Je, inawezekana kila kitu ni mpango wa Mungu?

Mkuu punguza mwemko! Hatugombani, sema wewe asili ya binadamu ni wapi?
Unachoona wewe muhemko, kwangu hata chafya hakijafika, kwa nini unaona muhemko?
Ni kwa sababu hujazoea rigorous examination na passioante debate?

Unaelewa kwamba wewe kuuliza swali ambalo huna jibu au ambalo mtu yeyote hana jibu lake ni ishara kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?

Kwa sababu angekuwepo, asingekuwa mchoyo hivyo kutupa maswali bila kutupa majibu?

Unaelewa nikisema sijui asili ya binadamu ni nini hilo halithibitishi Mungu yupo?

Unaelewa kwamba naweza kusema sijui asili ya mtu, halafu nikasema kwa uhakika mtu asili yake si Mungu na Mungu hayupo?

Unajua kwamba ukiuliza habari ya asili ya hiki ni nini, asili ya kile ni nini, hata nikikukubalia ni Mungu, halafu nikakuuliza asili ya Mungu ni nini hutaweza kunijibu?

Unaelea kwamba hunijibu maswali yangu, unaniuliza yako tu?

Unaelewa kwamba hunijibu maswali yangu kwa sababu habari zako za Mungu kuwepo si za kweli na ukitaka kujibu maswali yangu, hilo litaonekana?

Unaelewa hayo?
 
Shida maswali yako tiyar ya majibu napia yana zalisha maswali mengine. Mfano unasema hujui asili ya mwanadamu! Na unakaza shingo hakuna Mungu, na unakubali mwanadamu kazaliwa! Hapo huoni kama unajikoroga?
 
Shida maswali yako tiyar ya majibu napia yana zalisha maswali mengine. Mfano unasema hujui asili ya mwanadamu! Na unakaza shingo hakuna Mungu, na unakubali mwanadamu kazaliwa! Hapo huoni kama unajikoroga?
Naweza kusema sijui asili ya mtu na hapo hapo nikasema asili yake si Mungu. Mungu hayupo.

Naweza kutojua njia fupi kabisa ya kutoka Dar es salaam kwenda Bagamoyo, lakini nikajua haipitii Kilwa Kivinje.

Naweza kuwa sijui jibu la swali, lakini nikipewa jibu potofu nikajua hili potofu.

Naweza kuwa sijui square root ya 2 ni nini, lakini ukaniambia ni 10 nikajua jibublakonsi sahihi.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuthibitisha.

Kwa sababu hayupo.
 
Kwasababu tiyar unajibu lako, hata ukionyweshwa huwezi kukubali.
 
Kila ulichojaribu kukitaja kama huzuni kwako kina mbadala wake

Na kitu kinachoitwa shida ni kulingana na Mtu na ufahamu wake

Lunch yako wewe ya matatizo inaweza ikawa bajeti yangu ya mwezi isiyo na Masumbuko
 
Imani maana yake nini?

Nikisema nakuja nyumbani kwako, nina imani(sina hakika) upo kunipokea na sitakuta mlango umefungwa na hakuna wa kunipokea, maana yake nini?

Maana yake nina hakika upo?

Au sina hakika upo?
Hivi hata wewe hapo umeelewa nini Kiranga?

Labda ungeeleza wewe mwenyewe hapo maana yake nini.
 
Kwasababu tiyar unajibu lako, hata ukionyweshwa huwezi kukubali.

Wwanasaikolojia wana kitu kimoja wanakiita "projection".

"Psychological projection is a defense mechanism people subconsciously employ in order to cope with difficult feelings or emotions. Psychological projection involves projecting undesirable feelings or emotions onto someone else, rather than admitting to or dealing with the unwanted feelings."

Psychological Projection: Dealing With Undesirable Emotions

Projection ni kuchukua tabia yako, halafu mumlalamikia mtu mwingine kwamba anayo.

Kama wewe mwizi, utalaumu wengine kwamba ni wezi.

Ndicho ulichokifanya hapa, huenda bila kujua. Wewe ndiye unakataa majibu kwa sababu una jibu lako, lakini umenipakazia mimi kwamba niko hvyo.

Nitanyambulisha ka mifano, kitu ambacho wewe hujafanya.

Wewe ndiye una jibu lako la kwamba Mungu yupo, hata nikikuonesha kwamba Mungu hayupo hukubali.

Hata ukianza kusema Mungu yupo kwa sababu watu wote wanazaliwa na viungo sawa, nikikuonesha watu wanazaliwa bila mikono na kukuambia habari zako ni potofu, hutaki hata kukubali kwamba umekosea.
 
Kila ulichojaribu kukitaja kama huzuni kwako kina mbadala wake

Na kitu kinachoitwa shida ni kulingana na Mtu na ufahamu wake

Lunch yako wewe ya matatizo inaweza ikawa bajeti yangu ya mwezi isiyo na Masumbuko
Mungu alishindwa kuumba dunia ambayo haina mabaya, na haiwezekani kuwa na mabaya, ina mazuri tu?

Hujajibu swali hili.

Unaliruka tu.
 
Unaweka mada na kuihusisha biblia kisha unakataa na kusema isihusishwe na dini...ajabu sana
 
Hivi hata wewe hapo umeelewa nini Kiranga?

Labda ungeeleza wewe mwenyewe hapo maana yake nini.
Imani maana yake ni kukubali jambo bila kuwa na hakika.

Unakubali au unakataa?
 
Mi Mungu yupo sababu matendo yake yapo, Mara nyingi nimekuomba ulete ushahidi kama Mungu hayupo umeshindwa kuleta, unakiri tu mtu kazaliwa kilema! Hao wazazi wa huyo kilema wametoka wapi? Au wewe mwenyewe ulitoka wapi?
 
Mi Mungu yupo sababu matendo yake yapo, Mara nyingi nimekuomba ulete ushahidi kama Mungu hayupo umeshindwa kuleta, unakiri tu mtu kazaliwa kilema! Hao wazazi wa huyo kilema wametoka wapi? Au wewe mwenyewe ulitoka wapi?
Matendo yote unayisema yanaonesha Mungu yupo, unasema hivyo kwa sababu hujayachambua kwa undani.

Umesema Mungu yupo kwa sababu watu wote wanazaliwa na viungo sawa.

Nikakwambia kama watu wote kuzaliwa na viungo sawa kunaonesha Mungu yupo, basi Mungu hayupo.

Kwa sababu kuna watu wanazaliwa bila viungo.

Unakubali hilo?

Ukiuliza watu wanatoka wapi, kama vyote vilivyopo ni lazima viwe na chanzo kwenye kingine, nimekuuliza Mungu naye katoka wapi?

Hujajibu.

Hujibu maswali yangu.

Hukubali pale ambapo unakosea wazi kabisa.

Unalazimisha hoja.

Kwa sababu huyo Mungu unayemsema yupo, hayupo.
 
Mungu hayupo!!!!duh
 
Mungu alishindwa kuumba dunia ambayo haina mabaya, na haiwezekani kuwa na mabaya, ina mazuri tu?

Hujajibu swali hili.

Unaliruka tu.
Kuwa na mazuri tupu Bila mabaya

Ni sawa na hesabu ya Jumlisha bila ya Toa

Thamani ya kitu isingepatikana
 
Mungu hayupo!!!!duh
Mtu anakwambia Mungu yupo. Kwa sababu watu wote wanazaliwa na viungo sawa.

Wakati hajui kwamba kuna watu wanazaliwa bila mikono.

Ukimwambia kwa msingi huo, Mungu hayupo.

Kwa sababu kuna watu wanazaliwa bila mikono.

Hataki hata kukubali kwamba kakosea.

Ubishi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…