Je, inawezekana ukahamisha makaburi na yasitokee madhara?

Je, inawezekana ukahamisha makaburi na yasitokee madhara?

Nimenunua kiwanja pembeni kina makaburi matatu, ni kipande cha mita tatu kwa tatu, sasa nawaza niyahamishie sehemu nyingine huko ili nipate nafasi kubwa zaidi ya kiwanja, nimekuja kwenu ili nijue kama kuna madhara yoyote au la.


Hakuna madhara yoyote ya kuhamisha makaburi kwa ajili ya jambo la kimaendeleo isipokuwa tu ni lazima zifanyike taratibu zote za kisheria au makubaliano ya wahusika wa hayo makaburi nk.
 
Nikiongea na wahusika ili wahamishe wenyewe je?
Muhimu ni ridhaa yao watoe ruhusa hata ukihamisha wewe,watu,au wao haina shida.
Wao ndo watapendekeza wapi wapeleke kama ni makaburini au shambani.
Ila ni lzm uchukue kibali police na ubakie na kopi.
 
Unataka usumbue marehemu halafu wakuache salama

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Jokes
 
Kiwanja cha milioni 3.5 nihamishe makaburi kwa milioni 6 = 9.5M,rudisheni pesa zangu.
Labda kama unatumia kampuni hapo haizidi laki 3.
Tafuta vijana wa Kazi za makaburini ndio fani yao.
Baada ya zoezi unapatakasa hapo kwa imani yako Ili kuziondoa roho zilizopo
 
Sisi tumehamisha na hakuna kilichotokea
 
Nimenunua kiwanja pembeni kina makaburi matatu, ni kipande cha mita tatu kwa tatu, sasa nawaza niyahamishie sehemu nyingine huko ili nipate nafasi kubwa zaidi ya kiwanja, nimekuja kwenu ili nijue kama kuna madhara yoyote au la.

Wasiliana na serikali ya kijiji, wilaya, mkoa au halmashauri...

Hizo mambo za kuhamisha makaburi husimamiwa na serikali...
 
Mtatizo mengine huwaga mnajitaftia tu.
Makaburi si yakuish nayo, ni vile tu hii nchi mipango miji ni hovyo.

Kuhamisha makazi ya wafu huo ni upuuzi maana inakuwa ni dharau na kashifa, hata wew hupendi kusumbuliwa ukiwa umelala, je kwanini uwasumbue hao waliopp kaburin?

Uza icho kiwanja katafte mahala pengine, na nikuonye ole wako uharibu ama uhamishe hayo makaburi, majibu utayapata baada ya muda, na hakika utarudi hapa kutupa ushuhuda na kuomba ushaur wa jinsi ya kuwakimbia mizimu..ole wako kijana, be respectively kwa waliolala

Si ajabu hapo unapoishi sasa ni eneo la makaburi lililotumika miaka hata 100 na zaidi nyuma...

Na hakuna kitu chochote kimekutokea
 
Hakuna madhara... Watu wanafukua watu wa kale...
 
Watu wakifa na jambo lao limeisha, kama hakuna jambo la kisheria kuyahusu wewe ondoa tu, acha uoga.
 
Aiseee hao jamaa wana njaa kiasi gani kuuza kiwanja chenye miili ya ndugu zao, inaumiza yaani na wewe huoni kama unawadhalilisha hao wafu hata kama hawajitambui, fikiria hiyo scenario itokee kwa wapendwa wako..Bora ingekuwa ujenzi wa barabara au umeme maana ni kwa manufaa ya wengi ila mitoto yenye njaa na tamaa inauza utu wa wazazi au ndugu zao ..SHAME ON THEM
 
Uataribu wa watu kuzika katika viwanja vyao hasa huku mijini ni changamoto ambayo itakuja kuwa na madhara mbeleni hasa enwo likihitaji kuendelezwa, kwa mfano kwa dar es salaam inasemekana karibu eneo kubwa lilikuwa makaburi na ilibidi yahamishwe kupisha uendelwzwaji wa maeneo mbalimbali.
Itakuwa vizuri kama serikali ikikataza mara moja suala la kuzika katika viwanja na kuweka eneo maalum kwa ajili ya makaburi kuepuka adha hizo za mleta mada.
 
Back
Top Bottom