Je, huyu house boy atakuwa anavuta bangi?

Ninaishi nje kidogo ya mji ambako nimejenga kanyumba kadogo tu ka kunisitiri.

Ninaishi na mvulana wa kazi ambaye huwa ananisaidia shughuli za nyumbani kama usafi, kupika, kuangalia nyumba nk

Juzi asubuhi nilikuwa natoka, akanifungulia geti, wakati narudisha gari nyuma nikaona analifunga geti, nikamuuliza mbona unafunga geti? Akanijibu nilidhani umeshatoka.

Jana nimechelewa kurudi, nikakaa getini kama dakika kumi, nimepiga sana honi, hakufungua, nikapiga Simu yake akawa hapatikani.

Nikachukia jiwe na kuanza kugonga geti, hatimaye akaja kunifungulia.

Nikaingiza gari ndani, niliposhuka akaanza kunigombeza kwanini namharibia usingizi, akaenda mbali kwa kusema kuwa kuzurura usiku ni tabia mbaya nitakutana na Malaya wanipe ukimwi.

Leo nimerudi jioni hii, ananiambia gesi imeisha hivyo mtungi ameutupa jalalani.

Uzuri ni kwamba jalala liko humu humu ndani ya uzio.

Hivi huyu angekuwa house boy wako ungemwelewaje?
Mtaishije wawili tu wewe na houseboy? Ndo maana akuogopi.
 
oiii kwan wew ni mwanamke au mwanaume? House boy anakuleteaje habar hizo? Unashindwa kumtia hata makofi kwer? Mim nilikua na shamba boy mmoja akawa ananiletea habari za kunizoea.. Kunasiku nikaingia shamba usiku wa manane nikiwa nimewaka vibaya mno. Akaanza kama kunigombeza. ooh! Mbona unakuja usiku bila hata kunitaarifu. Nilimrukia teke la miguu miwili. nikaingia nae mpaka ndani. Kesho yake asubuh akaomba nauli arudi kwao singida.
 
Ninaishi nje kidogo ya mji ambako nimejenga kanyumba kadogo tu ka kunisitiri.

Ninaishi na mvulana wa kazi ambaye huwa ananisaidia shughuli za nyumbani kama usafi, kupika, kuangalia nyumba nk

Juzi asubuhi nilikuwa natoka, akanifungulia geti, wakati narudisha gari nyuma nikaona analifunga geti, nikamuuliza mbona unafunga geti? Akanijibu nilidhani umeshatoka.

Jana nimechelewa kurudi, nikakaa getini kama dakika kumi, nimepiga sana honi, hakufungua, nikapiga Simu yake akawa hapatikani.

Nikachukia jiwe na kuanza kugonga geti, hatimaye akaja kunifungulia.

Nikaingiza gari ndani, niliposhuka akaanza kunigombeza kwanini namharibia usingizi, akaenda mbali kwa kusema kuwa kuzurura usiku ni tabia mbaya nitakutana na Malaya wanipe ukimwi.

Leo nimerudi jioni hii, ananiambia gesi imeisha hivyo mtungi ameutupa jalalani.

Uzuri ni kwamba jalala liko humu humu ndani ya uzio.

Hivi huyu angekuwa house boy wako ungemwelewaje?
Kitendo cha kunipangia nirudi saa ngapi peke yake kibarua chake kingeota majani muda ule ule asubuhi ni safari ya kurudi kwao
 
Back
Top Bottom