Je, huu ni wakati sahihi kwa kanisa Katoliki kubadilika na kuendana na kasi ya makanisa ya Kilokole?

As long as wanasimamia misingi myema mbele ya Mungu, wapo sahihi.
 
Eti nikifa hamniziki 🤣🤣🤣

Kwani mliambiwa lazima nizikwe? Hata kama ni lazima kuzikwa, kwani nyinyi tu ndio mnajua kuchimba makaburi?

Nikifa lazima nizikwe maana bila hivyo nitanuka hadi mkimbie mtaa
Kwani unalazimishwa boss?
 
Toa michango boss.
 
Hamjaanza kuhama leo na bado tunajaza misa ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne na bado kitu mule mule[emoji23][emoji91][emoji91]

We nenda bana. Sisi hatunaga muda na mtu na hutatuona tunaweka nyuzi za kusimanga makanisa mengine.
 
waumin mnachangishwa sijui kujenga shule..shule inajengwa..inakamilika..inaanza kufanya Kazi..BADO tena wanakuja kukusanya sadaka za kuendesha hio shule.
Unamaanisha mkishajenga hayo majengo ndiyo yatalipa mishahara ya walimu, yatanunua chemicals za maabara na vitabu, yatalipa bills za maji na umeme, yatalipa kodi na gharama nyingine za uendeshaji, una maanisha hayo majengo yatajifanyia ukarabati!!?
 
Kanisa langu huwa ni jamii, kwani naeza toa sadaka kwa wasio jiweza, wenye uhitaj, pia jamii ndo itakayo nizika na siyo kanisa. Kanisa halikujui kama huna hela
 
Kama umeona kuna mapungufu ulifanya jitihada gani kusaidia kuyaondoa hayo. Kuhama hama hakutasaidia kwani uendako pia watu wanahama. Dawa ya tatizo ni kulikabili sio kulikimbia. Sisi jumuia yetu tumemwambia paroko kuwa tutachanga tunachoweza wasitupangie viwango maana pesa hawatupi wao, mbona kakubali na maisha yanaendelea.
Uzuri kanisa halizuii mtu kuingia kusali, sijui unatafuta nini zaidi ya hapo. Kuzikwa na padri? Unajua utakufa vipi? Unaweza ukafa hata maiti yako isionekane ndugu. Mambo ya mazishi ni ceremonies za mazoea tu, hakuna uzito wowote kiimani. Alikufa Bob Collymore aliyekua CEO wa Safaricom, mkatoliki. Yeye alitaka mwili wake uchomwe moto. Ukachomwa bila kushirikisha kanisa then the next day wakasali misa ya kumwombea marehemu kanisani.
Tafuta wenzako wenye idea za mabadiliko kama yako mpaaze sauti zenu huenda mkasikilizwa. Kama ndio umeanza kupitia JF safi, utawapata muungane
 
Unamaanisha mkishajenga hayo majengo ndiyo yatalipa mishahara ya walimu, yatanunua chemicals za maabara na vitabu, yatalipa bills za maji na umeme, yatalipa kodi na gharama nyingine za uendeshaji, una maanisha hayo majengo yatajifanyia ukarabati!!?
Na BADO ada inakusanywa kila mwaka...!?? Huo ni ujima
 
Pole kwakuwa ni muhanga katika Imani .Ukifa hakuna anayejijua wakuzike wasikuzike hurudi. Pale. inapopata faraja ya roho ndiyo ilpo Imani yako hivyo ili ufanikiwe nenda kwenye sehemu yenye Uhuru wa kuabudu kwa upande wako siyo kutaka nyingi na saba.
 
Naomba kujua maana ya Sentensi "USIHUKUMU KABLA HUJAHUKUMIWA"
"SAMEHE SABA MARA SABINI"
.......................Ieleweke na hii ipo clearly kabisa kwa muumini anayejua anachoabudu kwamba Kanisa siyo chombo cha kuhukumu/kusamehe dhambi za watu au kulazimisha maiti ikiri uwepo wa Mungu kazi ya Kanisa ni kuwaongoza watu kwenye njia sahihi na kwa ukali ili wamjue Mungu na wajue anataka nini kutoka kwao,Kanisa Catholic halipepesi macho hasa kwenye suala la nidhamu kwenye mambo ya Kimungu na hii kutokumzika mfu hiyo siyo hukumu linachofanya Kanisa ni kujitenga na unafiki wa kuaminisha jamii fulani alikuwa anaamini uwepo wa Mungu hali ya kuwa hajawahi hata mara moja kuonekana akifanya mambo ya Kimungu alikuwa anaishi kichafu chafu tu,(na Kikatoliki mambo ya Kimungu ni pamoja na sala za kila siku zilizoamriwa kama Jumuiya,kufunga ndoa kuhudhuria ibada etc)huwezi kufa kwenye pombe zako huko halafu utegemee Kanisa lije kuaminisha umma kwamba ulikuwa muumini safi na kuisaidia maiti yako kumkiri Mungu.

Huwa nashangaa mtu anayejiita Mkatoliki (kama mleta mada) anashindwa nini kuelewa jambo dogo kama hili na hii inaonyesha ni kwa namna gani hakujua/hajui maana ya imani,wanaojua hata afe baba yao na hakufanyiwa ibada hawashangai ni sheria imewekwa mtafute Mungu ukiwa hai hakuna siku litasimama Kanisa liisaidie maiti yako kukiri uwepo wa Mungu.
 
Siku hizi mi swala la michango tu ndio silielewi, wanajumuia wakigonga hodi kwako hata kama unaumwa usidhani ni kukujulia hali, wanaijia michango....
Na ni michango ya aina nyingi
Upo hapa unalalamika michango ya Jumuiya ambayo hugawanywa kila kaya let's say itoe 25,000/= siyo wewe peke yako na hulazimishwi kuchanga but wakati huo huo una wanao unawalipia school fees 2 millions na wapo watatu na ada hata ipandishwe vipi hulalamiki unalipa ila wakati huo huo unalalamikia kuendeleza pale unapoenda kumuomba Mungu ambaye unaamini anawalinda huko shuleni awasaidie wanao kimasomo halafu unajiita muumini?

Siku wakifeli lawama kwa Mungu ooh why God why God hapo tena yoote unayasahau,watu mnapenda vitu smooth sana hii imani wapo watu wameifia,Mtume Petro amesulubishwa kichwa chini miguu juu wapo waliotumbukizwwa kwenye mapipa ya mafuta yanayochemka lakini Mkristo wa leo unalalamika kutoa 5K mchango wa kupaka Kanisa rangi mimi natamani ifike siku Kanisa liseme yeyote asiyeweza kuziishi sheria za Mungu na Kanisa sawasawa huyo ametengwa,sijisifii ila mimi natoa sana michango na toka nianze kutoa hakuna siku nimekosa kula,kufanya maendeleo yangu binafsi au kuweka akiba ya kutosha.

Mkiambiwa toeni Zaka hamtaki unadhani kwa wingi Makanisa ya Kikatoliki yanaojaza kila mmoja angetoa Zaka kikamilifu kuna ambaye angeombwa atoe mchango wa aina yoyote?
 
Hongera kwa kutoa michango, niombee na mie nipate nitoe.....
 
Wewe wasema tu..hujui kanisa limeanza kufanya reform kwenye misimamo yake ndio mana sasahivi kuna walokole wa kikatoriki wanajiita charismatic..hii yote ni katika kufanya waumini wasiondoke..sema kwakua wewe ni zero brain na kondoo huwezi jua..hakuna kanisa linalotaka lipoteze waumini hata mmoja hakuna kanisa hilo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisa langu huwa ni jamii, kwani naeza toa sadaka kwa wasio jiweza, wenye uhitaj, pia jamii ndo itakayo nizika na siyo kanisa. Kanisa halikujui kama huna hela
Makanisa yanaangilia hela..Mungu wa dunia ni hela tu..tusake pesa..kila dini itakuja kwenye msiba wa nyumbani kwako.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…