MrFroasty
JF-Expert Member
- Jun 23, 2009
- 1,195
- 595
Angalizo lako halina ukweli wowote, katika uwanja wa kimataifa unaheshimika zaidi ukikumbatia lugha yako. Mataifa mengi yenye heshima zake kama ufaransa, china, urusi n.k. Watu wanazungumza lugha zao na mitaala yao yote wameweka kwenye lugha zao.Natamani sana nami GENTAMYCINE nijue Kuongea Kiingereza kizuri kama cha akina Nyerere na Mkapa na siyo nije nikijue vizuri baada ya Kustaafu Majukumu yangu au niwe nakiongea kwa kutegemea Kuandikiwa kisha kila nikiwa nahutubia niwe 'nazuga' kwa Kukiongea kwa Sekunde Tano, nakunywa Maji na nakohoa ili kuwaonyesha wanaonisikiliza kuwa nakijua kisha narejea tena Kusoma huku nikiwa natetemeka na kila mara.
ANGALIZO
Kujua Kiingereza si lazima kwani Kiswahili, Kizanaki na Kinyarwanda kinatosha na wala kujua Kiingereza si kipimo cha ama Mtu kuwa Msomi (Intellectual) au Mwerevu (Brainiac) katika Jamii ila katka Uga wa Kimataifa na kwa Heshima ya Lugha ya Kiingereza tokea enzi na enzi kutokujua Kiingereza (Kiswahili cha duniani kama alivyowahi kusema Mwalimu Nyerere) wakati hata 'Mitaala' yetu ya Elimu ni ya Kiingereza kunaweza Kutafsiriwa ni Uwendawazimu na Unafiki usiovumilika.
Yapo pia mataifa madogo kama uholanzi, norway n.k. Mataifa yao wanasomesha watoto wao lugha ya kiengereza, ni maamuzi ya mtu kuamua kurahisisha kutumia kiengereza. Lakini hii haina uhusiano wowote na heshima, ni maamuzi ya mtu na confidence yake.