Je, inawezekana kila kitu ni mpango wa Mungu?

Ukishasema mtazamo utabaki kuwa ni mtazamo tu na uthibitisho ni kitu kingine,yawezekana huo mtazamo ndio ukawa ukweli wenyewe au sivyo.
Mtazamoulioukweliukipimwa kuthibitishwa utaonekana kuwa ukweli?
 
Mkuu unajuaje kiongozi wasasa ni maridadi? Unaweza kujua miaka kumi ijayo huyu wasasa atazalisha kitu gani?


Kama huyu wa sasa ameweza kuleta maendeleo kwa kipindi hiki kifupi tu na bado ana nia ya kuleta zaidi ya hapa, sasa jiulize tutakuwa wapi baada ya miaka 10 ijayo? Kumbuka si Mwinyi wala Mkapa na Kikwete walijaribu kuleta maendeleo hapa nchini kwani kila mmoja wao alikuwa bize kulitaifisha hili taifa. Hatujawahi kuwa na rais maridadi kama huyu tuliyenaye na ndiyo maana waafrika wengi wanamlilia akatawale kwao.
 
Mungu hajadiliwi kama imani tu JF, anajadiliwa mpaka kama fact.

Ukitakakujadii habari za Mungu kamaimani nenda kwenye nyumba yako ya ibada (kanisani, msikitini etc) au kaa kwako umjadili, sitakufuata.

JF ni public square.

Mungu wako hayupo,unaweza kutengeneza imani kwamba yupo, lakinihilo halimaanishi yupo.

Hayupo.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha kwamba yupo.
 
Hadi hapo haujaona kuna utofauti kwamba kuna uthibitisho na Mtazamo na ndiyo kitu nachokizungumzia hapa?
Katika set theory kuna union, intersection, set na subset.

Unaweza kuwa na mtizamo uliosubset ya uthibitisho, maana yake, mtazamo wote upo ndani ya uthibitisho.

Kama vile unavyoweza kuwa na mkoa wa Dodoma ulio katika nchi ya Tanzania.

Maana yake ukiwa katika sehemu yoyote ya mkoa wa Dodoma, upokatika nchi ya Tanzania.

Sasa wewe unachosema ni kwamba, mtizamo hauwezi kuwa ndani ya uthibitisho.

Unasema kwamba mkoa wa Dodoma ni mkoa wa Dodoma tu, hauwezi kuwa ndani ya Tanzania, kwa sababu wenyewe ni mkoa wa Dodoma.

Mimi nakwambia Bunge la Tanzania lipo Dodoma, hivyo lipo nchini Tanzania.

Wewe unabisha, unasema Bunge halipo nchini Tanzania, lipo Mkoa wa Dodoma.
 
Wewe kama nani hapa JF hadi uzuie kujadili imani???
 
Mkuu watu wakila wakivimbia wanabana pua na kusema hakuna Mungu, kwanza tu jinsi watu wanvyo kutana na wenza wao wa ndoa ni ajabu tupu.
 
Kwa nini Bwana Mungu na si Bibi Mungu?

Huoni Bwana Mungu ni mfumodume wa watu tu wamejipangia?
Enenda zako Shetani wewe! imeandikwa; "kila dhambi watakazofanya wanadamu chini ya jua watasamehewa, lakini dhambi ya kumtukana ROHO MTAKATIFU haitasamehewa kamwe, siyo katika ulimwengu huu wala ule ujao".

Uu nani wewe unayeweza kumjadili MUNGU kama vile uwajadilivyo wanadamu wenzako??? Hivi kweli kinyago cha udongo kinaweza kumjadili yeye aliyekichonga?? Hivi chombo cha udongo kinaweza kumjadili yeye aliyekifinyanga??
 
Kwahiyo kila kitu ni mpango wa Mungu?
 
Hoja yangu mtazamo ni mtazamo na uthibitisho ni uthibitisho.

Sasa wewe ulitoa mfano hapa et umeliona kabisa jua linawaka halafu useme et kwa mtazamo wako jua linawaka,kwanini utumie neno mtazamo na sio kusema tu jua linawaka maana ni kweli jua linawaka?
 
Unahubiri na kukemea, lakini hujathibitisha Mungu yupo bado.
 
Kwa sababu inawezekana unafikiri unaliona jua linawaka, kumbe unaangalia TV nzuri sana ambayo imewekwa kama dirisha kukuonesha jua linawaka.
 
Unaanza kunichosha tu,tatizo ulazimisha mtazamo uwe ndio uthibitisho wakati tumeshaona kuna uthibitisho na Mtazamo.

Mimi kwa mtazamo wangu naweza kusema wewe ni mwanamke lakini pengine sio mwanamke ni mwanaume, uthibitisho ndiyo utafanya niweze kujua bila shaka kuwa wewe ni mwanamke au mwanaume.
 
Wapi nimesema nazuia kujadili imani?

Tatizo hata kusoma hujui, unataka kujadili uwepo wa Mungu!
We ndio hujui unachokieleza.

Unvyosema nikajadili kanisani au msikitini,maana yake nini? ina maana hapa hautaki pajadiliwe imani bali ni huko msikitini na kanisani tu.
 
Kwa sababu inawezekana unafikiri unaliona jua linawaka, kumbe unaangalia TV nzuri sana ambayo imewekwa kama dirisha kukuonesha jua linawaka.
Vizuri sana na ndiyo maana nasema kuna mitizamo na uthibitisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…