The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,950
- 12,550
Kiongozi ni yule Anaeonyesha njia.Na anayogafanya Mh.Raisi si ziara za kushtukiza.Nionavyo ni ziara anayoifanya tayari taarifa anazo mezani Hivyo basi anapojitokeza huwa anatoa Funzo kwa wale wote wenye Tabia na Mienendo ya Kuhujumu Nchi.Na kama Raisi aliyechaguliwa na Wananchi wake ni lazima afanye hivyo hiyo ni sehemu ya utendaji wake.Mnaoandika ya kuwa hii sasa ni ONE MAN SHOW IMA COMEDY Bakieni vivyo hivyo.Mwisho wa siku Tutarudi kwenye Mstari na siyo Bussiness as Usual,whether u like it or not.Wewe umeajiriwa eti ofisi yako siyo sitting room yako Nyumbani ufanye unapojisikia ima kupiga Dili NJAA NI MSHAURI MBAYA
Wewe
Fahamu kuwa.....Nidhamu ya woga inaondoa weledi.
Na Mtu atafanyaje kazi bila weledi.
Taifa letu changa linahitaji kuendelea.
Litakuwa Taifa la mazuzu kwa kukosa weledi.
Je pale alikuwapo Waziri/Katibu Mkuu/Mkurugenzi?
Ni Hatari kwa Rais kujibishana na mfanyakazi wa kada ya chini mbele ya vyombo vya habari, pasipo kuwapo na hao viongozi wateule wa Rais.
Katika hali ya kawaida, maendeleo ya nchi yoyote duniani yanashamirishwa na kurutubishwa na UBUNIFU wa wananchi na hasa watendaji wake. Ubunifu hauwezi kuibuka katika mazingira ya uwoga. Kinachofanyika sasa hivi ni kujenga mazingira ya uwoga na kudumaza ubunifu. Hii ni hatari sana kwani wataalam wetu watafanya kazi kama robot.Naam dadangu, aidha watu wana nidhamu au hawana. Na hakuna kitu kama "nidhamu ya woga". Ukiwa mtumishi wa umma ni lazima uogope; uogope kuvunja sheria, uogope kutumia madaraka yako vibaya, uogope kukutwa unavuruga! Unatakiwa utende kazi kwa kujiamini, kwa weledi na kwa ufanisi unaotakiwa kutokana na nafasi yako. Sasa bosi wako akitokea na kukuta umekunja nne ukaruka juu na kujimwagia chai na kuanza kujifanya unafanya kazi manake ni kuwa hukuwa mwoga in the first place! Ungekuwa unaogopa ungekuwa huna wasiwasi. Hivyo, woga wa kinidhamu unahitajika na viongozi waendelee kuwashtukiza na kuwatumbua hasa kama watumishi hawawaogopi mabosi wao au viongozi wao wajuu.
Tulidekezwa mno hadi tukadeka na kuamini tunatakiwa kudekezwa.
Yes, aweza kabisa na hakuna kizuizi chochote cha kikatiba!!Jamani, someni Katiba basi... duh.. kwani Rais ni rais wa kusimamia watu wa juu tu? Rais ana uwezo wa kumhoji mtumishi yeyote wa umma; hata tarishi!
Bro.. Una maana nzuri na maswali yako ni mazuri sana., ila Kwa mtazamo wangu Huyu jamaa Kwa kufanya hivi anawapa warning wahusika wote,chain nzima kwamba wanahitaji kuwa makini zaidi,alikuwa hashindwi **** maelekezo mh Makame Mbalawa.. Lakini anampa warning indirectly kuwa makini zaidi.Na ni vizuri kumfata mtu anayehusika na tatizo(kwenye kiini),kama ni airport,muhimbili,bandarini etcMantonga;
Nimekuelewa na ni vyema sana kwamba, Rais anapofanya ziara hizi tayari anakuwa na taarifa mezani kwake......kwa hiyo anakuwa anajua anachokwenda kukiona na kukifanya.
However, maswali yangu kwako na wengine wenye mtazamo na kuamini kama wewe ni haya;
Hivi hizi "taarifa za kiintelejinsia", zinakuwa zinamfikia yeye tu Rais na kuwapiga chenga wasaidizi wake mfano ktk ishu ya JNIA ni waziri wa sekta ya ujenzi, mwasiliano na uchukuzi, katibu mkuu wa wizara na kisha shuka chini huku hadi kwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege, mkuu wa mkoa nk??
Je, ni kwamba hawaamini hawa wasaidizi wake kwamba labda na wenyewe ni walewale tu, au ni kwa nini hasa?
Je, kuna umuhimu wa kuweka wasaidizi hawa kweli iwapo kazi zote za serikali zaweza kufanywa na mtu mmoja tu?? Je, si ingekuwa bora sana kupunguza gharama kwa kulifanya hili liwe rasmi kikatiba - kwa maana tusiwe na mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa nk?
I thought, kama Rais ana mainfoma wake na wanamletea taarifa yeye moja kwa moja, naye pia aweza kuzishusha taarifa hizi moja kwa moja kwa wasaidizi wake....kwamba mahali flani kuna moja mbili tatu, waziri au katibu mkuu au RC au yeyote nenda immeaditely shughulikia na niletee taarifa by this time.....
Hiki ndicho ambacho kina Ben Saanane wanakisema kuwa ktk serikali hii hakuna "chain of accountability" kiasi ambacho utendaji wa serikali ni ule wa ONE MAN SHOW....na ikitokea huyu mtu akatoweka leo aidha kwa kifo (Mungu apishilie mbali) au vyovyote vile, maana yake mchezo unakuwa umeishia hapo, tunaanza upya tena kumtafuta magufuli mwingine!!
Bro.. Una maana nzuri na maswali yako ni mazuri sana., ila Kwa mtazamo wangu Huyu jamaa Kwa kufanya hivi anawapa warning wahusika wote,chain nzima kwamba wanahitaji kuwa makini zaidi,alikuwa hashindwi **** maelekezo mh Makame Mbalawa.. Lakini anampa warning indirectly kuwa makini zaidi.Na ni vizuri kumfata mtu anayehusika na tatizo(kwenye kiini),kama ni airport,muhimbili,bandarini etc
Huo weledi ambao hauna woga umelifikisha wapi taifa; mnataka kuendelea kudekezwa?
Kama unafanya kazi yako vizuri kabisa na kwa kujiamini kwa nini uwe na nidhamu ya woga? Kama unafanya kazi vizuri kabisa boss ama mtu yeyote atakayeingia sehemu yako ya kazi utampokea kwa furaha na kujiamini. Hutakuwa na hata chembe ya woga!
Hiyo sasa itakuwa ni nchi ya mazombieNi afadhali kuwa na nidhamu ya woga kuliko kukosa nidhamu kabisa.
Go Magufuli.
Hiyo sasa itakuwa ni nchi ya mazombie
Maisha bila sukari yanawezekana.
Kungekuwa hakuna haja ya Serikali kuona hii issue inazidi kuipaka na hatimaye kujiingiza katika biashara ya kuagiza sukari toka nje.
Mkuu ili heshima kidogo iliyobaki uliyojiwekea humu miaka mingi mi ningekuomba huu ut um bo ulioanza nao sasa ungeufungulia new I'd na mpe taarifa mkuu ili ajue unapambana kupitia hiyo I'd ili asikupite kwenye udcYaani, katika utimamu wa akili kabisa unasema ni "heri ukose nidhamu kwa vile utafukuzwa kazi" kuliko kuwa na nidhamu? Mtu mwenye nidhamu ya woga anaweza kukiuka maadili lakini mwenye woga wa nidhamu atajitahidi kufuata maadili na weledi. Hakuna uzuri wa kuwa na mtu asiye na nidhamu.
Katiba ninayoisoma inaainisha "chain of command" sijui wewe mwenzangu unasoma ipi!Kwani akiwa Rais anakatazwa kushughulikia mambo yaliyoko chini kabisa; au hata Katiba hamuisomi?