Wewe mkuu tumia akili kidogo za kuzaliwa na utaelewa nini kilifanyika. MUNGU amekupa akili na anategemea utazitumia akili zako vizuri. Iko hivi; dhambi ni kama sumu inayoharibu mwili wote taratibu, sasa kama mwili ukiharibika ina maana hata mbegu za uzazi pia zinaharibika, sababu mbegu za uzazi ni sehemu ya mwili. Mbegu hizi za uzazi ambazo tayari zinakuwa zimeshaharibiwa na dhambi ndizo hizo hizo zinazotungisha mimba na mtoto anazaliwa. Matokeo yake kila anayezaliwa anakuwa ni UZAO WA DHAMBI, na dhambi ni maangamizi, ndiyo maana kuna magonjwa, njaa, vita, umaskini na hata kifo.
Aliyeichagua dhambi ni Mwanadamu mwenyewe, kwa hiari yake mwenyewe akachagua kutenda dhambi. Hata wewe umeshatenda dhambi nyingi tu tokea umezaliwa mpaka leo. Kwa umri wako huo ulionao unajua fika tofauti ya dhambi na mema, lakini kwa sababu ya kiburi bado unaendelea kutenda dhambi kila siku. Mbaya zaidi unamlaumu MUNGU kwa matendo yako mwenyewe.
Lakini kama ukiamua kuacha kutenda dhambi kabisa na kujitenga na uovu, hilo linawezekana kabisa sababu ni hiari yako tu. Hakuna mtu au malaika au shetani mwenye uwezo wa kukulazimisha wewe utende dhambi, kila kitu ni maamuzi yako mwenyewe!