Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Hatuwanasibishi waarabu na wayahudi ila tunawanasibisha na Ismail(عَلَیهِ‌السَّلام).

Ama wewe una ushahidi wowote kuwa waarabu si kizazi cha Ismail(عَلَیهِ‌السَّلام)?
Leta ushahidi wa kihistoria unaonyesha huo uhusiano ila uhusiano kati ya wayahudi na Ismael upo wazi na Ukitaka ujue ni uongo ndo maana unasema sijui Kuna waarabu wa aina mbili yaani kuwe na waarabu aina mbili harafu aina moja tu ndo ihusishwe na wayahudi?
 
1. Pomponius Mela (Karne ya 1 BK) – De Chorographia

Reference: Mela, Pomponius. "De Chorographia." (Karne ya 1 BK)

Pomponius Mela, mwanajiografia wa Kirumi, aliandika kuhusu Waarabu wa Arabia Deserta na akasema walikuwa watu waliotokana na uzao wa Ismail.

Kulingana na maelezo yake, Waarabu wa kaskazini mwa Arabia walihusiana na kabila la Adnani, ambalo linahusiana na Ismail (A.S.).

2. Diodorus Siculus (Karne ya 1 KK) – Bibliotheca Historica

Reference: Diodorus Siculus. "Bibliotheca Historica" (Book 3, Chapter 44). Translated by C.H. Oldfather. (Loeb Classical Library)

Diodorus Siculus, mwanahistoria wa Kigiriki wa karne ya 1 KK, aliandika kuhusu historia ya dunia na akataja kwamba Waarabu wa Arabia Deserta walitokana na Ismail (A.S.).

Aliandika kuhusu Makka na kusema kuwa ilikuwa sehemu muhimu ya biashara iliyojulikana kwa Waarabu wa kale.

3. Strabo (Karne ya 1 BK) – Geography

Reference: Strabo. "Geography" (Book 16, Chapter 4). Translated by H.C. Hamilton & W. Falconer. (Loeb Classical Library)

Strabo, mwanajiografia na mwanahistoria wa Kigiriki, aliandika kuhusu Waarabu na akataja makabila yao, akisema kuwa walihusiana na maeneo ya Hijaz, hasa Makka.

Alielezea kuwa Waarabu wa kaskazini walikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na familia ya Ismail, ingawa hakumtaja moja kwa moja.

4. Ptolemy (Karne ya 2 BK) – Geographia

Reference: Ptolemy. "Geographia" (Book 6, Chapter 7). Translated by J. Lennart Berggren & Alexander Jones.

Claudius Ptolemy, mwanajiografia wa Kigiriki, aliandika kuhusu maeneo ya Arabia na akataja makabila kadhaa ya Waarabu wa Kaskazini, ambao walihusiana na nasaba ya Ismail (A.S.).

Katika ramani zake za dunia ya kale, Ptolemy aliorodhesha Makka na maeneo ya karibu kama sehemu muhimu za kabila la Waarabu wa Adnani.

5. Theophanes the Confessor (Karne ya 9 BK) – Chronicle

Reference: Theophanes the Confessor. "Chronicle." Translated by Cyril Mango & Roger Scott.

Theophanes, mwanahistoria wa Byzantine, aliandika kuwa Waarabu walikuwa "watu wa Ismail", na alielezea kuwa Waarabu wa Kaskazini walihusiana na Makka.

Aliandika kuwa kabla ya Uislamu, Waarabu walikuwa na mila zao zilizoelekezwa kwenye maeneo matakatifu yaliyoanzishwa na nasaba ya Ismail.
 
Katika historia, kumekuwa na mijadala kuhusu kama maandiko ya zamani yalitabiri ujio wa nabii wa mwisho. Watu wengi wamechunguza vitabu vya kale wakitafuta dalili zinazoelezea mtu atakayekuja na mwongozo wa kiroho kwa mataifa yote. Katika makala hii, tutaangalia aya mbalimbali kutoka Injili zinazoonyesha utabiri wa ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

1.Kumbukumbu la  Torati 18:18 -  Nabii  kama Musa

"Nitawainulia nabii kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18)

Katika aya hii, Mungu anamwambia Musa kwamba nabii mwingine kama yeye atainuliwa kwa watu. Wanazuoni wanaeleza kuwa nabii huyu:
Atakuwa kutoka kwa ndugu wa Waisraeli → Ikiwa Waisraeli wanahusiana na Isaka, basi ndugu zao wa karibu ni kizazi cha Ismaili, ambacho kilizaa Waarabu.

Atakuwa kama Musa → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na Musa wote walikuwa manabii waliopokea sheria mpya na waliongoza jamii zao kwa mwongozo wa Mungu.

Atakuwa na maneno ya Mungu kinywani mwake → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alipokea Qur’an kwa ufunuo wa Jibril, kama Musa alivyopewa Taurati.

2.Isaya 42:1-13 -  Nabii  kutoka Kedar

Katika sura hii ya Isaya, kuna maelezo kuhusu mtumishi wa Mungu ambaye atakuwa nuru kwa mataifa yote:

Isaya 42:1 – “Tazama, mtumishi wangu nimtegemezaye, mteule wangu ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake, naye atawatolea mataifa hukumu.”
Huyu ni mtu ambaye Mungu amemchagua kwa kazi maalum.

Ataleta hukumu kwa mataifa yote, akimaanisha atakuwa na ujumbe wa kimataifa.

Isaya 42:11 – “Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao, na vijiji anavyokaa Kedari; na wakaao katika miamba na waimbe, wapige kelele kutoka vilele vya milima.”

Kedar alikuwa mtoto wa Ismaili na kizazi chake waliishi Arabia, ambapo Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alitokea.

3.  Isaya 21:13-17 - Ujumbe wa Arabia na Parani

Katika sura hii ya Isaya, kuna utabiri wa matukio yatakayotokea katika Arabia:

Isaya 21:13 – "Ufunuo juu ya Arabia. Mtapiga kambi nyikani, enyi watu wa Dedani."

Hii inaonyesha kuwa Arabia ni eneo la tukio kubwa la kiroho.

Isaya 21:14 – “Mleteeni mwenye kiu maji, enyi wenyeji wa Tema, mleteeni mkimbizi chakula chake.”

Tema ni sehemu ya Hijaz, ambako mji wa Madina upo.

Hii inahusiana na jinsi wakazi wa Madina walivyompokea Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na kumpa hifadhi.

4.  Yohana 14:16, 16:7-14 - Msaidizi (Parakletos)  na Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Yesu alisema:

Yohana 14:16 – “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi milele.” Yohana 16:7 – “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda, nitamtuma kwenu.”

Msaidizi huyu atafundisha ukweli wote (Yohana 16:13) → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alikuja na Qur’an kama mwongozo wa mwisho.

Neno Parakletos (Παράκλητος) linaweza kuwa Periklytos, ambalo linamaanisha "Aliyesifiwa"
(kwa Kiarabu, Ahmad – jina jingine la Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)).

Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Katika Qur’an, Mtume Isa(amani iwe juu yake) alitabiri kuja kwa mtume baada yake aitwaye Ahmad:

Surah As-Saff 61:6 "Na (wakumbuke) Isa bin Maryamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nikiwahakikishia yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na nikitoa habari njema ya (ujio wa) Mtume atakayekuja baada yangu, jina lake ni Ahmad."

Ahmad ni jina lingine la Muhammad.

Yesu anatabiri nabii anayekuja baada yake, ambaye atakuwa na ujumbe wa Mungu.

5.Ufunuo 12:5 & 19:15 - Fimbo ya Chuma

Ufunuo 19:15 – "Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili aweke mataifa chini, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma."

Hii inahusiana na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), ambaye atatawala kwa haki na nguvu za Mungu, na Qur’an inamtaja kama mtawala wa haki.

Hitimisho
Biblia ina maandiko ambayo, kwa muktadha wa tafsiri, yanaonyesha wazi dalili kuhusu ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Aya kutoka Kumbukumbu la Torati, Isaya, Yohana, na Ufunuo zinaweza kueleweka kama utabiri wa ujio wa Muhammad, hasa kwa vile anapatikana katika maeneo ya Arabia, anahusiana na Kedar, na anaitwa Ahmad, jina lingine la Muhammad.
Usijidanganye!! Mungu wake Yesu sio Mungu wa Mtume Mwamadi- Ni Mungu wawili tofauti! Pepo ya Wanaomfuata YESU ni Tofauti na Pepo ya Waislam. Agano la kale wa jipya akuna aliekuwa Mwislam na wala akuna aliongea chochote juu ya ujio wa mtume Binadamu baada ya Yesu: Yohana 14:16 – “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi milele.” Kinachokaa Milele maana yake akitokufa! Kaburi lake lipo Madina Sio Yeye...

Injili ni hekaya za kutungwa na kusadikika tu.

Quran ni hekaya za kutungwa na kusadikika tu.

Mtume Muhammad hajawahi kuwepo na hayupo.

Hakuna Mungu.
Hata wewe akili huna. Vinginevyo utoneshe picha ya akili zako.
 
Agano la kale wa jipya akuna aliekuwa Mwislam na wala akuna aliongea chochote juu ya ujio wa mtume Binadamu baada ya Yesu
Ipo mistari mingi ambayo inamuhusu Mtume Muhammad ﷺ lakini watu wengi mnadhani mistari hiyo inamuhusu yesu.

Kuhusu uwepo wa Uislam,dini hii ilikuwepo kabla hata ya kuumbwa kwa Adamuعَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ na ushahidi upo ila,ilipata jina la Al-Islaam baada ya ujio wa Mtume Muhammad ﷺ.
 
Agano la kale wa jipya akuna aliekuwa Mwislam na wala akuna aliongea chochote juu ya ujio wa mtume Binadamu baada ya Yesu
Ipo mistari mingi ambayo inamuhusu Mtume Muhammad ﷺ lakini watu wengi mnadhani mistari hiyo inamuhusu yesu.
Kuhusu kuwepo dini ya Uislamu ni kwamba hiyo dini ilikuwepo kabla hata ya kuumbwa kwa Adam عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ isipokuwa,ilipata jina la Al-Islaam baada ya ujio wa Mtume Muhammad ﷺ.
Mara Biblia kitabu cha kutunga, mara kimetabiri ujio wa mtume. Mara Mungu wao alitundukwa mara Issa nabii wetu.

Sometime kuwaelewa hawa jamaa inabidi ujitoe akili kwanza.
Hiyo Biblia imetengenezwa kutoka kwenye scriptures za Zabur,Taurat na Injil.Ikaongezewa maandiko mengine mapya na pia kuondoa baadhi ya maandiko ili kukidhi maslahi ya hao watungaji wa hiyo biblia.
Sasa kwa kuwa biblia imetokana na vitabu vya kweli,kuna baadhi ya maandishi hayajapotoshwa na baadhi yake ni hayo.
 
Kama unamzungumzia yesu ambaye alifia msalabani na ambaye yeye mwenyewe ni mungu basi ni kweli ulichokisema.
Lakini tukimzungumzia Yesu ambaye hakufa msalabani na wala yeye si mungu basi uliyosema si sahihi
Yesu wa Kwenye Quran Sio Yesu aliesulubiwa na Ponsyo Pilato Mrumi....Huyu Mnamjua nyie na Mtume Wenu alikuja 500+ baada ya Yesu Kufa na Kufufuka...Na akaja anataka tumwamini yeye ambaye ajawai mwona wala kukaa na kumsikiliza mmoja alieishi na kunsikiliza Yesu wa kweli
 
Ipo mistari mingi ambayo inamuhusu Mtume Muhammad ﷺ lakini watu wengi mnadhani mistari hiyo inamuhusu yesu.
Kuhusu kuwepo dini ya Uislamu ni kwamba hiyo dini ilikuwepo kabla hata ya kuumbwa kwa Adam عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ isipokuwa,ilipata jina la Al-Islaam baada ya ujio wa Mtume Muhammad ﷺ.

Hiyo Biblia imetengenezwa kutoka kwenye scriptures za Zabur,Taurat na Injil.Ikaongezewa maandiko mengine mapya na pia kuondoa baadhi ya maandiko ili kukidhi maslahi ya hao watungaji wa hiyo biblia.
Sasa kwa kuwa biblia imetokana na vitabu vya kweli,kuna baadhi ya maandishi hayajapotoshwa na baadhi yake ni hayo.
Mwamadi amekuja Duniani 500 years baada ya Yesu......akujua kusoma wala kuandika.....iweje aseme kuwa Bibilia ni batili? iweje aseme Yesu akusulubiwa?
Unasema
Ipo mistari mingi ambayo inamuhusu Mtume Muhammad ﷺ lakini watu wengi mnadhani mistari hiyo inamuhusu yesu.Kuhusu kuwepo dini ya Uislamu ni kwamba hiyo dini ilikuwepo kabla hata ya kuumbwa kwa Adam عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ isipokuwa,ilipata jina la Al-Islaam baada ya ujio wa Mtume Muhammad ﷺ.

1. Ibrahimu BAba wa Imani agano mojawapo ilikuwa kutahiri watoto wa kiume wafikapo siku saba- Nionyeshe haya katika Quran inayosema mambo ya kutahiri walio Waislam.
2. Kama Mwamadi amekuja kumalizia kile alichokiacha YESU iweje Quran ina sisitiza kwa Waislam kuwaua Waisrael na Wakristo?

Say (O Muhammad SAW) "O people of the Scripture (Jews and Christians)! You have nothing (as regards guidance) till you act according to the Taurât (Torah), the Injeel (Gospel), and what has (now) been sent down to you from your Lord (the Qur'ân)." Verily, that which has been sent down to you (Muhammad SAW) from your Lord increases in many of them their obstinate rebellion and disbelief. So be not sorrowful over the people who disbelieve
 
Attachments

  • 5_68.gif
    5_68.gif
    3.4 KB · Views: 3
Ipo mistari mingi ambayo inamuhusu Mtume Muhammad ﷺ lakini watu wengi mnadhani mistari hiyo inamuhusu yesu.
Kuhusu kuwepo dini ya Uislamu ni kwamba hiyo dini ilikuwepo kabla hata ya kuumbwa kwa Adam عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ isipokuwa,ilipata jina la Al-Islaam baada ya ujio wa Mtume Muhammad ﷺ.

Hiyo Biblia imetengenezwa kutoka kwenye scriptures za Zabur,Taurat na Injil.Ikaongezewa maandiko mengine mapya na pia kuondoa baadhi ya maandiko ili kukidhi maslahi ya hao watungaji wa hiyo biblia.
Sasa kwa kuwa biblia imetokana na vitabu vya kweli,kuna baadhi ya maandishi hayajapotoshwa na baadhi yake ni hayo.
kwa kukusaidia 1946 na 1956 wana historia waligundua Dead Sea Scrolls vyenye historia ya Dini na Mungu wa Israel (Mungu wake YESU) toka karne ya3 Kabla ya Yesu na mpka KArne ya Kwanza baada ya YESU -Bibilia na hivi vitabu vilivyogunduliwa vilikuwa na mambo sawa sawa 100%. Kumbuka kuwa Bibilia ni Kitabu cha Kikatoliki na Kimewekwa Makusanyo ya Vitabu mbalimbali toka kwa wale walioishi na kumwona Yesu. Mwamadi amjui na ajamwona Yesu Original
(The Dead Sea Scrolls, also called the Qumran Caves Scrolls, are a set of ancient Jewish manuscripts from the Second Temple period. They were discovered over a period of 10 years, between 1946 and 1956, at the Qumran Caves near Ein Feshkha in the West Bank, on the northern shore of the Dead Sea. Dating from the 3rd century BCE to the 1st century CE,[1] the Dead Sea Scrolls include the oldest surviving manuscripts of entire books later included in the biblical canons, including deuterocanonical manuscripts from late Second Temple Judaism and extrabiblical books.)
 
Yesu wa Kwenye Quran Sio Yesu aliesulubiwa na Ponsyo Pilato Mrumi....Huyu Mnamjua nyie na Mtume Wenu alikuja 500+ baada ya Yesu Kufa na Kufufuka...Na akaja anataka tumwamini yeye ambaye ajawai mwona wala kukaa na kumsikiliza mmoja alieishi na kunsikiliza Yesu wa kweli
Kiukweli tu nikwambie tu hadithi ya kwenye biblia ya mtu aliyezaliwa na bikra kisha baadae kusulubiwa kisha kufufuka si za kweli.
Ukweli ni kwamba huyo mtu aliyezaliwa na bikra hakusulubiwa bali alipazwa na Allah mpaka mbinguni ili kuokolewa dhidi ya wayahudi na wala hakuwa mungu.
 
"Kukaa nanyi milele"haimaanishi kuwa hatokufa bali,inamaanisha kuwa sheria zake zitadumu milele tofauti na Mitume(عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ)waliomtangulia.
Mtume Mwamadi sio yule alitabiriwa na YESU alie Hai........ Mtume kafa na Kazikwa:
Kiukweli tu nikwambie tu hadithi ya kwenye biblia ya mtu aliyezaliwa na bikra kisha baadae kusulubiwa kisha kufufuka si za kweli.
Ukweli ni kwamba huyo mtu aliyezaliwa na bikra hakusulubiwa bali alipazwa na Allah mpaka mbinguni ili kuokolewa dhidi ya wayahudi na wala hakuwa mungu.
hii Ameakuambia Nani? lete Uthibitisho acha longo longo.nipe ushaidi wa maandishi kussuport hizi pumba zako shekhee.nipo Nasubiria. Quran Imeshindwa thibitisha kifo cha Yesu na Pia imeshindwa kuficha hukuu wa Bikira Maria.Quran Inasema kabisa kuwa Yesu akufa na kweli amepaa Mbinguni....ila Nabii wa Mwisho kuja(muhamadi) amekufa na kuzikwa na watu 6 na mpaka leo ajafufuka....Anasubiria Ufufuko toka kwa YESU.
Quran sura 3, 4, 5, 19, 21, 23, and 66. Zina Mfagilia MAria MAma ake YESU..... Nipe haya inayomsifia 1.mama ake Mtume 2.Mke yeyote wa Mtume
Surah 19 yote ni juu ya mama ake Yesu
 
Mwamadi amekuja Duniani 500 years baada ya Yesu......akujua kusoma wala kuandika.....iweje aseme kuwa Bibilia ni batili? iweje aseme Yesu akusulubiwa?
Hayo hakuyasema yeye bali yalisemwa na Allah ambaye ndiye alivishusha vitabu vya halali ambavyo viliharibiwa ili kutengeneza biblia na kusingizia ni maneno ya Mungu ilhali ni kitabu kilichotungwa na wanadamu kwa kukopa baadhi ya maandiko kutoka kwenye vitabu vya Allah na kisha kuongezea na maneno yao binafsi kwa maslahi yao.
Kuhusu kusulubiwa kwa yesu hayo ni maneno ya majigambo ya wayahudi kuwa wao walimsulubu Mtume huyo wa Allah عَلَیهِ‌السَّلام lakini hawakumsulubisha yeye bali walizugwa

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا ﴿١٥٧﴾

157. Na kusema kwao (kwa kujifaharisha): Hakika sisi tumemuua Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam, Rasuli wa Allaah. Na hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa tu. Na hakika wale waliokhitilafiana katika hayo, kwa hakika wamo katika shaka nayo. Hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumuua.(Qur'an 4:157)
 
Mungu akusaidie Uijue kweli ya Yesu Kristo.

Nimekusikitikia sana.
Upo kwenye vifungo vikali sana.

MUNGU AKUFUNULIE KWELI YAKE
Wewe ndo upo kwenye vifungo vikali mara nyingi huwa mnadanganya Musa alikuwa mwarabu lakini mnasema waarabu wametokana na Ishmael wakati huohuo Musa hajatokea kwenye uzao wa Ismael
 
Hayo hakuyasema yeye bali yalisemwa na Allah ambaye ndiye alivishusha vitabu vya halali ambavyo viliharibiwa ili kutengeneza biblia na kusingizia ni maneno ya Mungu ilhali ni kitabu kilichotungwa na wanadamu kwa kukopa baadhi ya maandiko kutoka kwenye vitabu vya Allah na kisha kuongezea na maneno yao binafsi kwa maslahi yao.
Kuhusu kusulubiwa kwa yesu hayo ni maneno ya majigambo ya wayahudi kuwa wao walimsulubu Mtume huyo wa Allah عَلَیهِ‌السَّلام lakini hawakumsulubisha yeye bali walizugwa

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا ﴿١٥٧﴾

157. Na kusema kwao (kwa kujifaharisha): Hakika sisi tumemuua Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam, Rasuli wa Allaah. Na hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa tu. Na hakika wale waliokhitilafiana katika hayo, kwa hakika wamo katika shaka nayo. Hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumuua.(Qur'an 4:157)
huyu sio Yule YEsu aliesulubiwa na Warumi. huyu anaezungumziwa kwenye hii haya 157: Ni yesu mwingine mana Original YEsu alisulubiwa,akazikwa na akafufuka na akapaa Mbinguni na atarudi tena
 
Back
Top Bottom