Kwa miaka ya hivi karibuni watu wanaokuwa diagnosed na UTI imeongezeka maradufu. Katika kutafuta sababu nimekuja na sababu tatu ambazo zinazoweza kuchangia.
Wakuu, je wewe unadhani ipi ni sababu kubwa kwa ongeze la ugonjwa huu kati ya hizi
A: Ongezeko la mwanawake wa sikuhizi kushindwa kujisafisha au maji si masafi.
B: Ongezeko la madaktari ku diagnose magongwa ya sehemu za siri kuwa ni UTI hatakama si UTI.
C: Ongezeko la ngono kinyume na maumbile.
Haya mambo yanahitaji utafiti ili kuja na majibu sahihi, lakini kulingana na jamii na hali halisi. Mawazo yako bado ni sahihi na nitaongezea.
A: Ongezeko la mwanawake wa sikuhizi kushindwa kujisafisha au maji si masafi.
Hapa tatizo laweza kuwa ni kufahamu jinsi ya kujisafisha na kusababisha kuhama kwa bakteria toka njia ya haja kubwa kuja kwenye njia ya mkojo.
B: Ongezeko la madaktari ku diagnose magongwa ya sehemu za siri kuwa ni UTI hatakama si UTI.
1: Hapa kuna tatizo la daktari kuhitaji kipato, ili auze dawa hata kama kioimo si UTI.
2: Tatizo la daktari kutokuuliza dalili nyingine zaidi ili kutofautisha UTI vs STI.
3: Tatizo la mgonjwa kutokueleza vyema dalili zake richa ya kufahamu uwepo wa dalili hizo.
C: Ongezeko la ngono kinyume na maumbile.
Kunaweza kuwa na ukweli hasa kuhamisha wadudu husika
D: Kutokunywa maji ya kutosha ili kupata mkojo mara kwa mara na kuganya wadudu wasipate muda wa kuzaliana zaidi kwenye njia ya mkojo.
E: Matumizi yasiyofaa ya dawa yanayoleta usugu wa wadudu(wagonjwa kujitibia vs utoaji hovyo wa dawa kupitia wataalamu wa afya).
F: Ongezeko la wataalamu wenye ufahamu wa kutambua magonjwa.
G: Ongezeko la upatikanaji wa teknolojia ya kutambua ugonjwa.
H: Tatizo la wagonjwa kutojisafisha kabla ya kutoa mkojo kwaajili ya upimaji.
I: Tatizo la kutokutoa mkojo wa kati, badala ya ule wa kwanza (maelekezo kwa wagonjwa).
J: Matumizi ya visafishio (pads, tampoo, vimiminika nk.) vyenye kemikali na vinapoleta shida hudhaniwa UTI na kujitibia (usugu wa dawa)
K: Wagonjwa kutokumaliza dozi.
L: Wataalamu kutokufuata madaraja ya dawa.
M: Kutojuwepo na mfumi thabiti wa kupata taariga za mgonjwa kwa tiba aliyoipata mwanzo(data nit linked).
N: Kutokuwepo na formal referral systems, mgonjwa anaingia pipote na kutibiwa.
Nk.