Madogima ya kanisa katoliki yanapatikana kwenye Korani. Kama vile RCC inavyomwabudu Maria, waislamu pia humwabudu Maria na hata kwenye Korani yao wamemtaja mara 34. Kumbuka kuwa kanisa Katoliki humwita Yesu kuwa ni mwana wa Maria badala ya Mwana wa Mungu, na Korani pia humwita Yesu kama mwana wa Maria na kukataa kwamba sio Mwana wa Mungu, hata waislamu kama vile wakatoliki wanamwinua Maria kuwa “mkuu” kwa Yesu. Lakini uongo wa namna hii Yesu aliukemea pale aliposema:
Mathayo 22:41-46 “Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? 42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. 43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, 44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? 45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? 46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.”
Wayahudi walikuwa ni vipofu, hata wasijue ya kuwa masihi sio mwana wa Daudi kiuhalisi, bali Mwana Mungu. Hii ni jinsi ileile kama kumzania Masihi kwamba ni mwana wa Maria badala ya Mwana wa Mungu.