Ndiyo maana imani hailazimishwi,unaweza kuamua kuamini au usiamini.
Kwa hivyo suala la kwamba je Mungu kweli yupo kama tunavyoamini au hayupo tunaamini jambo si la kweli?
Naweza kujibu kuwa itakuja kudhihirika kama ilivyo dhihirika kwa imani ya Einstein.
Hivyo sitegemei tena wewe kulazimisha upewe uthibitisho.
Sijadili imani, najadili fact.
Ukisema unaamini Mungu yupo, sina mjadala nawe.
Nimesema mara nyingi sana hapa kwamba.
1. Natetea haki za watu tofauti kuamini imani tofauti, hata zile ambazo sikubaliani nazo.
2. Misingi ya haki ya kuamini unachotaka ipo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.Naikubalina kuithamini.
3. Misingi hiyo ilikuwapohata kablaTanzania haijakuwapokamanchi, iliwekwakatika Azimio linaloheshimika kabisa duniani "Universal Declaration of Human Rights" la December 10 1948. Azimiohili nalipenda sana na kulithamini sana.
Hivyo, sina nia ya kumuingilia mtu katikaimani yake.
As long as anakubali hiyoniimani.
Abudu chura, mti, kichaka cha kwenu, kivyako. Mradi usije anga zangu kusema unachoamini ndiyo ukweli wenyewe (fact).
Ukishanihubiria ama hapa JF ama popote, au kusema unachoamini ni kweli (fact) ushatoka kwenye uwanja wa imani, umekuja kwenye uwanja wa uthibitisho.
Umeshajianika kuulizwa maswali na kutakiwa kutoa uthibitisho.
Hapa sijadili imani, najadili fact.