SpraggaBenz
Member
- Dec 13, 2011
- 16
- 7
1.hoja yako ya kwanza inasema kuna nabii juu ya Israel hazijatimia na kwamba kuna agano la Ibrahim bado Mungu analisimamia. Hii ni hoja nzito sana mkuu lakini kwenye uzi wangu hakuna mahala nimekataa kuwa agano kati ya Mungu na Abraham limekufa ILA nilichosema na ndio mzizi wa mjadala ni NANI MRITHI WA BARAKA ZA ABRAHAM.... Je Israel ni ipi???Salamu wana jamvi,
Naomba nianze kuchangia mada hii nikionyesha msimamo wangu na imani yangu kuwa 'Israel hii ya leo bado ni taifa teule la Mungu. Pamoja na michango ya wanajamvi humuna mleta mada kujaribu kushawishi kwa maandiko kuwa Israel hii ya akina Netanyahu si lolote si chochote,na kuwa kanisa la leo ndio Israel mpya.Pamoja na dhumuni la YESU KRISTO kuja duniani kumkomboa mwanadamu hiyo bado haitoshi kulifanya kanisa kuwa Israel kamili hoja za kuunga mkono msimamo wangu ni nyingi na mojawapo ni hizi mbili.
1.Yako mambo yaliyotabiriwa tangu agano la kale hayajatimia na utimilifu wake utafanyika katika Israel hii hii ya akina Netanyahu na tena pale YESU atakaporudi mara ya pili.Hebu tutafakari hii kitu inyoitwa the GOLDEN GATE/EASTERN GATE OF JERUSALEM ambayo imendikwa ndani ya Biblia kwenye EZEKIEL 44.1-2 Nabii Ezekiel alioneshwa kwenye maono kuwa huo mlango/gate la mashariki halitafunguliwa mpaka atakaporudi YESU na sababu zake zikatolewa(Soma Ezekiel 44:1-2) na maandiko mengine nitawaletea na waarabu walishajaribu sana kubomoa huo mlango wa mashariki imeshindikana(Google ujisomee mwemyewe). Hivyo hoja yangu ni kuwa yapo maagano ambayo Mungu aliyaweka tangu enzi za akina Ibrahimu ambayo mpaka sasa yadumu kusubiri kutimia,wapi kama sio ISRAEL ya leo,na mengine mengi.
2.Dunia nzima inafahamu kuwa Israel ya leo ndio yenye wanasayansi bora kabisa waliotapakaa Ulaya na Amerika wakifanya mambo makubwa,kwa mfano inasemekana(sina uhakika) lakini haya yalitamkwa na Waziri mkuu wa Israel kuwa siku za karibuni kuwa katika makampuni makubwa 10 bora duniani ya IT,Telecom,Energy etc,yaliyoko Marekani matano yakiwemo(Yahoo,Whatsapp,Microsoft etc) yana research centres Tel Aviv hii ya leo,Kwa nini? Wazungu wa ulaya na Amerika wanaijua Israel hii ya leo mnayoipinga kuwa inazo zile baraka za Mungu kupitia Ibrahimu na uzao wake.Nani asiyejua kuwa modern agricultuere iko Israel,Jeshi lenye nguvu ni huko.Jamani habari za hili taifa la Isarel wanazijua waarabu wanaoizunguka Israel kama kweli hii Israel ya leo ndio ile ya ahadi ya Mungu?
Nimalize kwa kusema ahadi ya Mungu ni ya milele kanisa la leo kama Israel mpya limeandaliwa kwa ajili ya uzima wa milele baada ya maisha ya hapa duniani,
Nawasilisha, nitarudi
Hapana mkuu unabii kutimia sio justification ya ubaya unaofanyika.... Yesu angeweza kukubalika na waisrael wote ila angeuawa na hata warumi ila shida inaanza pale warumi waligoma kumuua walimuona hana kosa ila wayahudi wenyewe ndio wakamsaliti ukizingatia alitumwa kwao kuwakomboa!!! Hapo ndio shida ilipoanzia. Na ndio maana Yesu akasema haya baada ya kumkataa.Mie siyo msomaji sana wa maandiko ya dini lakini nimewahi kusikia Yesu toka anatoka mbinguni ilikuwa ni lazima aje afe kama kafara ya utakaso wa dhambi za wanadamu, kwa hiyo swala la wayahudi kumuua sifikiri linafaa kuwahukumu kwalo kwa sababu kama alishushwa Israel tutegemeeje angetimiza hiyo kafara ya kifo kwa kuuliwa na walesotho? Bila Shaka hilo lisingekuwa rahisi.
Mkuu jikite kwenye Biblia hayo ya kushinda vita sio necessairily kwa kuwa ni taifa teule bali msaada wa marekani tu unawaweka mjini ukitaka kufahamu hilo jiulize kwanini kabla wapagani (SIO MUNGU) hawajawapa Israep ardhi ya palestina walikuwa wanatandikwa kila siku.Wakuu,
Mimi niseme tu kuwa pamoja na madhaifu yao yote ujeuri walionao,na hata kumkataa YESU KRISTO wakidai bado wanamsubiri mesiah wao,hiyo haiondoi kuwa wao ni taifa teule na baraka alizowatamkia Mungu na maagano aliyoyaweka toka enzi za agano la kale hayajaondoka wala kutenguliwa,ukitaka kuamini kuwa Israel hii ya sasa ndio ile ya kwenye agano la kale nenda kaanzishe vita na wao, au panga njama yeyote ya kulidhuru taifa lao hapo ndio utajua kama Mungu wa baba zao akina Ibrahimu ndio huyu wa akina Netanyahu.
Mungu ni yeye yule jana leo na hata milele,chokoza Israel kama hautauona mkono wa Mungu ukiwatetea, haya mataifa mengine Mungu alituhurumia tu akasema hawa nao ngoja tu warithi baraka za Ibrahimu ingawa hizo baraka mpaka leo huku Africa na kwingineko tunazisoma na pengine hatuziishi ipasavyo
Mkuu una hoja nzito sana lakini mimi ningejikita mstari huu wa hicho kifungu cha 9:9Nashukuru kwa hoja na ukaribisho wako.
Naomba ukumbuke agano la jipya ni marejeo ya agano la la kale kwa wale walioandika agano jipya.
Wakichofanya ni ku compare yale yaliosemwa zamani yawe katika wakati uliopo.
Paulo Alikua anawaambia warumi si kwamba Neno la Mungu limetenguka kwa sababu si wote waisraeli walio uzao wa israel (naiongeza mimi si wote walio wakristo watokanao na kristo)
Alichokua akiangalia Mungu ni Ahadi rejea sura 9-9 warumi.
Naomba niegemee agano la kale zaidi sura ya 31- 3 Yeremia Mungu anasena hivi "naam nimekupenda kwa upendo wa milele"
Mkuu nadhani unaelewa maana ya neno milele.
Na aliekua akiambiwa amependwa kwa upendo wa milele ni israeli alie mzao wa ibrahim kulingana na warumi 9:9 "maana ahadi ni yenyewe ni hii, wakati maalam nitarudi nae sara atapata mtoto".
Sura ya 31:20 yeremia anaandika "je efrahim si mwanangu mpendwa? Maana kila nisemapo neno ninamkumbuka sana, kwa sababu hio moyo wangu unataabika kwaajili yake BILA SHAKA NITAMREHEMU. Asema Bwana.
Mpaka hapo mkuu unaona nafasi ya Rehema ilivyo kubwa mpaka moyo wa Mungu unataabika kwaajili ya mzao wa israel.
Mungu alitoa ahadi ya Upendo wa milele kwa israeli na ujajua wazi kabisa Mungu hasemi kitu asicho kitekeleza.kwa hali kama hiyo mkuu atashindwaje kumsamehe israeli kwa kosa lolite?
Sura ya 31:27-28 Yeremia anaandika "Mwenyezi Mungu asema hivi, tazama siku zinakuja nitakapoijaza nchi ya israeli na yuda watu na wanyama. 28"kadiri nilivyokua mwangalifu kuwang'oa kuwaboma kuwaangsha kuwaharibu na kuwatesa ndivyo nitakavyokua mwangalifu kuwapanda na kuwajenga.
Sura ya 31:36 Yer. Mwenyezi Mungu asema hivi "mimi hulifanya jua liangaze mchana, mwezi na nyota vimulike usiku. Pia mimi huitikisa bahari nayo hutoa mawimbi: jina langu mimi ni Mwenyezi Mungu wa majeshi. Basi nami nasema KADIRI NINAVYOTEGEMEZA MIPANGO HIO YOTE YANGU, KADIRI HIO HIO ISRAEL WATAKAVYOBAKI KUWA WATU WANGU.
31:37 Yer kama mbingu zinawezekana kupimwa na misingi ya dunia kuchunguzwa basi nitawatupilia mbali wazawa wa israel kwa sababa ya mambo yote walionitenda. Mimi mwenyezi Mungu nimesema.
Ndugu yangu zitto junior na wadau wengine, kwenye Biblia inapotaja dunia ujue ina maana ya ulimwengu.
Mimi nawe tumeshuhudia zama zetu ukuwaji wa tecnologia lakini hijaweza kuupima au kuuchnguza msingi wa ulimwengu na wala anga halijajulikana kwao.
Mungu aliahidi kama utakujawezekana kuupima msingi wa mbingu ndipo atakapowatupa wana wa usrael.
Mstari ule wa 36 ametaja nmna anavyofanya kazi mf kuitisa bahari kuamrisha jua na mwezi na nyota kuwa sehemu yake kwa mpangilio ameahidi kwa namna hio hio anavyotenda ndivyo atakavyowahifadhi wana wa israel.
Mpaka hapo hakuna shaka juu ya israeli kwamba nafasi yake kwa Mungu sio ndogo.
Swali ambalo halina majibu ni kwa sasa hao wana wa israeli waliotajwa ndio hawa tulio nao sasa?
Rejea rumi 9:9 kwamba ahadi ilikua mahsiusi kwa mwana wa sara never otherwise.
Karibu mkuu.
Naona wakuu bado sieleweki narudia tena ISRAEL NI TAIFA TEULE na AGANO LA MUNGU NA ISRAEL HALITOISHA KAMWE ila mzizi wa hoja yangu ni ISRAEL NI NANI???Ni vema kutofautisha kati ya taifa la Mungu na taifa teule. Wayahudi ni taifa teule. Hilo haliwezi kubadilika. Baadhi yao wapo kwenye taifa la Mungu.
Mungu alitwaa mwili kama Myahudi na akakaa nasi. Aliliteua taifa la Wayahudi kwa tukio hilo. Ni kitu kisichobadilika. Kwa maana hiyo, Israel ni taifa teule milele.
Taifa la Mungu ni wote wale waliopo katika Kanisa lake. Wapo Wayahudi wachache na watu wengi wa mataifa.
There is a non-empty intersection between taifa teule na taifa la Mungu but neither set contains the other.
Wayahudi sio kwamba watakua na upendeleo wakwenda mbinguni Kama hata wakifa katika Dhambi.....Kama hawatotubu na kumkiri kristo nao wataangamizwa katika Moto wa milele....ila hata kwa uasi wao walionao hivi Sasa bado ile Hali ya kuitwa taifa teule bado ipo ila haiwafanyi kuwa Bora zaidi ya wengine katika maswala ya kiimani Kama hawatotubuMkuu Mnabuduhe nimeona hoja yako nzito na natamani wana JF hada kwenye mada za kiimani waige mfano wako kwamba licha ya kuwa mara nyingi tuna misimamo tofauti ila unaapproach mada kwa utulivu na hoja sio jazba na mahaba ya kidini kwa hilo nikupongeze sana
Back to mada nimeona mengi ila ntajikita kwenye swali lako kwamba hakuna mahali kokote Biblia inasema wakristo ni taifa teule
Tuanze kwa ahadi ya Mungu kwa Israel
Kutoka 19:5
5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,
6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu
Sasa basi tuangalie ahadi hii amepewa nani ya kuwa taifa takatifu baada ya Yesu kukataliwa na wayahudi.
1 Peter 2:7-10
7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,Jiwe walilolikataa waashi,Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
......................
9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.Ishini kama Watumishi wa Mungu
Sasa swali hapa ili twende sawa je kama agano jipya kupitia petro anasema kuwa waaminio ndio taifa teule yaani wakristo Wa makanisa 5 waliokuwepo Asia ya magharibi ambao hawakuwa wayahudi je ina maana alikuwa anawapotosha mkuu??
Na kama amesema waaminio ndio taifa teule je ni lini wayahudi hawa wa kimwili wamekuwa waaminio wa kristo?? Na kama hawajawahi je wanapataje uhalali wakuitwa taifa teule??
Labda tuanzie hapa kwanza ili twende pamoja.... Natanguliza shukrani
HahahahaTaifa hilo limejaa matapeli na wavuta bange
Wayahudi sio kwamba watakua na upendeleo wakwenda mbinguni Kama hata wakifa katika Dhambi.....Kama hawatotubu na kumkiri kristo nao wataangamizwa katika Moto wa milele....ila hata kwa uasi wao walionao hivi Sasa bado ile Hali ya kuitwa taifa teule bado ipo ila haiwafanyi kuwa Bora zaidi ya wengine katika maswala ya kiimani Kama hawatotubu
Okay kama Israel ya kina Netanyahu ndio taifa teule na sio kanisa ina maana hapa Petro alipotosha aliposema wakristo wa makanisa matano kulea Asia nao ni TAIFA TEULE na TAIFA TAKATIFU ilihali alijua sio watoto wa Yakobo?? Na kama hakupotosha je tuchukue lipi kati yao kuwa ndio taifa teuleMkuu Zitto, asante kwa kuchuja hoja yako na kusema swali lako hitimisho lake ni jibu la swali hili: "Israeli ni nani?"
Kwenye historia ya wokovu, Israeli ni Yakobo, mtoto wa Isaac, mtoto wa Abraham. Bila shaka umesoma simulizi la jinsi Mungu alivyofanya agano na Yakobo na kumwambia tangu sasa utaitwa Israel. (Genesis 32:22-32)
Kwa hivyo basi, kihistoria ni kwamba Waisraeli ni kizazi chote cha Yakobo. Kiimani, kuna mnyambuko wa neno Israeli. Ni mnyambuko wa Kitheolojia ambao unahitimishwa kwa kusema Kanisa ni Israeli mpya.
Wayahudi wote ni kizazi cha Yakobo. Kwa hivyo kihistoria ni Waisraeli, hata kama wengi wao hawakubali kwamba Yesu ndiye Masia waliyemsubiri.
Kwanza inabidi tukubaliane kwamba sisi wakristo wakovu tumeupata kwa neema ,kwani waliokusudiwa kumpokea Masihi walikua waisraeli....sisi wakristo pia ni taifa teule kiroho maana sisi ndio tuliopokea ufalme wa Mungu toka kwa waisraeli...ukisoma Mathayo 21 :33-46 hoja yako inakua Ina nguvu kabisa kwamba Kuna kuhama kwa utaifa katika ulimwengu wa Roho hapo naunga mkono hoja yako, Sasa tuje kwenye hii Israeli yakina Netanyau.Okay kama Israel ya kina Netanyahu ndio taifa teule na sio kanisa ina maana hapa Petro alipotosha aliposema wakristo wa makanisa matano kulea Asia nao ni TAIFA TEULE na TAIFA TAKATIFU ilihali alijua sio watoto wa Yakobo?? Na kama hakupotosha je tuchukue lipi kati yao kuwa ndio taifa teule
1 Peter 2:7-10
7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,Jiwe walilolikataa waashi,Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8 Tena,Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha.Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.
9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.Ishini kama Watumishi wa Mungu
Mkuu labda sijaeleweka hakuna mahali nimesema Mungu kavunja AGANO na Abraham na Israel
Pia nimekubali Israel ni nchi ya ahadi
Pia nimekubali Israel ilichaguliwa na Mungu
Pia nimekubali Israel inahusika na unabii wa siku za mwisho
LAKINI nachohoji Israel ni nani kwa muktadha wa agano jipya.... Je ni lile taifa la kina Netanyahu lililopo pale mashariki ya kati au ni wakristo yaani waliomfuata Yesu.
Na nimeweka hapo mistari juu hivyo jikite hapo je Israel ni nani??
Natanguliza shukrani
Mkuu mi natofautiana nawewe kidogo ukisoma injili ya Mathayo 21 :33-46 unaona Yesu anawaambia mafarisayo kwa mifano ,mifano ambayo ilikua inawahusu kwani yote walifanya na Mfano wa Mwisho unaona mwenye shamba anamtuma Mwana nadhani unajua ule Mfano unamaanisha nini ila pia huyo Mwana wanamuua. Mistari iliyoendelea unaona kabisa Yesu anawaambia ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.Kuna taifa la Israel lenye wayahudi na kuna wakristo waliomwamini Yesu na kuwa kanisa.Mtu anapokuwa amemwamini Yesu hawi mwananchi wa Israel ila anakuwa kanisa.ile kuwa mwana wa Ibrahim hakuondoi haki ya waliokuwa na hio hadhi kiasili ila ni kuiongeza tu idadi ya wana wa Ibrahim..Kwa hio kama Mungu alifanya agano na Ibrahim la milele kwa nchi aliompa ile hadhi haijachukuliwa na kanisa.Bado ile nchi ipo na bado wayahudi wapo.Hao kina Netanyahu ni wayahudi wa asili kabisa na ile ni nchi yao.Na wameachwa wachache kwa mpango ulio rasmi kabisa.
Hapana mkuu imewekwa condition ya kuwa mtoto wa Abraham sio tu mpaka akuzae maana unasema wameongeza namba ya watoto wa Abraham.... Sasa baso tujiulize watoto wa Abraham ni nani??Kuna taifa la Israel lenye wayahudi na kuna wakristo waliomwamini Yesu na kuwa kanisa.Mtu anapokuwa amemwamini Yesu hawi mwananchi wa Israel ila anakuwa kanisa.ile kuwa mwana wa Ibrahim hakuondoi haki ya waliokuwa na hio hadhi kiasili ila ni kuiongeza tu idadi ya wana wa Ibrahim..Kwa hio kama Mungu alifanya agano na Ibrahim la milele kwa nchi aliompa ile hadhi haijachukuliwa na kanisa.Bado ile nchi ipo na bado wayahudi wapo.Hao kina Netanyahu ni wayahudi wa asili kabisa na ile ni nchi yao.Na wameachwa wachache kwa mpango ulio rasmi kabisa.
Wakatoliki na Orthodoxy wana tofauti gani?Wayahudi hawamtaTmbui Yesu kuwa masiah hivyo tunajisumbua bure. Wenyewe wanamsubiri masihya ambaye hajazaliwa.
Taifa teule ni lile ambalo liko kwenye biblia lakini siyo lile la agano jipya. Tembelea Jerusalem ndo utajua maana ya ukristo. Ukitaka kujua ukristo zaidi ongea na Orthodox ndo wanaoshikilia sehemu nyingi za Jerusalem. Nimefika na ninauhakika. Wakatoliki wana sehemu ndogo ya umiliki. Wakristo walipigana sana kurudisha Jerusalem kwa wayahudi/wakristo lakini walishindwa.