Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Jambo la imani halihitaji uthibitisho, linahitaji kuamini.Wewe usioamini Mungu na wenye kuamini Mungu,kama mnajadili suala la uwepo wa Mungu nje ya kuwa ni jambo la imani basi hamtakuja kuelewana hapa.
Na wewe unatumia mwanya huo kusema hakuna Mungu na ndiyo maana hawawezi kuthibitisha kwa sababu umelitoa suala la uwepo wa Mungu kama jambo la imani.
Sitaki imani, ukiamua kufuata imani, utajuaje imani yako ni sahihi au si sahihi bila uchunguzi? Na ukifanya uchunguzi kuhakiki imani yako kama ni ya kweli au la, bado upo kwenye imani au unatoka kwenye imani na kwenda kwenye uthibitisho?