Je, huyu Rais wetu wa sasa ni Vasco Da Gama mwingine? Ziara za nje zimekuwa nyingi sana kama enzi za Awamu ya Nne

Je, huyu Rais wetu wa sasa ni Vasco Da Gama mwingine? Ziara za nje zimekuwa nyingi sana kama enzi za Awamu ya Nne

Kama karudi juzi Mama anasema eti kuna hela sijui umoja wa Ulaya eti ni za kuchangamkia, ni moja ya kauli mbaya kabisa kutolewa na kiongozi ambaye nchi yake ina rasilimali nyingi kuzidi nchi nyingi za Ulaya.

Yaani anatuaminisha sisi ni maskini, yaani kweli anaamini hivyo?

Yaani badala ya kufanya kama Dkt Magufuli ili tujiamini tujifunge mkanda ili nchi yetu iweze kujitegemea yeye anaendekeza eti mikopo mikopo, dah basi tu
 
Kukop
Mama anatakiwa atengeneze long term plan na leadership ambayo haitategemea aina ya rais. Yaani aangalie ni namna gani rasilimali tulizonazo zinaweza ku finance maendeleo yetu. Yeye badala yake anaendq kukopa mikopo ya ujenzi wa madarasa???? Yaani unaenda kukopa hela za kuwekea rehani resources zetu??? Nadhani ile timu ya wachumi angeitumiq ila kwa sasa anapuyanga tu Mama. Mungu atusaidie maana huko mbeleni watoto wetu watatushangaa sana maana watakuta kila rasilimali ya nchi tumekikopea

Kukopa ujenge madarasa ni umasikini wa akili wakishamaliza shule wanakosa ajira.

Kopa jenga miundombinu ya kilimo uchochee uzalishaji export ikue upate mapato ufanye maendeleo.
 
Tangu UHURU ni kukopa tu hivi Hakuna mwenye akili ya kubuni chanzo kingine cha kupata pesa
 
Kukop

Kukopa ujenge madarasa ni umasikini wa akili wakishamaliza shule wanakosa ajira.
Kopa jenga miundombinu ya kilimo uchochee uzalishaji export ikue upate mapato ufanye maendeleo.
Yaani mi mpaka machozi yananitokaga nikifikiria. Sasa hivi nasikia kuna mradi vyuo vikuu eti world bank imeikopesha serikali kujenga miundombinu ya kuongeza idadi ya enrollments vyuoni ili kuongeza idadi ya wanaofika na kumaliza vyuo vikuu Tanzania.

Sasa unajiuliza sasa hivi tu graduate waliopo mitaani bila kazi ni wengi, unaenda kukopa tena ili kuongeza idadi ya graduate wasiokuwa na kazi unategemea nini?

Maana yake hao hao wazungu watakuja tena na mpango wa kukukopesha ili utatue tatizo la migogoro ya vijana wasiokuwa na ajira kuandamana na wakiandamana serikali ikiwapiga itasema ohh demokrasia haki za binaadamu kiasi kwamba nchi inakuwa dependents na nini wanataka wazungu
 
Kusafiri ni kuchezea kodi zetu.
Asiposafiri pia atalalamikiwa, atachekwa na kusemwa vibaya kama alivyosemwa hayati Magufuli.

Waswahili wanasema "maneno huumba" ndio maana kipindi cha JK waPo waliosema Tanzania inahitaji raisi mkali, na mwenye sifa za udikteta dikteta, basi ghafla akapatikana huyo aliehitajika.

Pia wakati wa hayati Magufuli wapo waliomcheka kwa kutokusafiri kwake including na ukali wake, na chembe chembe za udikteta, wakasema raisi ni mkali sana, ana chembe za udikteta na huwa hasafiri kama mwenzie aliepita nk, ghafla akaletwa tena mpole, na msafiri safiri kama watu walivyohitaji.
 
Awamu ya nne tulishudia Jakaya kikwete akifanya ziara za nje huku akisahau kabisa masuala ya ndani ya nchi yake mpaka akapachikwa jina Vasco Da Gama.

Awamu hii nayo naona ni mwendo uleule. Juzi alikuwa ulaya. Leo yupo Uarabuni.

Hii ishu ya Uarabuni asingeweza kuwakilishwa hata na balozi?
View attachment 2131649View attachment 2131650
Uwepo wa rais anayeongea na huyo mwarabu unaonyesha umakini wa Tanzania kulinganisha na ambavyo balozi angekuwa amekalia hicho kiti.

Wakati mwingine hayati JPM alikuwa anawapa mabalozi hizo kazi kwani katika masuala ya diplomasia hakuwa vizuri. Uwepo wa Rais mwenyewe unaonyesha ni kwa namna gani Tanzania inataka kufanya biashara na huyo mwekezaji.
 
Mama anatakiwa atengeneze long term plan na leadership ambayo haitategemea aina ya rais. Yaani aangalie ni namna gani rasilimali tulizonazo zinaweza ku finance maendeleo yetu. Yeye badala yake anaendq kukopa mikopo ya ujenzi wa madarasa???? Yaani unaenda kukopa hela za kuwekea rehani resources zetu??? Nadhani ile timu ya wachumi angeitumiq ila kwa sasa anapuyanga tu Mama. Mungu atusaidie maana huko mbeleni watoto wetu watatushangaa sana maana watakuta kila rasilimali ya nchi tumekikopea
JPM ndiye rais aliyekopa kuliko marais wote tangu uhuru. Yote hayo uliyoyaandika aliyafahamu vyema.
 
Mama anatakiwa atengeneze long term plan na leadership ambayo haitategemea aina ya rais. Yaani aangalie ni namna gani rasilimali tulizonazo zinaweza ku finance maendeleo yetu. Yeye badala yake anaendq kukopa mikopo ya ujenzi wa madarasa???? Yaani unaenda kukopa hela za kuwekea rehani resources zetu??? Nadhani ile timu ya wachumi angeitumiq ila kwa sasa anapuyanga tu Mama. Mungu atusaidie maana huko mbeleni watoto wetu watatushangaa sana maana watakuta kila rasilimali ya nchi tumekikopea
Fedha iliyokopwa haijajenga madarasa tu imeenda pia kwenye miradi ya maji, ujenzi wa vyuo hasa veta, kuimarisha miundombinu kwenye hifadhi zetu, kuimarisha utoaji huduma wa afya kwa ujenzi wa ICU, EMD kununua mitambo
.
Na fedha hii ilikua muhimu kwani iliingizwa kwenye uchumi ili kupunguza maumivu yaliyotokana na janga la uviko-19
 
Hapa naaamini sasa

Kikwete kashikilia usukani

Mama anafuata maelekezo tuu
 
Fedha iliyokopwa haijajenga madarasa tu imeenda pia kwenye miradi ya maji, ujenzi wa vyuo hasa veta, kuimarisha miundombinu kwenye hifadhi zetu, kuimarisha utoaji huduma wa afya kwa ujenzi wa ICU, EMD kununua mitambo
.
Na fedha hii ilikua muhimu kwani iliingizwa kwenye uchumi ili kupunguza maumivu yaliyotokana na janga la uviko-19
Sawa mkuu lakini tatizo letu la msingi kama taifa ni nini???? Kwa nini tusingetumia hizo hela government expenditure zinazochochea uchumi?

Kwa sababu ukiniuliza hayo madara yatarudishaje hela sijui.

Mi nilitegemea wachumi aliowateua wangemshauri
 
Kama karudi juzi Mama anasema eti kuna hela sijui umoja wa Ulaya eti ni za kuchangamkia, ni moja ya kauli mbaya kabisa kutolewa na kiongozi ambaye nchi yake ina rasilimali nyingi kuzidi nchi nyingi za Ulaya. Yaani anatuaminisha sisi ni maskini, yaani kweli anaamini hivyo????? Yaani badala ya kufanya kama Dkt Magufuli ili tujiamini tujifunge mkanda ili nchi yetu iweze kujitegemea yeye anaendekeza eti mikopo mikopo, dah basi tu
Me naami kifo Cha Magufuli si tuu mafisadi walifurahi hata viongozi aliokuwa nao madarakani walifurahi
 
Back
Top Bottom