Hapana.
Ngoja nikupe darasa.
Katika mantiki (logic) kuna kosa moja la kimantiki linaitwa "non sequitur". Mtu akifanya kosa la "non sequitur"katika kufikiri kimantiki maana yake anafanya kosa la kuunganisha mambo mawili ambayo hayana uhusiano.
Mathalani.
Nikiuliza, ubini wako nani wewe? Ukasema "Ramadhani". Nikasema, aaaah, kumbe wewe ni Muislamu. Hapo nimefanya kosa la "logical non sequitur".
Nimeunganisha vitu viwili ambavyo havina uhusiano wa moja kwa moja kama vitu ambavyo vina uhusiano wa moja kwa moja.
Nimechukulia kwamba, mtu mwenye ubini wa Ramadhani ni lazima atakuwa Muislamu.
Kumbe kuna Mchungaji Jaji Augustino Ramadhani!
Ndilokosa ulilofanya wewe hapa.
Mfano mwingine wa kihesabu.
Umeniuliza, square root ya 2 ni ngapi? Nikasema sijui. Ukasema basi kama hujui, square root ya 2 ni 10.
Nikakwambia jibu lako si la kweli, ni la uongo. Square root ya 2 haiwezi kuwa 10.
Unaniambia, sasa wewe hujui square root ya 2 ni nini, nikikwambia ni 10 utanibishiaje wakati hujui square root ya 2 ni nini?
Hujui kwamba, naweza kuwa sijui square root ya 2 ni nini, lakini nikajua kwamba square root ya 2 ni ndogo kuliko 2, na ukinipa jibu lolote la square root ya 2 ambalo nikubwa kuliko 2, nitajua ni jibu la uongo, lina contradiction. Lina contradict principle ya muhimu kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.
Ukisemakwamba kama sijui asili yangu na babu zangu siwezi kuelewa kwamba Mungu yupo na ndiye asili, ni sawa na kuniambia kwamba, kamasijui square root ya 2 ni nini, siwezikuelewa kwamba square root ya 2 ni 10.
Naweza kujua square root ya 2 si 10 bila kujua square root ya 2 ni nini, kwa kujua tu kwamba square root ya 2 inatakiwa iwe ndogo kuliko 2, isi contradict principle kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.
Naweza kuwa sijui asili yanguwala ya mababu, lakini pia nikajua asili yetu si Mungu na Mungu hayupo, kwa sababu dhana nzima ya kuwepo Mungu ina contradiction kama vile dhana ya square root ya 2 ni 10 ilivyo na contradiction.
Ndiyo maana huwezi ku prove factually kwamba Mungu yupo.
Kwa sababu hayupo.
Unaweza ku prove Mungu yupo, factually?