Je inawezekana kusoma CPA na kufanyiwa recategorization bila kua na degree ya uhasibu?

Kwa mtu ambaye tayari ni muajiriwa, na anataka kusoma degree nyingine, je aanze na uhasibu then CPA ndio afanyiwe recategorization, au haiwezekani kusoma CPA bila kua na degree ya uhasibu? Kama ilivyo school of law? Maana school of law ni lazima mtu amalize bachelor ya LLB?.
Inawezekana kabisa,,ukiwa na CPA unakuwa mhasibu,ila ukiwa na degree tu unakuwa afisa hesabu
 
usiingalie E, angalia kuwa HR kibao hawajui kuwa ukiwa na CPA meant tayari una degree ya uhasibu ndani yake.Kuna watu nawajua wana CPA na recategorization hawafanyiwi kisha wanaambiwa degree ya Uhasibu hawana (naongea in practical sense kama huamini kamuulizee DHRo wako)
2. Kuipata CPA sio rahisi kiivyo inahitaji dedications
3. Ukiwa mhasibu Halmashauri huitaji E ili uishi, kama matumizi yako sio ya anasa na ukiwa na heshima kwa wakuu wako na bidii utakuwa unakula posho posho zilizohalali hutaitaji mshahara ili uishi
4. Mhasibu Halmashauri anapata pesa kuliko Medical doctor (collectve kibunda)
Sawa asante, hicho ndio kinanikimbiza ualimu, maana baada ya kuchukua mshahara ndio basi tena mpaka Mwisho wa mwezi.
 
Watu wanatoka sekondari na wanazipata wala hupiti chuo boss.
Mkuu Kuna NTA LEVEL UNAFANYA MITIANI.
Ndio unapata sifa za kufanya mitiani ya CPA
Unaweza kumaliza secondary na ukaanza kufanya mitiani ya bodi kuanzia ngazi za Chini mpaka kufikia kupata CPA..
NB.
Sio lelemama au sandakalawe au ndiki ndikiki ni mchakato Kuna VIGEZO ili upate qualifications for sitting for CPA EXAMS

Ntaweka humu ngoja nipekue pekue makabrasha..

✌️
 
hao HR au DHRO akili mgando hawaelewi, hata walioko Mkoani hawaelewi
Kuna jamaa aliapata kazi toka sekretariati ya AJIRA akiwa na Intermediate stage ambayo ni degree in Accounting nakwambia alikataliwa, issue ikafika mkoa akakataliwa, ikarudi Dodoma ndio ikawa solved.

Hili jambo pia linawakuta wanausoma Procurement na kupata award za Board zao pasipo kuwa na degree za chuo
Tutofautishe kati ya sheria na mtu ambaye either ana chuki zake binafsi au mahaba yake; hao waliokua wanakataa huko wilayani na mkoani is either walikua na personal internet or walikua na mtu wao standby somewhere akiwa anasubiri wampe mchongo
 
usiingalie E, angalia kuwa HR kibao hawajui kuwa ukiwa na CPA meant tayari una degree ya uhasibu ndani yake.Kuna watu nawajua wana CPA na recategorization hawafanyiwi kisha wanaambiwa degree ya Uhasibu hawana (naongea in practical sense kama huamini kamuulizee DHRo wako)
2. Kuipata CPA sio rahisi kiivyo inahitaji dedications
3. Ukiwa mhasibu Halmashauri huitaji E ili uishi, kama matumizi yako sio ya anasa na ukiwa na heshima kwa wakuu wako na bidii utakuwa unakula posho posho zilizohalali hutaitaji mshahara ili uishi
4. Mhasibu Halmashauri anapata pesa kuliko Medical doctor (collectve kibunda)
Asante sana kwa ushauri.
 
Mshahara wako kama una degree ya walimu ni uleule hautofautian na degree ya uhasibu the same kama una diploma. Tofauti idara ya fedha halmashauri ndiyo roho kwahyo malupulupu kibao.
Tunapambana kuyafata hayo malupulupu boss, kuliko kupasuka mwezi kwa mwezi bora hayo malupulupu, hata ukipata 10,000 sio mbaya kulipo kwenda job hupati hata 100
 
Nina degree ya ualimu masomo ya physcis na mathematics.. nilitaka kusoma uhasibu open ndio nikaingiziwa ilo wazo la kusoma CPA, maana CPA halmashauri wanaanza na E, kwahiyo sitarudishwa nyuma sana.

Soma CPA straight kupitia stage za Atec.

Achana na mambo ya university utapoteza hela na kujichosha tu.

Kwa mtu aliyesoma PCM na akafaulu hata kwa div 2. Hawezi kufeli masomo ya CPA. Maana physics imeshamkomaza akili
 
Kwa mtu ambaye tayari ni muajiriwa, na anataka kusoma degree nyingine, je aanze na uhasibu then CPA ndio afanyiwe recategorization, au haiwezekani kusoma CPA bila kua na degree ya uhasibu? Kama ilivyo school of law? Maana school of law ni lazima mtu amalize bachelor ya LLB?.
Kwa kua wewe ni Optimists lolote linaweza kutokea! Una ngekewa
 
Mkuu Kuna NTA LEVEL UNAFANYA MITIANI.
Ndio unapata sifa za kufanya mitiani ya CPA
Unaweza kumaliza secondary na ukaanza kufanya mitiani ya bodi kuanzia ngazi za Chini mpaka kufikia kupata CPA..
NB.
Sio lelemama au sandakalawe au ndiki ndikiki ni mchakato Kuna VIGEZO ili upate qualifications for sitting for CPA EXAMS

Ntaweka humu ngoja nipekue pekue makabrasha..

✌️
Ok mkuu, weka kwa msaada wa wanaohitaji wasije wakadhani ni rahisi kama kumaliza drs 4 shule ya kata.
 
Soma CPA straight kupitia stage za Atec.

Achana na mambo ya university utapoteza hela na kujichosha tu.

Kwa mtu aliyesoma PCM na akafaulu hata kwa div 2. Hawezi kufeli masomo ya CPA. Maana physics imeshamkomaza akili
Shida ni moja HR Wengi hawatambui CPA kwenye recategorization, wanataka bachelor ya uhasibu kwanza ndio maana nikauliza, kusoma sio shida saana maana msuli nauweza vizuri tu.
 
Back
Top Bottom