Je, inawezekana kila kitu ni mpango wa Mungu?

Mabaya yapokwa sababu hakuna Mungu wa kuyazuia.

Kamamabaya hayana nafsi ya kuelewa na utashi wa kusema yatafute faida gani, kuuliza mabaya yanapata faida gani ni sawa na kuuliza "Mlima Kilimanjaro unapata faida gani kuwa Kilimanjaro"?

As if Mlima Kilimanjaro usipopata faida fulani Kilimanjaro utahama na kwenda kukaa Fouta Djalon kwenye faida zaidi!
Mkuu kumbe unaujua mlima Kilimanjaro! Hivi asili yaule mlima ni wapi?
 
Mungu huyo alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya na wala hauhitaji mabaya ili watu wasiwe na haja ya kuogopa mabaya, kwa sababu mabaya hayapo na wala hayawezi kufikirika kabisa?

Alishindwa kuumba ulimwengu huo?
Angeumba ulimwengu huo bado wewe ungehoji je ameshindwa kuumba ulimwengu wenye mabaya ndani yake na akaumba ulio na mema
 
Hapana. Nisingehoji.

Nahoji kwa sababu huu una contradiction.

Huo usingekuwa na contradiction hivyo usingekuwa na cha kuhoji.

In fact mimi si ninayehoji. Dhana ya kuwepo Mungu inajihoji na kujichanganya yenyewe kabla sijatia neno.

Mimi naonesha tu dhana inavyojichanganya. Hata nisingeonesha bado ingekuwa inajichanganya tu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Kiranga kwa kilugha chetu inamaanisha Shetani. Sasa nashindwa ni kwa namna gani nifanye uache ubishi maana ukweli unaujua mwenyewe. Mungu unamjua na nguvu zake unazijua ila kwa vile uashaasi subiri hukumu yako siku zinahesabika!!
 
Suala hapa ni kutofautisha kati ya mtazamo na uthibitisho.

Suala la mtazamo uwe sahihi au sio sahihi ni suala lengine ila uthibitisho na mtazamo ni vitu tofauti,hilo lazima liwekwe sawa kwanza maana umekuwa ukipotosha sana.
Uthibitisho hauwezi kuwa mtazamo uliosahihi?

Nikilitazama jua, linawaka, nikasema kwa mtazamo wangu jua linawaka hapa,na kweli jua linawaka, huomtazamo wangu hauendani na ukweli na hivyokuwa mtazamo sahihi ambao pia upo katikauthibitisho kwamba jua linawaka hapo nilipo?
 
Wewe unajionesha kuwa umedandia jambo usilolijua,nakwambia hivi suala la kwamba kuna Mungu ni imani.

Sasa kama wewe unajadili suala la uwepo wa Mungu tofauti na kwamba ni jambo la imani basi tambua umepotea njia.

Yani hao unaojadiliana nao kuhusu fact unawatambua kama waamini Mungu halafu hapa unasema haujadili imani bali fact.

Wewe una matatizo kwa kweli.
Imani haijadiliwi, ukishaingia katika mjadala, huku unafikiri unajadili imani, wewe ndiye uliyepotea njia.

Kuna watu kibao hawajadili imani zao hapa, kwa sababu wanajua suala zima la kujadili imani ni mufilisi wa mawazo.

Mimi najadili facts, sijadili imani.

Imani unaruhusiwa kuamini chochote unachotaka.

Lakini, katika facts, Mungu hayupo.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha kwamba yupo factually
 
Kiranga kwa kilugha chetu inamaanisha Shetani. Sasa nashindwa ni kwa namna gani nifanye uache ubishi maana ukweli unaujua mwenyewe. Mungu unamjua na nguvu zake unazijua ila kwa vile uashaasi subiri hukumu yako siku zinahesabika!!
Thibitisha Mungu yupo.
 
Uthibitisho hauwezi kuwa mtazamo uliosahihi?

Nikilitazama jua, linawaka, nikasema kwa mtazamo wangu jua linawaka hapa,na kweli jua linawaka, huomtazamo wangu hauendani na ukweli na hivyokuwa mtazamo sahihi ambao pia upo katikauthibitisho kwamba jua linawaka hapo nilipo?
Uthibitisho upi hasa unautaka wewe. Nitolee mfano thibitisha kwamba wewe ni mwanadamu na si mbuzi? Pia unapinga uwepo wa Mungu je unajua duniani kuna vitu kama mapepo,mizimu,majini na mashetani?
 
Wewe huna hoja,kifo na sababu za kifo ni vitu viwili hivyo. Kifo sio udhaifu kwamba ukiona mtu kaumwa akafa au kapata ajari na kufa ukadhani kuwa suala la kifo lipo kwa kuwa kuna vitu kama hivyo,kwa maana hiyo visingekuwepo hivyo vitu na kifo kisingekuwepo.

Na ndiyo maana kwako wewe unaona kifo ni udhaifu.
Kifonikitu kibaya au kizuri kwako? Akija mtu akwambie akuue sasa hivi, utafurahi au uta[pinga habari hiyo?
 
Uthibitisho upi hasa unautaka wewe. Nitolee mfano thibitisha kwamba wewe ni mwanadamu na si mbuzi? Pia unapinga uwepo wa Mungu je unajua duniani kuna vitu kama mapepo,mizimu,majini na mashetani?
Hahaah dah wejamaa siyo mchezo!!
 
Uthibitisho upi hasa unautaka wewe. Nitolee mfano thibitisha kwamba wewe ni mwanadamu na si mbuzi? Pia unapinga uwepo wa Mungu je unajua duniani kuna vitu kama mapepo,mizimu,majini na mashetani?
Mimi si binadamu, binadamu maana yake mtoto wa Adamu. Mimi siamini kwamba huyo Adamu alikuwepo, sasa utatakaje mimi nithibitishe kwamba mimi ni bin Adamu wakati mimisiamini kwamba Adamu alikuwepo?

Usifikiri kwamba unavyoamini wewe kila mtu anaamini hivyo!

Unaweza kuthibitisha kwamba kuna mapepo, mizimu, majini na mashetani?

Na kama yapo, unawezaje kuthibitisha kwamba kuwapo hayo kunathibitisha Mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo? Hujathibitisha kwamba huyo Mungu yupo.
 
Hapana. Nisingehoji.

Nahoji kwa sababu huu una contradiction.

Huo usingekuwa na contradiction hivyo usingekuwa na cha kuhoji.

In fact mimi si ninayehoji. Dhana ya kuwepo Mungu inajihoji na kujichanganya yenyewe kabla sijatia neno.

Mimi naonesha tu dhana inavyojichanganya. Hata nisingeonesha bado ingekuwa inajichanganya tu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Ndio Mungu yupo ila kwa sasa siwezi kuthibitisha alipo sababu sijui yuko wapi kwa sasa ila yupo,,kama wewe nikikuuliza trump yupo na unaweza kunithibitishia yupo
 
Uchawi ni nini kwanza ?

Tujuzane unapotaja "uchawi" unamanisha nini kabla sijakujibu kama upo au haupo?
Uchawi (kwa Kiingereza "Witchcraft") ni nguvu zinazotumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansikatika jamii nyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.

Lengo lake ni kujaribu bahati ya mtu na kujilinda na maadui wengine kimazingara, au kwa ajili ya kujifurahisha, japo wenye imani potofu hulichukulia maanani na kupandikiza chuki kwa ndugu jamaa hata jirani kuwa ni mchawi.
 
Ndio Mungu yupo ila kwa sasa siwezi kuthibitisha alipo sababu sijui yuko wapi kwa sasa ila yupo,,kama wewe nikikuuliza trump yupo na unaweza kunithibitishia yupo
Hata hujui tofauti ya "thibitisha mungu yupo" na "thibitisha Mungu yupo wapi".
 
Uchawi (kwa Kiingereza "Witchcraft") ni nguvu zinazotumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansikatika jamii nyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.

Lengo lake ni kujaribu bahati ya mtu na kujilinda na maadui wengine kimazingara, au kwa ajili ya kujifurahisha, japo wenye imani potofu hulichukulia maanani na kupandikiza chuki kwa ndugu jamaa hata jirani kuwa ni mchawi.
Unaweza kuthibitisha uchawi upo na si hadithi tu?

Babu zetu walipowaona wazungu wana redio, na wanaweza kutabiri kupatwa kwa jua, waliwaita wachawi.

Je, kutumia redio ni uchawi? Kuweza kutabiri kupatwa kwa jua ni uchawi?

Unajuaje kwamba unachofikiri wewe ni uchawi leo si kitu ambacho kinaweza kuelezewa vizuri tu kesho bila uchawi kama leo tunavyoweza kuelezea redio na kupatwa kwa jua, vitu ambavyo babu zetu waliviona uchawi, bila kuhitaji nadharia ya uchawi ?
 
Mimi si binadamu, binadamu maana yake mtoto wa Adamu. Mimi siamini kwamba huyo Adamu alikuwepo, sasa utatakaje mimi nithibitishe kwamba mimi ni bin Adamu wakati mimisiamini kwamba Adamu alikuwepo?

Usifikiri kwamba unavyoamini wewe kila mtu anaamini hivyo!

Unaweza kuthibitisha kwamba kuna mapepo, mizimu, majini na mashetani?

Na kama yapo, unawezaje kuthibitisha kwamba kuwapo hayo kunathibitisha Mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo? Hujathibitisha kwamba huyo Mungu yupo.
Ok, mkuu nijuze kadri ya uelewa wako
1.Ni nini asili ya viumbe Duniani,vinaendeshwa na nani na nguvu toka kwa nani?
2.Unaelewa nini juu ya mwili, Roho,Nafsi,Uzima na Kifo?
3. Kabla ya vitu hivyo unavyoviona kulikua na nn na nini hatima yake?
4. Kila kilicho na mwanzo huwa na mwisho je ni nini mwanzo wa wa hii dunia na mwisho wake ni nini?
Kwa kunjibu hayo maswali naomba sasa uthibitishe kwamba Mungu hayupo.
 
Mimi si binadamu, binadamu maana yake mtoto wa Adamu. Mimi siamini kwamba huyo Adamu alikuwepo, sasa utatakaje mimi nithibitishe kwamba mimi ni bin Adamu wakati mimisiamini kwamba Adamu alikuwepo?

Usifikiri kwamba unavyoamini wewe kila mtu anaamini hivyo!

Unaweza kuthibitisha kwamba kuna mapepo, mizimu, majini na mashetani?

Na kama yapo, unawezaje kuthibitisha kwamba kuwapo hayo kunathibitisha Mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo? Hujathibitisha kwamba huyo Mungu yupo.
Adamu maana yake ni damu yaani kwa kifupi mwana wa damu watu wote ni wana wadamu sababu damu ndiyo uhai wetu, labda wewe useme hutumia damu, kwahiyo huwezi kukwepa kutokuitwa binadamu.
 
Back
Top Bottom