Je, ilikuwa sahihi kwa Rais kuiasa hadharani familia ya Mzee Mwinyi isigombane?

Mkuu nadhani kifo na maziko ni fundisho si kwa waliiofiwa bali wa jumuiya yote, mama anaihasa familia ya Mwinyi lakini pia ni ujumbe kwa familia nyingine.
 
Huu ni uchochezi.

Mara nyingi migogoro ndani ya familia huchochewa na watu wa nje kama vile marafiki, majirani na wale wanao jinasibisha kuwa ndugu wa mbaaali.

Familia ya Hayati Mzee Mwinyi ni miongoni mwa familia zenye kujiheshimu na wanajitambua, hii ni kutokana na msingi mzuri walio pewa na Mzee.

Tuiache familia ifanye mambo yao, tuache chokochoko.
 
Hii stori nimesoma nikajikuta nasikitika na kuilewa zaidi kauli aliyoitoa mfalme Daudi katika WAH:1:2....Ubatili mtupu, asema Mhubiri, ubatili mtupu; yote ni ubatili . Mtu ana faida gani ya kazi yake yote anayoifanya chini ya jua? Kizazi kimoja kinapita, na kizazi kingine kinakuja, lakini dunia hudumu milele
 
Kumbe kuna mengi huyajui
 
Sio mbaya, na yeye si ajabu anayajua ya ndani kuliko sisi wa mitandaoni, na ukizingatia pale kwenye umati wa watu kuna MASHEIKH wakubwa, hivyo italeta nguvu ndani ya familia.

Allah awasimamilie hao Ndugu zetu, na awaepushe na wabaya
 
Marais wa nchi hii kuropoka ndio kazi yao hasa kwenye misiba ya watu mfano kwenye msiba wa komba ifahamike komba alikuwa na wake 4 alikuwa kazaa nao lakini watoto walio kuwa wana julikana kifamilia ni watoto wa wake 2 tu Magufuli alipo simama kutoa nasaha akasema hivi watu wengi wanafahamu kuwa komba kazaa wanawake 2 tu jambo ambalo sio kweli akasema mimi nivyo fahamu kazaa na wanawake wengine 2 hivyo kuna watoto wasio fahamika kifamilia bahati nzuli wale wanawake walikuwepo

Pale na watoto wao ikawa sababu ya kutambulika naisi watakuwa walimwambia Magufuli kusema maneno hayo hata mama shishi si ajabu upende wa mke mdogo umemwambia asema hivyo
 
Magu 😂😂
 
Kun umuhim kuoa mke mmoja aisee.
 
ALiyeongea ni Rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…