Hii mada ni nzuri kwa sisi wagonjwa watarajiwa (ofcourse kila mtu anaugua), sema mmeingiza ubishi wa kitaalamu mpaka mnatupoteza sasa.
Binafsi natumia dawa zote, za asili na hizi za Western, na zote zinanisaidiaga sana tu. Za kiasili nazitumia zaidi kama kinga, mfano ukitumia limao kama kinga kama Deception anavyosema ni kweli malaria unaweza usiisikie kabisa. Mi naweza kukaa zaidi ya miaka 2 bila kuugua malaria, naaminiga ni kwa sababu natumia sana limau pamoja na madawa mengine ya asili. Ikitokea nina malaria huwa natumia kwanza dawa za hospitali, nikimaliza dozi ndo naendelea na mambo yangu ya limau n.k.
Huwa naamini dawa za hospitali zinafanya kazi fasta, wakati hizi za asili ni slow, so za asili nazitumiaga kama kinga tu. Hivyo mimi kama mtumiaji naelewa vizuri anachozungumza Deception na pia naelewa vizuri wanachoongea kina georgeousmimi na madaktari wengine.
Kwahiyo badala ya kubishana mi ningewaomba chonde chonde mjikite kwenye kutoa uzoefu wenu ktk kutibu haya magonjwa ili mtusaidie sisi wagonjwa. Otherwise, mtakuwa mnatuchanganya zaidi na hayo maneno yenu ya kitabibu ndo kabisaa, mwishowe uzi utabaki wenu tu maprofessionals
Safi sana mito;Wewe sasa umenielewa ,na umenielewa kwa kuwa umeshajijengea attitude ya kutaka kuelewa,hongera kwa hilo.Huwa najisikia raha sana kupata watu kama ninyi.Kama umenifuatilia sawasawa utaona kwamba mimi sipingani na kila tiba za magharibi,bali hupingana na baadhi ya tiba fulani tu za magonjwa fulani na si zote.Hata mimi huwa natumia tiba za magharibi wakati fulani kuwa dawa zake ziko katika concentrated form ambapo huleta majibu kwa haraka zaidi.
Na ndio maana nilitoa angalizo kwa mwana JF mmoja kwamba anatakiwa atumie limao kama kinga kwa sasa na si tiba,sikutaka kueleza mambo yote kwa nini nimemwambia hivyo,ila kama hata limao utalifanyia extract likawa kwenye concentrated form pia linaweza kutumika kama tiba kama zilivyo dawa nyingine za malaria.Ni kasumba za kimagharibi tu ndizo zimetuharibu.
Sasa madaktari wanakuja hapa wanakimbilia kupinga tu bila kuhoji,mimi nilitegemea nimepata watu waelewa wa kwenda nao sambamba kwenye uzi huu kumbe hawana tofauti na wale wengine wanaopenda kupinga bila kuhoji.Sisi inatuwia vigumu kutengeneza extract zetu wenyewe kwa sababu nyingi sana ambazo nikianza kueleza sitamaliza,unaweza kuandika kitabu.
Wachina wana dawa zao za kutibu magonjwa mbalimbali kama malaria nk kwa kuwa wana uwezo wa kutengeneza hizo extracts,hivyo wachina wengi hawatumii dawa za magharibi.Watu wanakurupuka na kuja kupinga tu bila kuhoji,mbona mimi sikupinga tiba za magharibi zaidi ya hizi za magonjwa ya ki-propaganda?
Mimi niliona yule jamaa kafanya jambo jema kuwaita madaktari humu kumbe ndio wamekuja kuharibu tu,hawajui hata pa kuanzia kuhoji na badala yake hukimbilia kupinga mambo wasioyajua.Kweli wasomi ni wengi lakini waelimika ni wachache sana.