii sio sawa kwa media kubwa kama EAST AFRICA RADIO/TV KUPUBLISH UJINGA HUU.

Haijakaa kitaalamuView attachment 2940741
Wapewe adhabuu hapo ni sawa na wamevaa jezi za mamelod.
 
Salaam wakuu.

Hivi sasa tunaona serikali na wadau mbalimbali wakitoa support kwa timu za mpira za simba na yanga kuelekea michezo yao ya robo fainali klabu bingwa barani afrika.

Inatokea media yenye waandishi wa mchongo na kupost maneno yenye ukakasi yasiyo na chembe ya kutia moyo timu za nyumbani licha ya hali halisi.

Hii sio sawa kwa media kubwa kama EAST AFRICA RADIO/TV KUPUBLISH UJINGA HUU.

Haijakaa kitaalamuView attachment 2940741
Kwenye mpira Tanzania kuna "Watani wa Jadi".

Hilo huwezi kulimaliza hata kwa sheria.

Ni bora ulikubali tu.
 
Ngoja nikae na utabiri wangu moyoni....watanzania sio watu wa kuwaambia kitu...watakushushia mvua za maneno mpk utabiri utavurugika... 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Na bora ukae kimya.
 
Ila Yanga mnadeka sana.Engeneer Hersi kuna dhambi ya usaliti alifanya kubwa sasa inaitesa sana Yanga.
 
Kwenye mpira Tanzania kuna "Watani wa Jadi".

Hilo huwezi kulimaliza hata kwa sheria.

Ni bora ulikubali tu.
Kwahyo chombo cha habari cha Tanzania kinatakiwa kusimamia upande gani.
 
Chombo cha habari kinatakiwa kuwasilisha maoni ya washabiki.

Washabiki wakiichoka timu ya nyumbani na kushangilia timu ya kigeni, hiyo ni haki yao.

Tafuta sababu kwa nini wamefanya hivyo, utibu chanzo cha ugonjwa, si utake kutibu dalili za ugonjwa.

Mgonjwa akiwa na TB, anakohoa, wewe unampa Cofta kupunguza kikohozi, badala ya kutibu TB, hapo utakuwa unafanya kazi ya bure tu.
 
We jamaa inavyoonekana ni hata hujui misingi ya vyombo vya habari.
Vyombo vya habari havitakiwi kuwa na upande ndiyo maana chombo cha habari chenye kuonesha mapenzi fulani kwa upande fulani waziwazi basi huanza kupoteza mvuto.

Nini maana ya serikali kuzi support timu zote mbili katika hatua zilizofikia.

Hauangalii Azam tv the way wanaziterm simba na yanga na namna wanavyozielezea kuelekea mechi zao.

Kilichofanywa na EATV Sio professionalism
 
Back
Top Bottom