Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

mfano mtu anakupa jukumu la uangalizi wa Banda lake la kuku halafu baada ya muda anakuja kukuuliza wamezaliana kuku wangapi unamjibu kuwa hufahamu idadi yake wakati hilo ndilo jukumu lako la msingi; unafikiri mwenye Banda atachukua hatua gani?
Mkuu Sitetei uzembe..Ila tatizo ni Swali ,Wakati na Eneo aliloulizwa..viongozi Wengi bado wanaishi awamu zilizopita..Hivyo swala la uzembe bado lipo..Ila kama huu ndiyo utaratibu mpya Basi tujiandae kwa Maigizo ..
 
Huyu Mama anasimamia;
Afya,
Elimu Sec,
Elimu Msingi,
Utawala,
Ardhi,
Kilimo,
Maji,
Mifugo,
Uhandisi Majengo,
Uhandisi Barabara,
Utamaduni,
Mazingira,
Fedha na Uchumi,
Mipango,
Maliasili, nk

Je anatakiwa kujua Kila Fungu lililoelekezwa humo??
Anatakiwa ajue ujenzi wa barabara tu!! Maana hiyo ndo fahari ya bosi wake.
 
Wanakagera wanajielewa sana ndomaana unaona Meya alivojibu bila kubabaika data zote ziko kichwani ,muda mwingine bilakua na maamuzi ya vile mambo hayaendi.
 
Mi nadhani usimfananishe Waziri na Mkurugenzi mtendaji. Nimefanya kazi Halmashauri, Mkurugenzi alitakiwa kujua Pesa za Road Fund kwa kicwa! Hata kama si kwa kichwa angekuwa na kinote book chenye data mbalimbali. All in all Ushauri tu kwa Rais wangu Mpendwa Atumie lugha ya kistaha kwa mawaziri wake. Nami si kwa Huyu Mama bali kwa Waziri Marawa ambae akimkosa itakuwa ngumu kumpata mtu wa Kariba Ya MH. Dk, Mbarawa!
 
Unadhani Mkuu anafuata hovyohovyo. Anaangalia maantinki iliyoandikwa. Alichokifanya Pascal Mayalla ni Positive Criticism ambazo Mkuu huzifanyia kazi.
 
Ingawa nilimhurumia yule mama lakini DED unapohudhuria ziara za Rais lazima ujiandae kitakwimu kwa vitu vya msingi maana Rais anategemea wewe ndio umpe majibu ya msingi kwenye halmashauri yako. Ni adhabu kubwa lakini italeta changamoto kwa wengine. Mabadiliko yana gharama ..
 
Ni ushenzi sana. DED huwezi kujieleza wakati wewe ndo key player hata meya anakuzidi? then unajitapa wewe ni kichwa, mtaalamu, really?
....I hope unawazungumzia wale ma DED wa awamu zilizopita ambao kabla ya kuwa DED amekuwa mkuu wa Idara na amekuwa anakaimu u DED for many years, so they know every shilling deposited into their account. Kama unazungumzia hawa walioteiliwa majuzi fasta fasta that is something else...
 
Nilishasema humu kwamba: "Three of the hallmarks of bad governance are:
1. Arbitrariness
2. Ambiguousness
3. Capriciousness
 
Naomba kuuliza hivi katika mataifa ya watu walioendelea na kustaarabika, kiongozi unaweza kufanya maamuzi ya kuumiza hisia za wasaidizi wako hadharani na raia wakakushangilia?

Namba wenye majibu wanisaidie.
.....Hahahaaaa wenzetu kwanza kauli zao ....can you please share this ana that? Wako so gentle..
 
Kibongobongo ni sawa tu mkuu. Inaonekana wengi hawafit kwenye nafasi walizopo. Haiitaji kuwa genius kufahamu at least makadirio ya fedha za miradi muhimu. Mfano mradi wa barabara. Ina maana hafanyi kazi yake ipasavyo na pengine vipaumbele vyake ni vya tofauti. Kwasababu angekuwa anafanya kazi yake, angekuwa hata na namba za makadirio au projections kutoka kwenye vikao. Kwasababu pesa zilishafika. Kuambiana humo ndani haijawahi kusaidia.
 
Sina uhakika sana kuhusu hilo la kuwa targeted kisiasa. Lakini kwa upande mwingine ni wazembe.

Au pengine hawajui vipambele muhimu ndo maana tunakwama...

Anashindwa kufahamu pesa za barabara?

Mradi muhimu kabisa?

A very important infrastructure?

Pesa zimekuja, zimefika hadi kwenye idara yeye asijue? Tena mkurugenzi?

Anataka mwaka hazina ndo aulizwe? Au sijui mkuu wa idara?

Ambao wao wanapewa pesa hizo baada ya mkurugenzi kuidhinisha?

Hakukuwepo na vikao vya uamuzi wa fund allocation kuelekea idara mbali mbali?

Kwakweli mimi binafsi nilishangazwa sana kwa uzembe wao mkubwa.

I would’ve fired them too!
 
Amemzalilisha sana huyu Mama Mkurugenzi. Hivi kuwa Rais ni kuwa mkatili namna hii?

Kama sijakosea alimvyonza kama ni kweli tume ya maadili ya viongozi wa umma ipo wapi.

Rais wetu kwa kweli anazalilisha watu. Basi angeishia hapo. Sasa hata inafikia kuvua madaraka?

This now is too much!
 

umeandika maneno meeeengi lakini ni PUMBA tupu. Unamaanisha kuelewa na kukariri ni vitu sawa? Hivi mtu akiulizwa Passport Number yake akasema haikumbuki kwa muda ule, does it mean kwamba haielewi na iwe kosa la kuadhibiwa? si suala tu la kumpa dakika chache anafungua mkoba wake na kukusomea/kukutajia? Issue kubwa JPM anapenda kuabudiwa/kuogopwa/kunyenyekewa. Alitarajia yule Ustaadhat Dau ajibu huku akitetemeka au ikiwezekana akiwa amepiga magoti. Kiutendaji haiku hivyo. Karama ya uongozi haipo kwa JPM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…