Mkuu sio kila unachogugo kipo sawa, wakati mwingine ishirikishe akili yako hata kidogo.
Mabomu 2000 yenye uzito wa kilo 910 jumla ni kilo 1,820,000. Hizo ni tani 1820.
Ndege kubwa Boeing 747-400ER max take off yake ni 412,770 kg (Tani 412.77) na Airbus A380 ni tani 575 (575,000 kg).
Antonov Mriya 225 MTOW ni tani 640 (640,000 kg) na hii ndo ndege kubwa kulilo zote duniani.
Sasa mkubwa ndege gani hiyo ya kivita ambayo inauwezo wa kubeba mzigo wa tani 1,820??
Maana hata strategic bomber ya US B-52 ina MTOW ya tani 216.
So, sio kila kitu unakiandika kama ulivyokiona. Nini kazi ya ubongo sasa??