VITU VYA KUZINGATIA PINDI UENDAPO KUNUNUA SABUFA (RADIO)
Je, huwa unazingatia nini ukitaka kununua sabufa?
leo nimekuja na elimu bora ya kuwajuza vitu vya kuzingatia ukitaka kununua radio.
wengi wenu hudhani kuwa radio yenye watt kubwa ndo radio bora
.
ukweli ni kwamba
Watt peke yake haitoshi. Kuna mambo
matatu muhimu ya kuzingatia:
- Frequency (Hz)
- Distortion
- Watt.
Frequency (Hz) – Uzito wa bass?
Frequency hupimwa kwa
Hertz (Hz), na inaonyesha
aina ya sauti ambayo sabufa inaweza kutoa.
- Hz ndogo (mf. 20Hz – 50Hz) → sauti nzito sana (bass ya ndani (yaani deep bass)
- Hz kubwa (mf. 100Hz – 200Hz) → sauti ya juu kidogo isiyokuwa na uzito wowote
Sabufa nzuri inahitaji kucheza Hz za chini, kwa sababu:
- Ndiyo zinazotoa mtikisiko wa bas, hapa ndo unasikia tumbo hutetemeka.
kwa hiyo, hakikisha frequency (Hz) inaRange
20Hz – 150Hz bass nzito na safi.
2. Distortion – Usafi wa Sauti (clear sound)
Jumewahi kujiuliza mbona sabufa zingine huwa zina sauti saafi, zinachuja sauti hadi unasema "mashallah
" basi hiyo ndo distortion
Distortion hupimwa kwa
asilimia (%), mara nyingi huandikwa kama:
- THD (Total Harmonic Distortion) nyuma ya radio au kibox chake
Kadiri distortion inavyokuwa:
- Ndogo (mf. 0.1% – 1%) → sauti safi sana, ile yenyewe
- Kubwa (mf. 5% – 10%) → sauti haina mvuto wowote (muddy sound).
N.B Ni bora sabufa yenye Watt ndogo lakini distortion ndogo, kuliko Watt kubwa yenye sauti chafu.
Watt – Nguvu ya Sauti
Watt inaonyesha
nguvu ya sauti, si ubora wa sauti.
Kuna aina mbili muhimu:
Jamani, ubora wa radio (sabufa, soundbar, home theater) haupimwi kwaukubwa wa watt (wattage)
Watt inapima uwezo tu wa radio kufikisha ubora (bass kali, sauti safi) katika umbali flani tu. kwa hiyo watt (power) inasukuma ubora uliopo. kama radio yako ina muddy sound, ffrequency ya chini, watt itasukuma hiyo hiyo.
hivyo basi;
Watt nyingi bila Frequency nzuri na Distortion ndogo = kelele tu.
nazani mmepata funzo kuanzia leo, mtu asikuletee tanganzo la radio kwa kuweka kigezo cha watt kubwa. angalia frequency (Uzito wa bass) na distortion, (clear sound).
HITIMISHO
Sabufa nzuri
si ile yenye Watt nyingi pekee, bali ile yenye:
Frequency ya chini (Hz ndogo) – bass nzito
Distortion ndogo (%) – sauti safi
Watt za kweli (RMS) – nguvu ya kutosha
Ukiona redio au sabufa imeandikwa:
“3000W”
Usikimbilie kununua.
Angalia:
- Inacheza mpaka Hz ngapi?
- Distortion ni asilimia ngapi?