Dogma ya utatu inasema Yesu ndiye huyo huyo Mungu baba ,tofauti na maandiko ambayo yanasema YHWH ni Mungu baba na Yesu ni Mungu ,maana wa Mungu
Hata Zaburi inasema hivi
1. Zaburi 45:7 (SUV)
"Umependa haki, umechukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta Kwa mafuta ya furaha kupita wenzio."
2. Waebrania 1:8-9 (SUV)
8 "Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili."
9 "Umeipenda haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta Kwa mafuta ya furaha kupita wenzio."
Hapa, maandiko yanaonyesha kwamba:
Yesu ni Mungu, lakini pia anamtambua Baba kama Mungu wake.
Baba amemtia Yesu mafuta (kumtenga na kumtukuza) zaidi ya wenzake, akimpa utukufu wa kipekee.
Hili linathibitisha nafasi ya Yesu kama Mfalme wa milele, aliye juu ya wote.
Huu ni uthibitisho wa Uungu wa Kristo na pia uhusiano wake wa kipekee na Mungu Baba, akionyesha nafasi yake kama Masihi na Mwokozi wa ulimwengu