Je, inawezekana kuhamisha unit za umeme wa Single phase kutoka meter moja kwenda meter nyingine?

Je, inawezekana kuhamisha unit za umeme wa Single phase kutoka meter moja kwenda meter nyingine?

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Nimebadilisha matumizi ya umeme kutoka Single phase system kwenda 3 phase system, kwenye remote meter ya single phase system nilibakiza units kama 700 hivi, naweza kuziamishia kwenda single phase nyingine ya jengo jingine?

Maana naambiwa Unit za single phase haziwezi kutumika kwenye 3 phase na kama inawezekana nini steps za kufanya hili unit ziweze kuhamishwa?
 
Habari, Ndugu Mteja,

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu kuhusu suala hili. Tulikumbana na changamoto ya muda katika akaunti yetu, lakini kwa sasa huduma zimerejea katika hali ya kawaida.

Iwapo bado hujapata majibu ya suala lako, tunapenda kukufahamisha kuwa huduma hiyo inawezekana kutekelezwa. Utaratibu wake ni kwamba mteja anatakiwa kuandika barua ya maombi ya Unit Transfer, akiambatanisha na vielelezo vinavyoonyesha salio la unit lililokuwepo kabla ya uhamisho.

Katika barua yako zingatia vifuatavyo: Anuani kwenda kwa meneja TANESCO, wilaya yako, majina kamili, namba ya simu, namba ya mita, mkoa, wilaya, kata pamoja na eneo ulilopo. Baada ya kuandika barua hiyo utaipiga picha au scan kisha tuma kupitia ukurasa huu kwa msaada zaidi.

Asante kwa uvumilivu na ushirikiano wako. ^HN​
 
Back
Top Bottom