Je, huu ni mwendelezo wa Serikali kutudharau Walimu Shule za Msingi?

Nimesoma maoni yote hakuna hata mmoja aliyeonyesha mzizi wa tatizo wote tunamlaumu mtoa mada ,lazima kama wadau wa elimu tujiulize kwa nini tatizo hili litokee ?Nani anatakiwa kulaumiwa ni huyu mwalimu au Serikali?
Wakulaumiwa ni walimu wa shule ya msingi kwa sababu hawatimizi wajibu wao ipasavyo hasa kufundisha zile KKK mwishowe mwanafunzi anafika darasa la saba hajui kusoma wala kuandika sasa kwakuwa mwalimu mkuu anatetea cheo chake anaamua kuiba mtihani mmoja na kuisovu kisha kuwapa majibu wanafunzi wasiojua kusoma wanaingia nayo kwenye chumba cha mtihani.

Muda mwingine walimu hudiriki kujificha chooni na hapo wanakuwa wamewapanga wanafunzi kwamba ukifika muda fulani muombe ruhusa ya kwenda kujisaidia wachache wachache wakifika huko chooni wanapewa vimemo wanaenda navyo kwenye chumba cha mtihani au majibu yanabandikwa chooni wanafunzi wanajifanya wanaenda kujisaidia kumbe wanaenda kukariri hayo majibu na kurudi kwenye chumba cha mtihani.

Matokeo yakitoka unakuta hata asiyejua kusoma kafaulu kwenda form one. Unajiuliza huyu kafaulu vipi? Kumbe ni walimu ndio wanawapa majibu
 
Usilalamike sana inawezekana nanyi mtasimamia sekondari mwezi novemba
 
Nafikiri serikali iko sahihi; lengo kudhibiti hujuma za mitihani.
 
Mwalimu bora anabidi apate division 1 hadi 3 na sio Division four
Mwalimu Bora wa primary ni yule aliyefaulu vizuri mtihani wa primary,
Mwalimu Bora O'level ni yule aliyefaulu vizuri mtihani wa O'level
Kwa aliyepata division 4, anafit kufundisha primary, kwa sababu hio div4 ni ufaulu wa elimu ya O'level sio primary level
 
Wakulaumiwa ni walimu wa shule ya msingi kwa sababu hawatimizi wajibu wao ipasavyo hasa kufundisha zile KKK mwishowe mwanafunzi anafika darasa la saba hajui kusoma wala kuandika sasa kwakuwa mwalimu mkuu anatetea cheo chake anaamua kuiba mtihani mmoja na kuisovu kisha kuwapa majibu wanafunzi wasiojua kusoma wanaingia nayo kwenye chumba cha mtihani.

Muda mwingine walimu hudiriki kujificha chooni na hapo wanakuwa wamewapanga wanafunzi kwamba ukifika muda fulani muombe ruhusa ya kwenda kujisaidia wachache wachache wakifika huko chooni wanapewa vimemo wanaenda navyo kwenye chumba cha mtihani au majibu yanabandikwa chooni wanafunzi wanajifanya wanaenda kujisaidia kumbe wanaenda kukariri hayo majibu na kurudi kwenye chumba cha mtihani.

Matokeo yakitoka unakuta hata asiyejua kusoma kafaulu kwenda form one. Unajiuliza huyu kafaulu vipi? Kumbe ni walimu ndio wanawapa majibu
Msovero una akili ndogo Sana
Nenda shule yoyote ya msingi kachukue takwimu za uwezo wa kkk kwa wanafunzi
Uje useme ni asilimia ngapi watoto hawajui kkk

Kuhusu mitihani kuchitiwa ni tatizo la mwanadamu kote duniani

Wapi hapa duniani mtihani haulindwi?

Nchini Tanzania mitihani yote inalindwa kwa mtutu wa bunduki kasoro mtihani wa darasa la saba

Kuna weakness ktk kulinda mtihani wa darasa la saba

Ukitaka kuamini, Basi tuiombe serikali ilinde mtihani wa darasa la saba na waache huru mtihani kidato Cha 4 kwa waalimu
 
Mleta mada kama ni mwalimu serikali ilikuajiri kimakosa

Hiyo kitu inaitwa segregation of duties

Huwezi kufundisha wewe,utunge mtihani wewe, usimamie wewe na usahihishe wewe!
una akili sana
 
Nipo shuleni ofisini

Mbele yangu Kuna mzigo mkubwa wa daftari za stadi za kazi darasa la tano ninazopaswa kusahisha

Naangalia nje namuona mwalimu wa sekondari yuko bize kusimamia mtihani wa darasa la Saba

Najiuliza kwanini nisisimamie mwenyewe mwalimu wa shule ya msingi?

Je, Serikali imenichukia sana kiasi cha kuninyang'anya majukumu yangu?

Hili limenisikitisha sana nahisi nakosa furaha yangu ya kawaida hapa shuleni

Ni kawaida yangu asubuhi kuwatia moyo watahiniwa kuwa watulivu kisaikolojia ila ukweli leo nimejikuta nimeshindwa kufanya hivyo

Je, huu ni muendelezo wa serikali yetu kutudharau waalimu shule za msingi?
nafikiri mleta mada anasumbuliwa na inferiority complex.
pili ni hasira za kukosa nafasi ya kusimamia hivyo unadhani walimu wa Sekondari wamechukua ridhiki yako.
Hili jambo ni la kawaida sana ktk kutekeleza kazi na hatuwezi kuwapangia baraza la mitihani namna ya kufanya kazi.
lakini zaidi sana ninyi walimu wa shule za msingi mumekuwa waoga kupitiliza, mnapokea maelekezo ya mdomo toka kwa maafisa wenu badala ya kufuata taratibu za baraza.
sasa safari hii angalau baraza limekuja na mwarobaini wa kudhibiti wizi.
na binafsi nimefurahi kwa sabb wengi wa wanaosimamia ni wataaluma na walimu wa sec ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakilalamika kuletewa watoto wabovu. ni fursa nzuri kwao kusimamia kwa weledi ili tupate cream.
mwisho kama mdau wa elimu toka sekta binafsi ninaunga mkono hatua za Serikali kudhibiti wizi huu.
 
Nipo shuleni ofisini

Mbele yangu Kuna mzigo mkubwa wa daftari za stadi za kazi darasa la tano ninazopaswa kusahisha

Naangalia nje namuona mwalimu wa sekondari yuko bize kusimamia mtihani wa darasa la Saba

Najiuliza kwanini nisisimamie mwenyewe mwalimu wa shule ya msingi?

Je, Serikali imenichukia sana kiasi cha kuninyang'anya majukumu yangu?

Hili limenisikitisha sana nahisi nakosa furaha yangu ya kawaida hapa shuleni

Ni kawaida yangu asubuhi kuwatia moyo watahiniwa kuwa watulivu kisaikolojia ila ukweli leo nimejikuta nimeshindwa kufanya hivyo

Je, huu ni muendelezo wa serikali yetu kutudharau waalimu shule za msingi?
Ishukuru serikali imekupunguzia mzigo...Sasa ungeenda kusimamia hiyo mitihani hizo karatasi Stadi za Kazi nani angekisahihishia?
 
Msovero una akili ndogo Sana
Nenda shule yoyote ya msingi kachukue takwimu za uwezo wa kkk kwa wanafunzi
Uje useme ni asilimia ngapi watoto hawajui kkk

Kuhusu mitihani kuchitiwa ni tatizo la mwanadamu kote duniani

Wapi hapa duniani mtihani haulindwi?

Nchini Tanzania mitihani yote inalindwa kwa mtutu wa bunduki kasoro mtihani wa darasa la saba

Kuna weakness ktk kulinda mtihani wa darasa la saba

Ukitaka kuamini, Basi tuiombe serikali ilinde mtihani wa darasa la saba na waache huru mtihani kidato Cha 4 kwa waalimu
Mkuu Nitake radhi kwanza, ningekuwa na akili ndogo ningefeli au ningekuwa form four failure kama walimu wa shule ya msingi. Kuhusu KKK ni ukweli kuwa wengi wenu hamjui kuifundisha mnasingizia kwamba ni mtaala mpya japo serikali inawapa semina za mara kwa mara kuhusu mtaala huo lakini bado ni tatizo ndio maana mtoto anaanza la kwanza anafanya mtihani wa darasa la saba hajui kusoma, kuandika wala kuhesabu lakini cha ajabu eti naye anafaulu kuingia kidato cha kwanza
 
Mleta mada hu stahili kufanya task hiyo Kama unalalamikia viji sent VYA siku 2 tu je akikunia mchafuzi mwenye bungulutu hutachafua kweli wewe!!!???
ENDELEAAA KUSAHIHISHA MALUNDO YAKO
 
Mkuu Nitake radhi kwanza, ningekuwa na akili ndogo ningefeli au ningekuwa form four failure kama walimu wa shule ya msingi. Kuhusu KKK ni ukweli kuwa wengi wenu hamjui kuifundisha mnasingizia kwamba ni mtaala mpya japo serikali inawapa semina za mara kwa mara kuhusu mtaala huo lakini bado ni tatizo ndio maana mtoto anaanza la kwanza anafanya mtihani wa darasa la saba hajui kusoma, kuandika wala kuhesabu lakini cha ajabu eti naye anafaulu kuingia kidato cha kwanza
Labda akili ya kukesha kukariri theories mbalimbali ktk masomo, Ila si akili ya kutathmin Mambo
Na nyie ndo wale wasemao tozo inalipwa na watanzania wote Ila kodi ya TRA inalipwa na wafanya biashara pekee
 
mkuu kua mpole na wewe utaenda simamia mitihani ya form 4, malipo ni hapa hapa dunuani
 
Mshahara wako si uko palepale? Vunga tu achana na hako kaposho ka 120k kasikufanye ukose raha.
 
Back
Top Bottom