Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Hiyo Quran imeandikwa na watu au imeshushwa hebu tueleze huyo Allah aliedondoshea wapi hiyo Quran?
 
Wakati vinateremshwa Bible ilikuwa Bado kuandikwa? Embu tutafutieni zile bilble original
 
Ibrahimu BAba wa Imani agano mojawapo ilikuwa kutahiri watoto wa kiume wafikapo siku saba- Nionyeshe haya katika Quran inayosema mambo ya kutahiri walio Waislam.
Katika Qur’an tumeambiwa tufuate mila ya Ibrahim عَلَیهِ‌السَّلام.
"...(fuateni) mila ya baba yenu Ibrahim..." (Qur'an 22:78)
Na katika mila hizo ni kutahiriwa kama ambavyo tumeamrishwa sisi.
Mtume ﷺ alisema:
"Fitrat tano ni hizi: Kutahiriwa, kunyoa nywele za sehemu za siri, kupunguza masharubu, kukata kucha, na kunyoa nywele za kwapani." (Sahih al-Bukhari na Muslim)
 
Wapi katika aya hiyo wamesema tuwauwe wakristo na Waisraeli zaidi ya kuwasisitiza mayahudi na wakristo kufuata maagizo ya vitabu vya awali vya Allah na Qur’an?
 
Hivyo vitabu vilivyogunduliwa vilikuwa ni maneno ya nani?
 
Luka : 2:21
"Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba."
Naomba haya ya Quran inayoelezea tukio kama hili kwa Mwislam yeyote yule .
 
Wapi katika aya hiyo wamesema tuwauwe wakristo na Waisraeli zaidi ya kuwasisitiza mayahudi na wakristo kufuata maagizo ya vitabu vya awali vya Allah na Qur’an?
👇
Surah 3:151: "We shall cast terror into the hearts of those who disbelieve (all non-Muslims)
 
Quran Imeshindwa thibitisha kifo cha Yesu na Pia imeshindwa kuficha hukuu wa Bikira Maria.
Kwa mujibu wa Qur’an Isaعَلَیهِ‌السَّلام ambaye nyinyi mnamwita yesu hajafa ila yupo mbinguni.
Kuhusu ukuu wa Mariamu Qur’an haijauficha kwa kuwa Mariamu alikuwa na sifa zote zilizotajwa kwenye Qur’an lakini Qur’an imepinga kuwa yeye ni mama wa mungu.
 
Quran Inasema kabisa kuwa Yesu akufa na kweli amepaa Mbinguni....ila Nabii wa Mwisho kuja(muhamadi) amekufa na kuzikwa na watu 6 na mpaka leo ajafufuka....Anasubiria Ufufuko toka kwa YESU.
Ni kweli Mtume Muhammad ﷺ amefariki na hajafufuka na hatofufuka mpaka siku ya kiama na atakayemfufua ni Allah na si yesu ambaye ni binadamu kama yeye.
 
Quran sura 3, 4, 5, 19, 21, 23, and 66. Zina Mfagilia MAria MAma ake YESU..... Nipe haya inayomsifia 1.mama ake Mtume 2.Mke yeyote wa Mtume
Surah 19 yote ni juu ya mama ake Yesu
Ni kweli, na alistahili hizo sifa lakini kubwa ni kwamba hakuzaa mungu yaani yeye si Mama wa mungu bali alikuwa ni mwanamke mchamungu na aliyemzaa mtoto Nabii jambo ambalo hata hiyo sura uliyoitumia kama ushahidi wako inafafanua.
 
Hiyo Quran imeandikwa na watu au imeshushwa hebu tueleze huyo Allah aliedondoshea wapi hiyo Quran?
Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu (Kalamullah) yaliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad ﷺ kupitia Malaika Jibril.

Qur'an ilishuka kutoka Lauhul Mahfudh (Ubao uliohifadhiwa) na iliteremshwa hadi Baytul 'Izzah (Nyumba ya Heshima) katika mbingu ya kwanza. Hii ilikuwa hatua ya kwanza ya kuteremka kwa Qur'an. Baada ya hapo, Qur'an ilianza kushuka kwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka 23 kwa Mtume Muhammad ﷺ, ikitekeleza matukio na mahitaji ya jamii. Sehemu kubwa ya Qur'an ilishushwa Makkah (aya za Makkiyya), ambazo zilijikita katika imani, uongofu, na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Baada ya hijra, aya nyingi za Madina (aya za Madaniyya) zilitokea, zikihusiana na sheria, haki, na utawala wa kijamii. Hivyo, Qur'an ilishuka kwa hatua kutoka Baytul 'Izzah na kumfikia Mtume ﷺ, ikifundisha maadili na sheria za Kiislamu.
 
Wakati vinateremshwa Bible ilikuwa Bado kiandikwa? Embu tutafutieni zile bilble original
Hakuna bible original ila vitabu ila kuna vitabu vitabu vya Allah ambavyo ni original kabla ya Qur'an navyo ni Zabur,Taurat na Injil
Hata hivyo, kutokana na uingiliaji wa wanadamu, vitabu hivi vilipoteza usahihi wa asili yake. Kwa sasa, nakala zinazopatikana za Taurat na Injili ni zile zilizorekebishwa na kuhaririwa na wanadamu, na hivyo haviwezi kuaminika kama vitabu vya asili vilivyoteremshwa na Allah. Kwa upande mwingine, Zabur, ambayo ni kitabu alichoteremshiwa Nabii Daudi عَلَیهِ‌السَّلام, haipo tena katika umbo lake la asili, na hivyo hatuwezi kuipata katika hali yake ya awali.
 
Kulingana na hustoria kati ya Biblia na Qurani kipi kilianza?
Unaijua Talmud? Unaijua Septuagint? Umesoma canonicity?
Kama huna elimu ya hayo mambo ni bora ujikalie kimya.
 
Tafuta pesa wee jamaa acha kufuatilia historia za maisha ya watu wa Middle East
 
Luka : 2:21
"Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba."
Naomba haya ya Quran inayoelezea tukio kama hili kwa Mwislam yeyote yule .
Kwa Qur’an kusema kuwa tufuate mila za Ibrahim عَلَیهِ‌السَّلام hiyo imeelezea moja kwa moja kuwa ni lazima tutahiriwe na pia hadithi ya Mtume ﷺ
"Mtume ﷺ alisema: 'Tunahitaji kumtahiri mtoto mchanga siku ya tatu au ya saba baada ya kuzaliwa.'"
(Sunan Abu Dawood, Kitab al-Tahara)
Hivyo, kwa mantiki hiyo ni sheria kwa waislamu kutahiriwa
 
Huo ubao upo wapi Kwasasa
 
Kulingana na hustoria kati ya Biblia na Qurani kipi kilianza?
Unaijua Talmud? Unaijua Septuagint? Umesoma canonicity?
Kama huna elimu ya hayo mambo ni bora ujikalie kimya.
Hivyo vyote ni vitabu vya wanaadamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…