Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Hayo hakuyasema yeye bali yalisemwa na Allah ambaye ndiye alivishusha vitabu vya halali ambavyo viliharibiwa ili kutengeneza biblia na kusingizia ni maneno ya Mungu ilhali ni kitabu kilichotungwa na wanadamu kwa kukopa baadhi ya maandiko kutoka kwenye vitabu vya Allah na kisha kuongezea na maneno yao binafsi kwa maslahi yao.
Kuhusu kusulubiwa kwa yesu hayo ni maneno ya majigambo ya wayahudi kuwa wao walimsulubu Mtume huyo wa Allah عَلَیهِ‌السَّلام lakini hawakumsulubisha yeye bali walizugwa

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا ﴿١٥٧﴾

157. Na kusema kwao (kwa kujifaharisha): Hakika sisi tumemuua Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam, Rasuli wa Allaah. Na hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa tu. Na hakika wale waliokhitilafiana katika hayo, kwa hakika wamo katika shaka nayo. Hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumuua.(Qur'an 4:157)
Hiyo Quran imeandikwa na watu au imeshushwa hebu tueleze huyo Allah aliedondoshea wapi hiyo Quran?
 
Wakati vinateremshwa Bible ilikuwa Bado kuandikwa? Embu tutafutieni zile bilble original
 
Ibrahimu BAba wa Imani agano mojawapo ilikuwa kutahiri watoto wa kiume wafikapo siku saba- Nionyeshe haya katika Quran inayosema mambo ya kutahiri walio Waislam.
Katika Qur’an tumeambiwa tufuate mila ya Ibrahim عَلَیهِ‌السَّلام.
"...(fuateni) mila ya baba yenu Ibrahim..." (Qur'an 22:78)
Na katika mila hizo ni kutahiriwa kama ambavyo tumeamrishwa sisi.
Mtume ﷺ alisema:
"Fitrat tano ni hizi: Kutahiriwa, kunyoa nywele za sehemu za siri, kupunguza masharubu, kukata kucha, na kunyoa nywele za kwapani." (Sahih al-Bukhari na Muslim)
 
Kama Mwamadi amekuja kumalizia kile alichokiacha YESU iweje Quran ina sisitiza kwa Waislam kuwaua Waisrael na Wakristo?

Say (O Muhammad SAW) "O people of the Scripture (Jews and Christians)! You have nothing (as regards guidance) till you act according to the Taurât (Torah), the Injeel (Gospel), and what has (now) been sent down to you from your Lord (the Qur'ân)." Verily, that which has been sent down to you (Muhammad SAW) from your Lord increases in many of them their obstinate rebellion and disbelief. So be not sorrowful over the people who disbelieve
Wapi katika aya hiyo wamesema tuwauwe wakristo na Waisraeli zaidi ya kuwasisitiza mayahudi na wakristo kufuata maagizo ya vitabu vya awali vya Allah na Qur’an?
 
kwa kukusaidia 1946 na 1956 wana historia waligundua Dead Sea Scrolls vyenye historia ya Dini na Mungu wa Israel (Mungu wake YESU) toka karne ya3 Kabla ya Yesu na mpka KArne ya Kwanza baada ya YESU -Bibilia na hivi vitabu vilivyogunduliwa vilikuwa na mambo sawa sawa 100%. Kumbuka kuwa Bibilia ni Kitabu cha Kikatoliki na Kimewekwa Makusanyo ya Vitabu mbalimbali toka kwa wale walioishi na kumwona Yesu. Mwamadi amjui na ajamwona Yesu Original
(The Dead Sea Scrolls, also called the Qumran Caves Scrolls, are a set of ancient Jewish manuscripts from the Second Temple period. They were discovered over a period of 10 years, between 1946 and 1956, at the Qumran Caves near Ein Feshkha in the West Bank, on the northern shore of the Dead Sea. Dating from the 3rd century BCE to the 1st century CE,[1] the Dead Sea Scrolls include the oldest surviving manuscripts of entire books later included in the biblical canons, including deuterocanonical manuscripts from late Second Temple Judaism and extrabiblical books.)
Hivyo vitabu vilivyogunduliwa vilikuwa ni maneno ya nani?
 
Katika Qur’an tumeambiwa tufuate mila ya Ibrahim عَلَیهِ‌السَّلام.
"...(fuateni) mila ya baba yenu Ibrahim..." (Qur'an 22:78)
Na katika mila hizo ni kutahiriwa kama ambavyo tumeamrishwa sisi.
Mtume ﷺ alisema:
"Fitrat tano ni hizi: Kutahiriwa, kunyoa nywele za sehemu za siri, kupunguza masharubu, kukata kucha, na kunyoa nywele za kwapani." (Sahih al-Bukhari na Muslim)
Luka : 2:21
"Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba."
Naomba haya ya Quran inayoelezea tukio kama hili kwa Mwislam yeyote yule .
 
Wapi katika aya hiyo wamesema tuwauwe wakristo na Waisraeli zaidi ya kuwasisitiza mayahudi na wakristo kufuata maagizo ya vitabu vya awali vya Allah na Qur’an?
👇
Surah 3:151: "We shall cast terror into the hearts of those who disbelieve (all non-Muslims)
 
Quran Imeshindwa thibitisha kifo cha Yesu na Pia imeshindwa kuficha hukuu wa Bikira Maria.
Kwa mujibu wa Qur’an Isaعَلَیهِ‌السَّلام ambaye nyinyi mnamwita yesu hajafa ila yupo mbinguni.
Kuhusu ukuu wa Mariamu Qur’an haijauficha kwa kuwa Mariamu alikuwa na sifa zote zilizotajwa kwenye Qur’an lakini Qur’an imepinga kuwa yeye ni mama wa mungu.
 
Quran Inasema kabisa kuwa Yesu akufa na kweli amepaa Mbinguni....ila Nabii wa Mwisho kuja(muhamadi) amekufa na kuzikwa na watu 6 na mpaka leo ajafufuka....Anasubiria Ufufuko toka kwa YESU.
Ni kweli Mtume Muhammad ﷺ amefariki na hajafufuka na hatofufuka mpaka siku ya kiama na atakayemfufua ni Allah na si yesu ambaye ni binadamu kama yeye.
 
Quran sura 3, 4, 5, 19, 21, 23, and 66. Zina Mfagilia MAria MAma ake YESU..... Nipe haya inayomsifia 1.mama ake Mtume 2.Mke yeyote wa Mtume
Surah 19 yote ni juu ya mama ake Yesu
Ni kweli, na alistahili hizo sifa lakini kubwa ni kwamba hakuzaa mungu yaani yeye si Mama wa mungu bali alikuwa ni mwanamke mchamungu na aliyemzaa mtoto Nabii jambo ambalo hata hiyo sura uliyoitumia kama ushahidi wako inafafanua.
 
Hiyo Quran imeandikwa na watu au imeshushwa hebu tueleze huyo Allah aliedondoshea wapi hiyo Quran?
Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu (Kalamullah) yaliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad ﷺ kupitia Malaika Jibril.

Qur'an ilishuka kutoka Lauhul Mahfudh (Ubao uliohifadhiwa) na iliteremshwa hadi Baytul 'Izzah (Nyumba ya Heshima) katika mbingu ya kwanza. Hii ilikuwa hatua ya kwanza ya kuteremka kwa Qur'an. Baada ya hapo, Qur'an ilianza kushuka kwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka 23 kwa Mtume Muhammad ﷺ, ikitekeleza matukio na mahitaji ya jamii. Sehemu kubwa ya Qur'an ilishushwa Makkah (aya za Makkiyya), ambazo zilijikita katika imani, uongofu, na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Baada ya hijra, aya nyingi za Madina (aya za Madaniyya) zilitokea, zikihusiana na sheria, haki, na utawala wa kijamii. Hivyo, Qur'an ilishuka kwa hatua kutoka Baytul 'Izzah na kumfikia Mtume ﷺ, ikifundisha maadili na sheria za Kiislamu.
 
Wakati vinateremshwa Bible ilikuwa Bado kiandikwa? Embu tutafutieni zile bilble original
Hakuna bible original ila vitabu ila kuna vitabu vitabu vya Allah ambavyo ni original kabla ya Qur'an navyo ni Zabur,Taurat na Injil
Hata hivyo, kutokana na uingiliaji wa wanadamu, vitabu hivi vilipoteza usahihi wa asili yake. Kwa sasa, nakala zinazopatikana za Taurat na Injili ni zile zilizorekebishwa na kuhaririwa na wanadamu, na hivyo haviwezi kuaminika kama vitabu vya asili vilivyoteremshwa na Allah. Kwa upande mwingine, Zabur, ambayo ni kitabu alichoteremshiwa Nabii Daudi عَلَیهِ‌السَّلام, haipo tena katika umbo lake la asili, na hivyo hatuwezi kuipata katika hali yake ya awali.
 
Hiyo Biblia imetengenezwa kutoka kwenye scriptures za Zabur,Taurat na Injil.Ikaongezewa maandiko mengine mapya na pia kuondoa baadhi ya maandiko ili kukidhi maslahi ya hao watungaji wa hiyo biblia.
Sasa kwa kuwa biblia imetokana na vitabu vya kweli,kuna baadhi ya maandishi hayajapotoshwa na baadhi yake ni hayo.

Kwa mantiki hiyo,habari za Mariam wa kwenye Biblia na Yesu baadhi yake ni kweli na baadhi yake si sahihi zimepotoshwa kwa ajili ya maslahi binafsi ya wahusika
Kulingana na hustoria kati ya Biblia na Qurani kipi kilianza?
Unaijua Talmud? Unaijua Septuagint? Umesoma canonicity?
Kama huna elimu ya hayo mambo ni bora ujikalie kimya.
 
Katika historia, kumekuwa na mijadala kuhusu kama maandiko ya zamani yalitabiri ujio wa nabii wa mwisho. Watu wengi wamechunguza vitabu vya kale wakitafuta dalili zinazoelezea mtu atakayekuja na mwongozo wa kiroho kwa mataifa yote. Katika makala hii, tutaangalia aya mbalimbali kutoka Injili zinazoonyesha utabiri wa ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

1.Kumbukumbu la  Torati 18:18 -  Nabii  kama Musa

"Nitawainulia nabii kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18)

Katika aya hii, Mungu anamwambia Musa kwamba nabii mwingine kama yeye atainuliwa kwa watu. Wanazuoni wanaeleza kuwa nabii huyu:
Atakuwa kutoka kwa ndugu wa Waisraeli → Ikiwa Waisraeli wanahusiana na Isaka, basi ndugu zao wa karibu ni kizazi cha Ismaili, ambacho kilizaa Waarabu.

Atakuwa kama Musa → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na Musa wote walikuwa manabii waliopokea sheria mpya na waliongoza jamii zao kwa mwongozo wa Mungu.

Atakuwa na maneno ya Mungu kinywani mwake → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alipokea Qur’an kwa ufunuo wa Jibril, kama Musa alivyopewa Taurati.

2.Isaya 42:1-13 -  Nabii  kutoka Kedar

Katika sura hii ya Isaya, kuna maelezo kuhusu mtumishi wa Mungu ambaye atakuwa nuru kwa mataifa yote:

Isaya 42:1 – “Tazama, mtumishi wangu nimtegemezaye, mteule wangu ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake, naye atawatolea mataifa hukumu.”
Huyu ni mtu ambaye Mungu amemchagua kwa kazi maalum.

Ataleta hukumu kwa mataifa yote, akimaanisha atakuwa na ujumbe wa kimataifa.

Isaya 42:11 – “Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao, na vijiji anavyokaa Kedari; na wakaao katika miamba na waimbe, wapige kelele kutoka vilele vya milima.”

Kedar alikuwa mtoto wa Ismaili na kizazi chake waliishi Arabia, ambapo Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alitokea.

3.  Isaya 21:13-17 - Ujumbe wa Arabia na Parani

Katika sura hii ya Isaya, kuna utabiri wa matukio yatakayotokea katika Arabia:

Isaya 21:13 – "Ufunuo juu ya Arabia. Mtapiga kambi nyikani, enyi watu wa Dedani."

Hii inaonyesha kuwa Arabia ni eneo la tukio kubwa la kiroho.

Isaya 21:14 – “Mleteeni mwenye kiu maji, enyi wenyeji wa Tema, mleteeni mkimbizi chakula chake.”

Tema ni sehemu ya Hijaz, ambako mji wa Madina upo.

Hii inahusiana na jinsi wakazi wa Madina walivyompokea Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na kumpa hifadhi.

4.  Yohana 14:16, 16:7-14 - Msaidizi (Parakletos)  na Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Yesu alisema:

Yohana 14:16 – “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi milele.” Yohana 16:7 – “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda, nitamtuma kwenu.”

Msaidizi huyu atafundisha ukweli wote (Yohana 16:13) → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alikuja na Qur’an kama mwongozo wa mwisho.

Neno Parakletos (Παράκλητος) linaweza kuwa Periklytos, ambalo linamaanisha "Aliyesifiwa"
(kwa Kiarabu, Ahmad – jina jingine la Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)).

Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Katika Qur’an, Mtume Isa(amani iwe juu yake) alitabiri kuja kwa mtume baada yake aitwaye Ahmad:

Surah As-Saff 61:6 "Na (wakumbuke) Isa bin Maryamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nikiwahakikishia yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na nikitoa habari njema ya (ujio wa) Mtume atakayekuja baada yangu, jina lake ni Ahmad."

Ahmad ni jina lingine la Muhammad.

Yesu anatabiri nabii anayekuja baada yake, ambaye atakuwa na ujumbe wa Mungu.

5.Ufunuo 12:5 & 19:15 - Fimbo ya Chuma

Ufunuo 19:15 – "Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili aweke mataifa chini, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma."

Hii inahusiana na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), ambaye atatawala kwa haki na nguvu za Mungu, na Qur’an inamtaja kama mtawala wa haki.

Hitimisho
Biblia ina maandiko ambayo, kwa muktadha wa tafsiri, yanaonyesha wazi dalili kuhusu ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Aya kutoka Kumbukumbu la Torati, Isaya, Yohana, na Ufunuo zinaweza kueleweka kama utabiri wa ujio wa Muhammad, hasa kwa vile anapatikana katika maeneo ya Arabia, anahusiana na Kedar, na anaitwa Ahmad, jina lingine la Muhammad.
Tafuta pesa wee jamaa acha kufuatilia historia za maisha ya watu wa Middle East
 
Luka : 2:21
"Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba."
Naomba haya ya Quran inayoelezea tukio kama hili kwa Mwislam yeyote yule .
Kwa Qur’an kusema kuwa tufuate mila za Ibrahim عَلَیهِ‌السَّلام hiyo imeelezea moja kwa moja kuwa ni lazima tutahiriwe na pia hadithi ya Mtume ﷺ
"Mtume ﷺ alisema: 'Tunahitaji kumtahiri mtoto mchanga siku ya tatu au ya saba baada ya kuzaliwa.'"
(Sunan Abu Dawood, Kitab al-Tahara)
Hivyo, kwa mantiki hiyo ni sheria kwa waislamu kutahiriwa
 
Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu (Kalamullah) yaliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad ﷺ kupitia Malaika Jibril.

Qur'an ilishuka kutoka Lauhul Mahfudh (Ubao uliohifadhiwa) na iliteremshwa hadi Baytul 'Izzah (Nyumba ya Heshima) katika mbingu ya kwanza. Hii ilikuwa hatua ya kwanza ya kuteremka kwa Qur'an. Baada ya hapo, Qur'an ilianza kushuka kwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka 23 kwa Mtume Muhammad ﷺ, ikitekeleza matukio na mahitaji ya jamii. Sehemu kubwa ya Qur'an ilishushwa Makkah (aya za Makkiyya), ambazo zilijikita katika imani, uongofu, na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Baada ya hijra, aya nyingi za Madina (aya za Madaniyya) zilitokea, zikihusiana na sheria, haki, na utawala wa kijamii. Hivyo, Qur'an ilishuka kwa hatua kutoka Baytul 'Izzah na kumfikia Mtume ﷺ, ikifundisha maadili na sheria za Kiislamu.
Huo ubao upo wapi Kwasasa
 
Kulingana na hustoria kati ya Biblia na Qurani kipi kilianza?
Unaijua Talmud? Unaijua Septuagint? Umesoma canonicity?
Kama huna elimu ya hayo mambo ni bora ujikalie kimya.
Hivyo vyote ni vitabu vya wanaadamu
 
Back
Top Bottom