Loeb S Mpalasinge
JF-Expert Member
- Dec 1, 2013
- 1,585
- 1,546
Concept ya taifa teule,ilianza wakati wa moses(kama aliwahi kuishi),ni wakati wa moses ndipo jina la mungu jehova lilipojitokeza,
wakati huyu mungu akijitambulisha kwa moses,alisema kuwa kina Abraham,isaka na yakobo hawakumtambua huyo mungu kwa jina la jehova,
hapa unapata kujua wazi kuwa abraham,isaaka na yakobo waliabudu mungu yuleyule alieabudiwa na watu wa caanan,mungu huyo ni El,
na hata abraham kipindi akiwa mgeni pale kaanan,alimtambua Melkizedeki kama kuhani mkuu wa mungu El,
huyo el alikuwa mungu mkuu wa jamii zote za caanan,
sasa unajiuliza kwani jehova aendelea kukubali taifa lake teule litumie jina la mungu wa kipagani?
Jehova anajitetea kwa moses kuwa ,hapo mwanzo kina abraham,isaac na yakobo walinjua kwa jina jingine lakini jina lake halisi ni jehova,
lakini tena ukirudi kuchimba story ya jehova,inaonekana jehova alikuwa ni miongoni wa miungu iliyoabudiwa na kabila la wamedian,Yahwew ama jehova kwa kiswahili alikuwa ni mungu wa vita wa median,kwahiyo inshort alikuwa mungu wakipagani pia,
baada ya moses kumuua mtumishi wa farao alikimbilia nchi ya midian,akakaa kwa miaka mingi,na huko ndiko alipomuoa mkewe zilipa,
baba mkwe wa moses alikuwa ni kuhani wa mungu yahwew ama jehova kwa kiswahili,
so huko median ndiko hasa concept ya mungu jehova alipoitoa moses,
na ni hapo ndipo concept ya taifa la mungu ilipoanza
Shukrani mkuu wa ushauri mzuri....Nje ya kujadili na kukosoa imani za watu wengine huwa huna kazi ya kufanya?Au ndivyo mnafundishwa pale kwenye chuo cha Ahsante Nkapa pale Morogoro?Why don't you invest more of your time trying to solve the problems facing your religious community in which ignorance and poverty are persistent?Ukiyafanya hayo hakika utapata thawabu kwa Mnyazi Mungu na jamii yako itapunguza chuki kwa jamii zilizo busy kujishughulisha na maendeleo yao kiuchumi,kiroho na kijamii.
Ni ushauri tu ndugu yangu!
Mkuu labda sijaeleweka hakuna mahali nimesema Mungu kavunja AGANO na Abraham na IsraelKuna kitu kimoja kingekuwepo kama kusingekuwa na Israel yenye waisrael.
# Mungu angeprove kwamba ni muongo.Maana aliweka agano na Ibrahim.
Kwamba ahadi alizomwahidi Ibrahim hakuweza kuzisimamia.
# Kwa hio hii nchi ingekaliwa na watu wengine hata hio Habari ya hakuna Mungu ingeanza kuwa na mashiko,,maana kama Mungu angekuwa kafeli kwa wayahudi hata sisi tungekuwa na mashaka ya kumuamini.
Lakini sivyo ilivyo maana yote aliosema Mungu yapo vile vile na ameprove kwamba sio muongo na kila alichosema kiko vile vile.Sio Mungu wa kusadikika.Yupo..
Mkuu umeiva, kifupi tu waisrael wa mashariki ya kati Mugu kawalaani.AFTERMATH
Hivyo basi kwa kuwa Mungu alikwisha dhamiria kurudisha uhusiano na mwanadamu ikabidi ageukie mataifa mengine ambayo ndio yangeendeleza agano lile na hapo ndipo likapatikana agano jipya ambapo neema ya wokovu haukuwa wa Wayahudi pekee sababu walimkataa bali ukawa wa mataifa yote as long as watamfuata Yesu (Yohana 1:11-12) pia Mathayo 21:42-43 ambapo tunaona ufalme wa Mungu umehamishwa kutola Israel kwenda kwa mataifa mengine.
42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?
43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
View attachment 929907
Swali linaibuka je Israel inabakia taifa la Mungu??
NDIO ni kweli Mungu aliendelea na agano na taifa la Israel ila tafsiri ya taifa la israel ni lipi limebadilika kupitia agano jipya.
Warumi 9
6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.
7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;
8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.
Na pia hapa ndipo tunaona kunazaliwa waisraeli wa kimwili (mashariki ya kati) na Israel ya Kiroho (wakristo)
Warumi 2:28-29
28 Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;
29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Hivyo kufikia hapa tunaona kuna wayahudi/waisrael aina mbili sasa je ahadi za ISRAEL ya agano la kale anarithi nani za kuwa taifa teule,chaguo la Mungu n.k
Galatia 3
6 Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
.......................................
13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.Ahadi kwa Abrahamu
..............................
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Kupitia mistari hii tunaona sasa ahadi zote walizopewa Abraham na Israel zinarithiwa rasmi na wale wote wamfuatao Yesu yaani wakristo ambao ndio wale paulo kawaita waisrael wa Kiroho sio kimwili. Hivyo ningependa nichukue fursa hii kutoa msimamo wangu kwamba Israel hii ya kimwili sio taifa la Mungu na halitokaa liwe unless na wao wamfuate Yesu hapo ndipo watakuwa NCHI YA AHADI na taifa la Mungu. Kwa kuhitimisha kupitia agano jipya ambapo sasa wanaomfuata wote Yesu bila kujali ni muisrael au lah ndio wanakuwa TAIFA TEULE ama ISRAEL hivyo baraka zote ahadi zote na unabii wote wa TAIFA LA ISRAEL sio tena wa hii Israel ya yakobo bali ni wote wamfuatao Yesu kristo na hii ni kwa mujibu wa Biblia.
However upande kinzani unasema Israel ya mashariki ya kati bado ni taifa teule kama zamani na hakuna kilichobadilika na wanatumia mstari huu.
Warumi 3:3-4
3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?
4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,Ukashinde uingiapo katika hukumu.
Nakubaliana na Mstari huu unaosema Mungu hajawaacha wayahudi licha ya kumkataa lakini bado msimamo uko pale pale kwamba ni lazima wamkiri massiah ndio wawe teule till then hawana tena hadhi ya kuitwa taifa teule kulingana na vifungu nilivyoweka.
View attachment 929908
ANGALIZO
Kumekuwa na interpretation nyingi sana za unabii kuhusu Israel ya kimwili yaani hii ya mashariki ya kati na nina hofu kuwa na wakristo pia wameingia mkenge kama wa wayahudi wa kale kwa kutoelewa unabii na wakatafsiri kwa akili zao kiasi kwamba Yesu alipokuja hawakujua na wakamkataa. kuna wakristo wengi leo wanaamini vita na matetemeko yaliyotabiriwa kwenye ufunuo ni ya kimwili au hekalu litajengwa kimwili hivyo watashituka Yesu amekuja kivingine wao bado wanasubiri vita ya amragedon sijui kujengwa hekalu ilihali hizo mambo zina maana tofauti kabisa ingawa hii ni mada ya siku ingine ila nachoweza hitimisha ni kwamba Biblia imeandikwa kwa codes nyingi hivyo kuitafsiri inahitaji umakini na utulivu sana sio kwenda kichwakichwa mfano inapotabiri kuwepo kwa njaa na kiu haimaanishi njaa ya kimwili ila ukisoma Amos 8:11 utajua njaa inaongelewa ni ya kusikiliza neno la Mungu such phrases mtu akisoma kwenye ufunuo ana conclude kuwa kutakuwa na njaa,vita matetemeko,ukame huu wa kimwili kumbe zina maana nyingine kabisa hivyo nilitaka kuliweka hilo sawa. Kwa kusema hayo naomba kuwasilisha mada kwa ajili ya michango na maoni ya wanajukwaa letu pendwa.
Cc cc Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Mkuu nashukuru kwa mchango wako ila labda tuwekane sawa....Asante sana mkuu zitto junior kwa mada hii pia pole kwa kejeli ya mdau mmoja hapo juu.
Umeelezea vizuri sana kwa kile kilichoitwa taifa teule hakipo tena kijiografia bali kiroho. Lakini kule kuwepo kiroho kwa siku hizi hakutaondoa ile ahadi alioahidi Mwenyezi Mungu kwa Ibrahim.
Yametokea mambo mengi sana tokea kipindi kile mpaka ujio wa Kristo,na tokea Kristo mpaka leo hadi kiyama.
Unaweza kua zile kabila 12 za yakobo zilizo zaa Israeli hazipo tena katika umoja ambao ungezaa taifa lakini katika ufalme ule wa Mungu israel hatakosa kiti chake iwe ameamini Kristo ama laa.
Kule kuamini kwetu kristo sisi wa mataifa mengine ndio kumetupa nafasi ya kuwa taifa teule la Mungu hata kama kimwili hatukutahiriwa .
Lakini tujue toba ya israel inaweza kukubaliwa kwa haraka zaidi kuliko mwingine kwa sababu Mungu yeye alisema ni Mungu anaetimiza makubaliano.
Alisema pia mwingine anaweza kumwadhibu kwa gango iwapo akipotea lakini Israeli anamudhibu kwa fimbo nyembamba kumrejesha.
Nafasi ya israeli kwa Mungu sio ndogo kwa sababu ya ahadi/agano.
Nafasi kwa Mkristo kwa Mungu sio ndogo kwa sababu ya kuamini.
Wale wote (YESU) waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyaka wana ambao si kwa nguvu ya mwanadamu bali kwa nguvu ya Mungu mwenyewe.
Shida ilianzia toka tumboni mkuu Na Mama yao Rebeka alikua anajua kwani alijulishwa na BWANA baada ya kuuliza Soma mwanzo 25:21-23 angalau ni nje ya madaNafikiri shida ilianzia kwa Esau alipokubali kuuza haki yake ya uzao wa kwanza ndio ikampa confidence Yakobo kuwa yeye ndio anastahili baraka za ''first born'' ikapelekea atumie ujanja mwingi ili aweze kutumia hiyo fursa aliyoachiwa na Esau.
Pili kwenye Biblia Mungu alikuwa anaheshimu sana maamuzi ya watu wake mfano Nuhu alimlaani Canaan kisa dhambi ya baba yake yaani Ham na Mungu aliitimiza laana hiyo kwa kuangamiza kizazi chote cha canaan kupitia Israel.....
So Mungu habariki wizi bali ametuachia free will ya kuamua hatma yetu yeye anasimamia tu.... Sasa Isaka ndio kambariki Yakobo hapo Mungu azuie tena ilihali ni maamuzi ya Isaka mwenyewe!!! Ila kama wamgemshirikisha Mungu kabla ya kutoa hizo baraka huenda ndio Mungu angeingilia na kumpa haki yake Esau!!
Muhimu hapa ni kumshirikisha Mungu mapema ndio hatoruhusu walaghai kama Yakobo kujipenyeza.
Nashukuru kwa hoja na ukaribisho wako.Mkuu nashukuru kwa mchango wako ila labda tuwekane sawa....
1. Majibu yangu yote ni kwa mujibu wa AGANO JIPYA hiyo bold ya kwanza ningeomba tusaidiane umeisoma wapi kwenye Bible kuwa muisrael ataenda mbinguni hata kama hajamkubali Yesu??
Yohana 14:6
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Sasa naomba tusaidiane mstari ambao unasema mtu anaweza kwenda mbinguni bila kumkubali Yesu???
2. Pia umesema toba ya israel husikilizwa haraka sababu Mungu anatimiza agano..... Sijakataa toba ya Israel au agano la israel kuwa halitimizwi bali hoja yangu najikita ISRAEL ni nani.... Je warithi wa agano la Abraham ni nani??
Galatia 3
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
Sasa tunafahamu wenye imani kwa Mungu agano jipya ni wakristo sababu walimuamini Yesu sasa hao wayahudi ni lini walimuamini Yesu?? Kama hawana imani huoni automatically sio watoto wa Abraham
Galatia 3
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Hivyo ningeomba unionyeshe wapi kwenye agano jipya ambapo Israel ya netanyahu iliwahi kuwa ya wakristo ili wawe watoto wa Ibrahimu
Kwa kuhitimisha ningeomba pia unipe maana ya mstari huu
Mathayo 21:43
42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?
43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake
Je biblia ina maana gani kusema ufalme wa Mungu umeondolewa kwa Israel kwenda mataifa mengine.....
Karibu kwa mjadala
Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo maana inagusa moja ya topic zenye utata katika ulimwengu wa imani ila ningependa tusome kwa utulivu uzi wote alafu tujadiliane kwa hoja ili tuweze kusolve hili swali la karne nyingi sasa.
View attachment 929882
UTANGULIZI
Mwanzoni kulikuwa na agano kati ya wanadamu na Mungu kupitia Adam ila tunaona Adam analivunja agano hili
(Hosea 6:7)
Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu;
Hivyo Mungu alitaka kurudisha uhusiano tena na mwanadamu tunaona akapatikana Nuhu ambaye alimcha Mungu sana na akachaguliwa kuianza dunia upya baada ya gharika. Sasa baada ya gharika dhambi ilirudi tena kupitia Ham ambaye alipelekea Nuhu kumlaani mwana wake Ham yaani canaan kuwa atakuwa mtumwa wa kaka zake Ham yaani Shem na Yapheth (Hili la muhimu sana huko mbeleni) hivyo uzao wa Ham ukawa na watu waovu sana mfano Nimrod wa Babylon aliyeleta ibada za sanamu na dini za kipagani hadi kuleta machafuko kwenye ukoo wa Nuhu na kusababisha dunia nzima kumuacha Mungu wa Nuhu.
Katika sintofahamu hii aliyesimama imara alikuwa Shem/Melchizedek ndie aliendelea kushika wokovu na hata Abraham alipozaliwa aliendelea kumsimamia kiimani na hivyo hata alipokufa Abraham kati ya wanadamu wengi ndio aliendeleza imani ya kumuabudu Mungu wa babu zake (YAHWEH) hivyo baada ya Mungu kuona Abraham ana msimamo thabiti kwake akampa ahadi ya kuwa na uzao wa watu wengi kama nyota za angani lakini pia alimpa ahadi ya kumpa nchi hii ya canaan.
Mwanzo 15
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Hivyo ni kupitia ahadi hii ndipo taifa la Israel lilipotabiriwa rasmi kuwepo. Na ahadi hiyo itakuja kutekelezwa na mjukuu wake yaani Yakobo ambaye aliiba urithi wa mtoto wa kwanza hivyo hii baraka ya Abraham akairithi yeye na tunaona uzao wake kupitia Joshua na Caleb ndio wanaingia kwenye nchi hii ya canaan rasmi na kuasisi taifa la Israel.
Je Mungu aliichagua Israel??
Kumb. La torati 7:6
6 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.
Kupitia mstari huu tunaona Israel ilichaguliwa na Mungu lakini je kwanini aliichagua??
Kumb. Torati 7:7-8
7 BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote;
8 bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu.
Hivyo Mungu aliwachagua Israel sababu hiyo ya kutimiza uapo kwa mababu ikiwemo Nuhu + Abraham. Na hili ndio lilisababisha Israel wapewe nchi ya Canaan sababu ilikuwa inahitimisha unabii wa Nuhu kuwa Canaan atakuwa mtumwa wa shem (Babu wa Abraham) na sio kwa sababu nyingine yeyote.
Mwanzo 9
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake
View attachment 929883
Ramani ya canaan
Hivyo baada ya Agano hili na Israel ambalo kupitia wao ndio Mungu alipanga kuwaletea Messiah yaani Yesu ili aweze kurejesha uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu kama wa kipindi cha Adamu lakini wayahudi walimkataa Yesu kwa sababu hawakujua kutafsiri unabii ulioandikwa kuhusu maisha ya Yesu kwenye agano la kale. Kwa kifupi maisha yote ya Yesu kuanzia kuzaliwa mpaka kufa yalikuwa yanaendana na unabii wa agano la kale 1 korinto 15:1-4 Mfano wa nabii zilizotimizwa kupitia maisha ya Yesu ni hizi. Kuanza mahubiri yake galilaya ulitabiriwa na Isaya 9:1-2 na ukatimia Mathayo 4:13, Pia Yesu kupanda Punda kuingia jerusalem ulitabiriwa na Zakaria 9:9 na kutimia Mathayo 21:1-9 n.k yaani kuna mistari zaidi ya 100 iliyotabiriwa kuonyesha Huyo Messiah ataishije.
Lakini wao wayahudi hawakuliona hili sababu walidhani Yesu atakuwa handsome boy, Damu ya kifalme,Mwanajeshi kama alexander the great n.k hivyo kwa jinsi alivyokuja "kimasikini" wakaona kama anakufuru mwisho wa siku wakamuua na yote ni kutokana na kushindwa kutafsiri maandiko ya unabii.
Matendo 13:26-27
27 Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.
asante mkuu ntapita kwa neema ya Mungu.Wakuu Pendael24 na Mnabuduhe nimependa hoja zenu zilizoshiba ingawa ntakuwa na maswali kidogo ili twende pamoja.
Meanwhile wakuu mitale na midimu Son of Gamba mpitie hizi hoja.
Nashukuru kwa hoja na ukaribisho wako.
Naomba ukumbuke agano la jipya ni marejeo ya agano la la kale kwa wale walioandika agano jipya.
Wakichofanya ni ku compare yale yaliosemwa zamani yawe katika wakati uliopo.
Paulo Alikua anawaambia warumi si kwamba Neno la Mungu limetenguka kwa sababu si wote waisraeli walio uzao wa israel (naiongeza mimi si wote walio wakristo watokanao na kristo)
Alichokua akiangalia Mungu ni Ahadi rejea sura 9-9 warumi.
Naomba niegemee agano la kale zaidi sura ya 31- 3 Yeremia Mungu anasena hivi "naam nimekupenda kwa upendo wa milele"
Mkuu nadhani unaelewa maana ya neno milele.
Na aliekua akiambiwa amependwa kwa upendo wa milele ni israeli alie mzao wa ibrahim kulingana na warumi 9:9 "maana ahadi ni yenyewe ni hii, wakati maalam nitarudi nae sara atapata mtoto".
Sura ya 31:20 yeremia anaandika "je efrahim si mwanangu mpendwa? Maana kila nisemapo neno ninamkumbuka sana, kwa sababu hio moyo wangu unataabika kwaajili yake BILA SHAKA NITAMREHEMU. Asema Bwana.
Mpaka hapo mkuu unaona nafasi ya Rehema ilivyo kubwa mpaka moyo wa Mungu unataabika kwaajili ya mzao wa israel.
Mungu alitoa ahadi ya Upendo wa milele kwa israeli na ujajua wazi kabisa Mungu hasemi kitu asicho kitekeleza.kwa hali kama hiyo mkuu atashindwaje kumsamehe israeli kwa kosa lolite?
Sura ya 31:27-28 Yeremia anaandika "Mwenyezi Mungu asema hivi, tazama siku zinakuja nitakapoijaza nchi ya israeli na yuda watu na wanyama. 28"kadiri nilivyokua mwangalifu kuwang'oa kuwaboma kuwaangsha kuwaharibu na kuwatesa ndivyo nitakavyokua mwangalifu kuwapanda na kuwajenga.
Sura ya 31:36 Yer. Mwenyezi Mungu asema hivi "mimi hulifanya jua liangaze mchana, mwezi na nyota vimulike usiku. Pia mimi huitikisa bahari nayo hutoa mawimbi: jina langu mimi ni Mwenyezi Mungu wa majeshi. Basi nami nasema KADIRI NINAVYOTEGEMEZA MIPANGO HIO YOTE YANGU, KADIRI HIO HIO ISRAEL WATAKAVYOBAKI KUWA WATU WANGU.
31:37 Yer kama mbingu zinawezekana kupimwa na misingi ya dunia kuchunguzwa basi nitawatupilia mbali wazawa wa israel kwa sababa ya mambo yote walionitenda. Mimi mwenyezi Mungu nimesema.
Ndugu yangu zitto junior na wadau wengine, kwenye Biblia inapotaja dunia ujue ina maana ya ulimwengu.
Mimi nawe tumeshuhudia zama zetu ukuwaji wa tecnologia lakini hijaweza kuupima au kuuchnguza msingi wa ulimwengu na wala anga halijajulikana kwao.
Mungu aliahidi kama utakujawezekana kuupima msingi wa mbingu ndipo atakapowatupa wana wa usrael.
Mstari ule wa 36 ametaja nmna anavyofanya kazi mf kuitisa bahari kuamrisha jua na mwezi na nyota kuwa sehemu yake kwa mpangilio ameahidi kwa namna hio hio anavyotenda ndivyo atakavyowahifadhi wana wa israel.
Mpaka hapo hakuna shaka juu ya israeli kwamba nafasi yake kwa Mungu sio ndogo.
Swali ambalo halina majibu ni kwa sasa hao wana wa israeli waliotajwa ndio hawa tulio nao sasa?
Rejea rumi 9:9 kwamba ahadi ilikua mahsiusi kwa mwana wa sara never otherwise.
Karibu mkuu.