Kanisa Katoliki la Mitume linaanzia katika ngazi ya familia. Kama ukibatizwa katika ukatoliki, wewe una jukumu la kuitangaza injili kuanzia kwako, halafu unaenda jumuiya, kanda, parokia, jimbo n.k. Makanisa yanaendeshwa kwa zaka na sadaka, michango ya ujenzi n.k. Sasa wewe jumuiya huenda, kazi iliyopewa na Bwana wetu Yesu Kristu ya kutangaza injili unaofanyika wapi? Huko Kanisani unaotaka kumpeleka mtoto akabatizwe kanisa liliota kama uyoga? Nani analipia umeme? Padre anakula nini? Anavaa nini? Atakuja je kuzika huyo marehemu wako? Wewe ndio mlinzi wa usiku hapo Kanisani! Hivi kama sio kujenga makanisa waumini wote inabidi tutoke huko tuliko Mbagala, Gongolamboto, Tegeta, Kimara, Kigamboni wote twende Msimbazi na St. Joseph au St Peter? Hujui Jumuiya ndio zinajenga makanisa mapya?
Mimi nakuruhusu kwenda unaotaka iwe kwa Mwaiposa, Kakobe, Lusekelo. Wakifa itarudi maana mmiliki hatakuwepo!