Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Hakuna bible original ila vitabu ila kuna vitabu vitabu vya Allah ambavyo ni original kabla ya Qur'an navyo ni Zabur,Taurat na Injil
Hata hivyo, kutokana na uingiliaji wa wanadamu, vitabu hivi vilipoteza usahihi wa asili yake. Kwa sasa, nakala zinazopatikana za Taurat na Injili ni zile zilizorekebishwa na kuhaririwa na wanadamu, na hivyo haviwezi kuaminika kama vitabu vya asili vilivyoteremshwa na Allah. Kwa upande mwingine, Zabur, ambayo ni kitabu alichoteremshiwa Nabii Daudi عَلَیهِ‌السَّلام, haipo tena katika umbo lake la asili, na hivyo hatuwezi kuipata katika hali yake ya awali.
Hivo vitabu sio vya Allah hivo ni vitabu vya wayahudi havina uhusiano wowote na Allah
 
Huo ubao upo wapi Kwasasa
Al-Lawh Al-Mahfuwdhw ni Ubao Uliohifadhiwa mbinguni. Umehifadhika kutokana na mabadiliko, kuongozeka na kupunguka na umehifadhiwa na mashaytwaan. Nao ni Ubao ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Amethibitisha kila kitu ndani yake.
 
Hivo vitabu sio vya Allah hivo ni vitabu vya wayahudi havina uhusiano wowote na Allah
Hivyo ni vitabu vya Allah alivyoviteremsha kwa wayahudi kama yeye mwenyewe anavyokiri kwenye Qur’an
نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾
3. Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na Akateremsha Tawraat na Injiyl.(Qur’an 3:3)

وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na Tukamfuatishia katika njia yao (Manabii hao), ‘Iysaa mwana wa Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa Injiyl yenye mwongozo na nuru ndani yake, inasadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na Tumeifanya mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.(Qur'an 5:46)

حَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾
163. Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw,[55] (kizazi chake) na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr.(Qur’an 4:163)
 
Mbona hakuna mahusiono Wala kumbukumbu yoyote inayowahusisha wayahudi na Allah ndo maana tukisema uislam ni dini ya kubumba bumba tu ambayo ilijaribu kujinasibisha na uyahudi ili ionekane Ipo relevant
 
Ikiwa Waisraeli wanahusiana na Isaka, basi ndugu zao wa karibu ni kizazi cha Ismaili, ambacho kilizaa Waarabu.

Mkuu Kwa kuzingatia maandiko na ulichonukuu ni wazi kuwa ndugu wa karibu wa Israel ni esau
 
Mbona hakuna mahusiono Wala kumbukumbu yoyote inayowahusisha wayahudi na Allah ndo maana tukisema uislam ni dini ya kubumba bumba tu ambayo ilijaribu kujinasibisha na uyahudi ili ionekane Ipo relevant
Allah aliteremsha Zabur, Taurat na Injil kwa Mitume wake ili wawafikishie ujumbe wana wa Israel(wayahudi).
 
Allah aliteremsha Zabur, Taurat na Injil kwa Mitume wake ili wawafikishie ujumbe wana wa Israel(wayahudi).
Sawa ikawaje ghafla vikakopiwa kwenye Quran Kisha uongo ukatengenezwa kuwa vimeshushwa.

Na kwanini mnaeneza uzushi kuwa mitume walikuwa waarabu.

Na kwanini mnamnasibisha Allah na Imani ya kiyahudi wakati hawana mahusiano?
 
Katika historia, kumekuwa na mijadala kuhusu kama maandiko ya zamani yalitabiri ujio wa nabii wa mwisho. Watu wengi wamechunguza vitabu vya kale wakitafuta dalili zinazoelezea mtu atakayekuja na mwongozo wa kiroho kwa mataifa yote. Katika makala hii, tutaangalia aya mbalimbali kutoka Injili zinazoonyesha utabiri wa ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

1.Kumbukumbu la  Torati 18:18 -  Nabii  kama Musa

"Nitawainulia nabii kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18)

Katika aya hii, Mungu anamwambia Musa kwamba nabii mwingine kama yeye atainuliwa kwa watu. Wanazuoni wanaeleza kuwa nabii huyu:
Atakuwa kutoka kwa ndugu wa Waisraeli → Ikiwa Waisraeli wanahusiana na Isaka, basi ndugu zao wa karibu ni kizazi cha Ismaili, ambacho kilizaa Waarabu.

Atakuwa kama Musa → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na Musa wote walikuwa manabii waliopokea sheria mpya na waliongoza jamii zao kwa mwongozo wa Mungu.

Atakuwa na maneno ya Mungu kinywani mwake → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alipokea Qur’an kwa ufunuo wa Jibril, kama Musa alivyopewa Taurati.

2.Isaya 42:1-13 -  Nabii  kutoka Kedar

Katika sura hii ya Isaya, kuna maelezo kuhusu mtumishi wa Mungu ambaye atakuwa nuru kwa mataifa yote:

Isaya 42:1 – “Tazama, mtumishi wangu nimtegemezaye, mteule wangu ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake, naye atawatolea mataifa hukumu.”
Huyu ni mtu ambaye Mungu amemchagua kwa kazi maalum.

Ataleta hukumu kwa mataifa yote, akimaanisha atakuwa na ujumbe wa kimataifa.

Isaya 42:11 – “Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao, na vijiji anavyokaa Kedari; na wakaao katika miamba na waimbe, wapige kelele kutoka vilele vya milima.”

Kedar alikuwa mtoto wa Ismaili na kizazi chake waliishi Arabia, ambapo Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alitokea.

3.  Isaya 21:13-17 - Ujumbe wa Arabia na Parani

Katika sura hii ya Isaya, kuna utabiri wa matukio yatakayotokea katika Arabia:

Isaya 21:13 – "Ufunuo juu ya Arabia. Mtapiga kambi nyikani, enyi watu wa Dedani."

Hii inaonyesha kuwa Arabia ni eneo la tukio kubwa la kiroho.

Isaya 21:14 – “Mleteeni mwenye kiu maji, enyi wenyeji wa Tema, mleteeni mkimbizi chakula chake.”

Tema ni sehemu ya Hijaz, ambako mji wa Madina upo.

Hii inahusiana na jinsi wakazi wa Madina walivyompokea Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na kumpa hifadhi.

4.  Yohana 14:16, 16:7-14 - Msaidizi (Parakletos)  na Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Yesu alisema:

Yohana 14:16 – “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi milele.” Yohana 16:7 – “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda, nitamtuma kwenu.”

Msaidizi huyu atafundisha ukweli wote (Yohana 16:13) → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alikuja na Qur’an kama mwongozo wa mwisho.

Neno Parakletos (Παράκλητος) linaweza kuwa Periklytos, ambalo linamaanisha "Aliyesifiwa"
(kwa Kiarabu, Ahmad – jina jingine la Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)).

Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Katika Qur’an, Mtume Isa(amani iwe juu yake) alitabiri kuja kwa mtume baada yake aitwaye Ahmad:

Surah As-Saff 61:6 "Na (wakumbuke) Isa bin Maryamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nikiwahakikishia yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na nikitoa habari njema ya (ujio wa) Mtume atakayekuja baada yangu, jina lake ni Ahmad."

Ahmad ni jina lingine la Muhammad.

Yesu anatabiri nabii anayekuja baada yake, ambaye atakuwa na ujumbe wa Mungu.

5.Ufunuo 12:5 & 19:15 - Fimbo ya Chuma

Ufunuo 19:15 – "Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili aweke mataifa chini, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma."

Hii inahusiana na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), ambaye atatawala kwa haki na nguvu za Mungu, na Qur’an inamtaja kama mtawala wa haki.

Hitimisho
Biblia ina maandiko ambayo, kwa muktadha wa tafsiri, yanaonyesha wazi dalili kuhusu ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Aya kutoka Kumbukumbu la Torati, Isaya, Yohana, na Ufunuo zinaweza kueleweka kama utabiri wa ujio wa Muhammad, hasa kwa vile anapatikana katika maeneo ya Arabia, anahusiana na Kedar, na anaitwa Ahmad, jina lingine la Muhammad.
Muongo mkubwa wewe unaandika vipande vipande yohana 14:16 umeifupisha endelea Hadi mstari wa 17 utajua Kama aliongelewa roho mtakatifu.

Kuna gape kubwa Sana Kati ya uislam na ukristo. Mohamed Yule Ni muhuni mmoja tu aliyokuwa anachukua kwenye biblia anachanganya na yake.
 
Sawa ikawaje ghafla vikakopiwa kwenye Quran Kisha uongo ukatengenezwa kuwa vimeshushwa.
Hivyo vitabu havijakopiwa kwenye Qur’an bali biblia ndio ilitungwa kwa kuvikopi vitabu hivyo vya Allah wakati Qur’an iliteremshwa kwa Mtume Muhammadﷺ .
 
Na kwanini mnaeneza uzushi kuwa mitume walikuwa waarabu.
Nani kasema haya? Sio Mitume wote walikuwa waarabu kwa mfano Musaعَلَیهِ‌السَّلام na Isaعَلَیهِ‌السَّلام walikuwa ni wana wa Israel(waisrael)
Labda wewe useme wapi uliuona uzushi huo
 
Muongo mkubwa wewe unaandika vipande vipande yohana 14:16 umeifupisha endelea Hadi mstari wa 17 utajua Kama aliongelewa roho mtakatifu.
Huyo roho mtakatifu ndiye ambaye mnasema ni mmoja katika waungu watatu?
 
huyu sio Yule YEsu aliesulubiwa na Warumi. huyu anaezungumziwa kwenye hii haya 157: Ni yesu mwingine mana Original YEsu alisulubiwa,akazikwa na akafufuka na akapaa Mbinguni na atarudi tena
Una maanisha mungu alisurubiwa na alio waumba

Na biblia ina sema nini kuhusu mtu kusurubiwa msalanani?
 
Muongo mkubwa wewe unaandika vipande vipande yohana 14:16 umeifupisha endelea Hadi mstari wa 17 utajua Kama aliongelewa roho mtakatifu.

Kuna gape kubwa Sana Kati ya uislam na ukristo. Mohamed Yule Ni muhuni mmoja tu aliyokuwa anachukua kwenye biblia anachanganya na yake.
Hawa jamaa wa upande ule wanahangaika sana na ukristo halafu cha ajabu wakristo hawajihangaishi nao
 
Back
Top Bottom