Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kuna wakati huwa nafikiri ama wanajifanya hawaelewi makusudi kwa kile wanasaikolojia wanachokiita "cognitive dissonance", ama watu tuko na tofauti za msingi katika ubongo kiasikwamba unaweza kuwaonesha watu wawili rangi ile ile (metaphorically speaking0 mmoja akasema nyekundu na mwingine akasema bluu, kwa sababu zile zile.haha hahha aiseee ...kuna watu wanavichwa vigumu sana ""... mkuu huwa unatirilika vyema mnooo"".. ajabu ni kwamba "" maswali ambayo huwa unaulizwa Humu ""ulishawahi kuyapatia majibu yake mara 8000" lakini hawakomi bado wanarudia kuuliza tu "" ilhali majibu Yke " walishapatiwaga""...
We angalia.
Unamuuliza mtu kwanini anasemaMungu yupo?
Anakujibu kifo. Kifoni sababu tosha kusema Mungu yupo.Watu wameshindwa kuzuia kifo, kwahiyo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Wakati, ukiangalia, kifo ni sababu ya kusema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo. Angekuwepo,kwa nini aruhusu kifo kiwatenganishe viumbe wake wanaopendana sana? Baba na mtoto, mama na mtoto, baba na mama, marafiki etc.. Huyu Mungu ana ukatili gani mpaka aruhusu kifo?
Mwingine anakwambia complexity ya duniainaonesha lazima kuna muumba, complexity haiwezi kutokea bila muumba.
Wakati, ukishasema complexity haiwezi kutokea bila muumba, maana yake muumba naye ni complex na yeye hawezi kuwepo bila muumba. Ukisema complexity haiwezikutokea bila muumba ushakubali Mungu hayupo, kwa sababu Mungu naye kamakaumba vitu complex, na yeye ni complex na hivyo atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, ad infinitum, ad absurdium.
Sasa hapo utaona watu tulivyo tofauti na sababu zile zile zinavyomfanya mmoja aseme Mungu hayupo, na mwingine aseme Mungu yupo.