Je, inawezekana kila kitu ni mpango wa Mungu?

Je, inawezekana kila kitu ni mpango wa Mungu?

Kama anaweza kuthibitisha, hakuna tatizo.

Kamahawezi kuthibitisha,tatizoni "false advertisement".

Nisawa na mtu kukuuzia muhogo, halafu anakwambia huu muhogo ni dawa ya UKIMWI.

Lazima athibitishe. Asipoweza kuthibitisha anakuwa tapeli anayeweza kuhatarisha maisha ya watu. Kuna watu watapata matumaini feki kwamba muhogo dawa ya UKIMWI na kufanya ngonozembe wakijua muhogoutawaponya, halafu wakafa kwa vile muhogo hauponyi UKIMWI.

Thibitisha muhogounaosema unaponya UKIMWI unaponya UKIMWI kweli.

Kama hujathibitisha, unafanya "false advertisement".

Thibitisha Mungu yupo kweli.

Kama hujathibitisha, na unasemayupokweli, unafanya "false advertisement".
Nimeuliza hivi "mtu akisema anachoamini ni kweli" hapo tatizo lipo wapi?

Mtu ana haki ya kuamini na anaona anachokiamini ni jambo la kweli,hapo kuna kosa gani?

Hayo ya kutangaza dawa ya ukimwi ni masuala mengine kabisa hayana uhusiano na mtu kusema anachokiamini ni jambo la kweli.
 
Mbona unarudia swali ambalo nimelijibu kirefu tu katika bandiko ulilolinukuu?

Unaelewa kwamba ukisema unaamini maana yake unakubali kwamba unajipa nafasi kwamba imani yako inaweza ikawa si kweli, na hivyo kusema "naamini ni kweli" ni sawa na kusema "nakubali kwamba imani yangu inaweza kuwa si kweli, lakini ni ya kweli", na kwamba kauli hii inajipinga yenyewe, ni contradiction, ni oxymoron?

Unaelewa hili?
 
Bado hujajibu upotovu ni nini?
Upotovu ni kukubali kitu ambacho sicho, mfano wake ni kuamini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo wakati dhana ya kuwepo Mungu huyo inajipinga yenyewe. Angekuwepo, dunia isingekuwa na baya lolote.

Kama unabisha, thibitisha Mungu huyo yupo.
 
Wewe siyo mpotovu unaepinga hakuna Mungu? Ni kwanini binadam wote tuna muundo wa viungo sawa?
 
Mbona unarudia swali ambalo nimelijibu kirefu tu katikabandiko ulilolinukuu?

Unaelewa kwamba ukisema unaamini maana yake unakubali kwamba unajipa nafasi kwamba imani yako inaweza ikawa si kweli,na hivyo kusema "naamini ni kweli" ni sawa na kusema "nakubalikwamba imaniyangu inaweza kuwa si kweli, lakini ni ya kweli", na kwamba kauli hii inajipinga yenyewe, ni contradiction, ni oxymoron?

Unaelewa hili?
Haujajibu nilichokuuliza,we ulileta mambo ya kutangaza dawa ya ukimwi na ndiyo hayo uliyokuwa ukiyazungumzia.

Haujajibu ni vp inakuwa kosa mtu kuona kile anachoamini ni kweli na kusema anachokiamini ni kweli?
 
Wewe siyo mpotovu unaepinga hakuna Mungu? Ni kwanini binadam wote tuna muundo wa viungo sawa?
Hujathibitisha Mungu yupo.

Binadamu wote hatuna muundowa viungo sawa, kunawengine wana vidole sita.

Na kama binadamu kuwa sawaunafanya ndiyo sababu ya kuonesha Mungu yupo,basi unaonesha sababu ya kusema Mungu hayupo.

Kuna warefu na wafupi, weusina weupe.

Wengine wanazaliwa na vilema, wengine hawana vilema.

Wengine wanahitaji miwani kuona, wengine wanaona bila miwani.

Wengine wana makaliomakubwa, wengine viflatscreen.

Wengine wanazaliwa wawili wameungana pamoja,wengine wanazaliwa mapacha laikini hawajaungana.

Wengine wanazaliwa na moyo mkubwa tunawachangia waende India kufanyiwa operation, wengine wana mioyo ya kawaida.

Kwa hivyo, hoja yako inaonesha Mungu hayupo zaidi ya inavyoonesha Mungu yupo.

Kwa sababu si kweli kwamba watu wote tunazaliwa na viungo sawa.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo woet angekuwepo, asingewapendelea wengine wazaliwe na afya, na kuwapotezea wengine wazaliwe na vilema vya maisha.
 
Haujajibu nilichokuuliza,we ulileta mambo ya kutangaza dawa ya ukimwi na ndiyo hayo uliyokuwa ukiyazungumzia.

Haujajibu ni vp inakuwa kosa mtu kuona kile anachoamini ni kweli na kusema anachokiamini ni kweli?
Kwa sababu claim ya kitu kuwa kweli inataka uthibitisho.

Kama unaweza kuthibitisha imani yako nikweli, hakuna tatizo.

Kama huwezi, unafanya claims ambayo huwezi kuithibitisha. Sasa tutajuaje kwamba wewe si tapeli tu?
 
Kwa sababu claimya kitu kuwa kweli inataka uthibitisho.

Kama unaweza kuthibitisha imani yako ni kweli, hakuna tatizo.

Kama huwezi, unafanya claims ambayo huwezi kuithibitisha. Sasa tutajuaje kwamba wewe si tapeli tu?
Ukishasema imani hauwezi tena kuniambia nithibitishe,ndiyo maana wewe unasema hapa haujadili imani.

Halafu hayo ya utapeli yameingiaje hapa? maana utapeli ni kosa.
 
Mungu ana macho, masikio, na roho ngapi? Mungu kama baba anaweza sikiliza watoto wote wa duniani kwa masikio hayo mawili kwa wakati mmoja? Je, ni mpango wa Mungu kuleta magonjwa kama polio, ukimwi, cancer, malaria na mengine yanayopeleka watu kila kukicha bila kufikia umri mkubwa?

Mwenyezi Mungu kabebeshwa mizigo mpaka wana Siasa wanaofanya kazi za Kaizari wanataka awaangalie? Ya Mungu tungemuachia na ya Kaizari yakaendelea. Ndiyo maana tulisema Serikali haina dini. Inaudhi wabunge na mawaziri kupoteza muda kuanza kushukuru Mungu wakijua katiba yetu haina dini.

Mungu yupo rohoni mwako siyo yule wa kusingizia kwa kila kitu. Uendeshe gari umelewa ugonge uue eti kazi ya Mungu??????
 
Sasa kama unatambua hivyo kunawengine wanazaliwa hivyo kwa nini wewe usishukuru kuzaliwa ukiwa na afya tele?
Mjadala si kuhusu mimi. Mimi nikishukuru au nisiposhukuru si muhimu. Mimi ni mtu mmoja tu.

Mjadala wa muhimu kabisa ni kuhusu kuwapo kwa Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote.

Kama yupo, na unatumia usawa wa viungo vya watu kama uthibitisho kwamba yupo, huoni kwamba wanaozaliwa vilema wanaonesha hayupo?

Kwa nini Mungu mjuzibwa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao watu wengine wanazaliwa wazima, wengine wanazaliwa vilema?

Mungu gani wa upendeleo hivyo?

Alishindwa kufanya watu wote wazaliwe bila vilema?
 
Ukishasema imani hauwezi tena kuniambia nithibitishe,ndiyo maana wewe unasema hapa haujadili imani.

Halafu hayo ya utapeli yameingiaje hapa? maana utapeli ni kosa.
Nakwambia uthibitishe kwa sababu umesema ni kweli.

Unheaema ni imani yako tu, hata sina sababu ya kukutaka uthibitishe.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Au umechanganyikiwa tu hujui tofauti ya imani na fact?
 
Back
Top Bottom