Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Jina la Yesu lina nguvu sana kuliko unavyoweza kufikiri,Mimi Yesu amenitendea makuu kuna nyakati nimepitia changamoto kubwa Sana kiasi Cha kutaka kukata tamaa, hakukuwa na yeyote wa kunisaidia hata Marafiki zangu walikuwa mbali nami, Tumaini pekee nililobaki nalo ni Yesu Kristo MUNGU na mwokozi wangu, hakika alinisaidia ktk hali isiyoweza kuelezeka kibinadamu.

Ndugu yangu mtoa uzi na wana JF wote mnaosoma comment hizi,mwaminini Yesu Kristo,Ukimwamini atakutendea mambo mengi mema, huwezi kujua ukuu wa Yesu km hujapitia ktk changamoto za maisha ambazo ktk hali ya kawaida ni vigumu kutatulika na unapokaribia kukata tamaa unatokea msaada ambao hukuutegemea kabisa na ktk hali isiyoweza kuelezeka kibinadamu.
 
Naomba kuelewesha maana halisi ya maneno haya ambayo yametumika sana kwenye uzi huu.

1. Mapepo
2. Majini
3. Shetani
 
Ni kweli hata biblia lazima ziko Za feki Na iko halisi lakini ni biblia ipi ya kweli ndio kishindo kuijua kwani Yesu hakuleta biblia wala hakuandika kitabu chochote . Wala Hakuna aliyeandika chochote kuhusu alichosema yeye wakati alipokuwepo
Hio biblia original ipo wapi Ili tuilinganishe na hizi.
Ukitaka kujua biblia jielimishe nini maana ya neno Biblia,waandishi wa injili ni nani.
Unapaswa usome historian ya biblia imetoka wapi.Hii ni shule.
Yesu si mwandishi, mitume wake ndio walioandika Yale aliyosema na kufanya Yesu pili sio KILA kitu kuhusu Yesu kimeandikwa. Kumeandikwa kuzaliwa kwake na alipoanza injili yaani akiwa na miaka 30 hadi 33.
Maisha yake ya ujana, maisha ya mitume kabla awajawa Wakristo hayajaandikwa, sababu si muhimu.
 
True katika shida ndugu na jamaa watakukimbia lakini Yesu na mama mzazi hawawezi kukuacha,ipo siri kuu Kati ya mtoto na mama.
 
True katika shida ndugu na jamaa watakukimbia lakini Yesu na mama mzazi hawawezi kukuacha,ipo siri kuu Kati ya mtoto na mama.
Amen.Kamwe sitamwacha Yesu,nitamng'ang'ania km rubi kwasababu Yeye ni Rafiki wa kweli.
 
Ila hakuna aneweza kuendesha gari, kanuni za usalama barabarani, Ukitegemea Yesu atakuokoa.

Yesu ni imani tu, na kupitia imani watu wamejitengenezea flusa, sasa ni matajili kuliko watu wanaojihangaisha na biashara.
Ndio Yesu ni imani itendayo Kazi kwa anaeamini.
Fursa ni matamanio ya mwanadamu kuilisha nafsi yake.
Si Kwamba wote wanaopata ajali awazingatii kanuni za barabarani.
 
Ndio Yesu ni imani itendayo Kazi kwa anaeamini.
Fursa ni matamanio ya mwanadamu kuilisha nafsi yake.
Si Kwamba wote wanaopata ajali awazingatii kanuni za barabarani.
Bali hawakuwa na imani ya Yesu mioyoni mwao siyo.
Ila mwenzi mmoja nyuma, nilisoma habari ya mchungaji, aliepata ajali, akiwa kwenye gari yake ndogo, baada ya kugongwa na lori.

Abiria wake mmoja alikufa palepale eneo la ajari, mchungaji alifia hospitali.

Labda hii yesu alichelewa kuona wachawi walioisababisha ajari ile mpaka imemuua wakala wake.
 
Kuna dini ina uhusiano wa karibu na mapepo na mashetani, wao ni wapinga Kristo, watapinga kila kitu, watasema Yesu hajawahi kuponya wala kutoa pepo, ili tu aonekane sana na yule karani wa mama mfanyabiashara ambaye alioa katoto ka miaka tisa
Alafu wakezao wanashinda kwa mwamposa 😂😂
 
Umethibitisha vipi hio ajali imesababishwa na uchawi.
Mungu ana namna nyingi za kuchukua watu wake,pili kuwa mchungaji sio tiketi ya kuwa una Yesu, unaweza ukawa kivuli tu au mchungaji feki,kwani ujaona wachungaji wakianguka dhambini mfano kunaswa kwenye uzinzi,ulevi,wizi nk.
Yesu amnyimi mtu ulinzi amuitae
 
Alafu wakezao wanashinda kwa mwamposa [emoji23][emoji23]
Mwamposa anawararua sana hela zenu kwa hizo, Shuhuda.

Kama umeshawahi ule mnada feki wa mabegi na nguo, ndicho anachokifamya mwamposa.

Ukinunu kanga moja unapata ofa beg la mgongoni moja mitandio saba kwa Tsh 1,000 tu.
ukiangalia unaona kweli watu wananunua na wanapewa hizo ofa. wapo wengine huweka TV, Radio kubwa na hata piki piki, Ukiangalia watu wanashinda na wanaondoka na zawadi.

Kumbe huu ni mchezo wa kuwaibia watu wasio werevu, hivyo nikuambie ndugu yangu Mwamposa ni mfanya biashara tu, njia anayopitia ni ya kuaminisha watu ili muamini.

Imani ya mtu haipo kwenye mavazi yake ni vitendo vyake tu, Mwamposa anawatayarisha hao, kama mzee kakobe alivyokua akifanya, kipindi kile cha uponyaji feki wake.
 
Mimi sio muumini wake.
 
Hao watoto waliouliwa na huko Misri ndo kwanza taarifa hizo napata kwako,liweke wazi hili.
Ili la uzinzi wa mtu na watoto umelipata wapi kwangu ni geni
Umeshawahi kusoma Biblia?
 
KILA mtu ana utashi wake na uamua upande autakao kulingana na interest zake.Hakuna mipaka Kati ya nguvu na asili.Mwanadamu ni roho na roho ndio utenda Kazi ndani ya mwanadamu.Roho ni nguvu.dhambi ni roho chanzo ni nguvu hasi.
Nguvu ni Nguvu, Ukiikiuka INATENDA, Ukiitii INATENDA kadri ya Ukamilifu wa hesabu za Utiifu wako au Ukiukaji wako.

Roho ni Ukamilifu/Utakatifu, yaani kutokuwa na dhaifu lolote. Haina baya wala jema, juu wala chini, Haina Nina wala haikosi jina, haina Jana wala Leo. Iko nje ya mipaka yote.

Katika yote hayo vingi vinabaki kuwa Mafumbo au Viini Macho, yaani HAVIPO(shetani, malaika, dhambi, mungu mwema, nk.
 
Ila hakuna aneweza kuendesha gari, kanuni za usalama barabarani, Ukitegemea Yesu atakuokoa.

Yesu ni imani tu, na kupitia imani watu wamejitengenezea flusa, sasa ni matajili kuliko watu wanaojihangaisha na biashara.
Hata gari hakuacha Yesu amfundishe na kumuongoza, alimtafuta Binadamu mwenzake. Kisha wanaimba "amtegemeaye binadamu" hata kwenye ajali, ni binadamu wenzake ndio waliomtoa ikiwezekana kumfikisha hospital.
 
Ni kweli hata biblia lazima ziko Za feki Na iko halisi lakini ni biblia ipi ya kweli ndio kishindo kuijua kwani Yesu hakuleta biblia wala hakuandika kitabu chochote . Wala Hakuna aliyeandika chochote kuhusu alichosema yeye wakati alipokuwepo
Kwani Luka kazi yake ilikuwa ni nini?
 
Nguvu zipo za aina nyingi duniani na zote sins asili.Mada inazungumzia nguvu ya jina la Yesu.Kwa mujibu wa elimu ya mwili au ulimwengu unaonekana wenye kuhitaji ushahidi Mungu, shetani, malaika,dhambi havipo.
Labda nikupe shule kuhusu Roho.Roho inaweza ikawa nzuri au mbaya tegemeana na asili ya hio roho.
Roho ni elimu ya ulimwengu usioonekana huwezi idhibitisha kimwili,kama unatambua uwepo wa roho kwann usitambue uwepo wa Mungu, shetani, dhambi, malaika maana hizi nao ni roho.
 
Roho ni Moja tu. Roho i katika Umoja.

Malaika, Mungu, Shetani, nk ni maumbo ya kufikirika atumiayo binadamu kutafsiri Roho. Kimsingi Hayapo.
Ukisema zipo nyingi, basi kuna kilichofanya kuwa nyingi, na hakika hicho ndio Kikuu zaidi, na ndio Nguvu, vingine vinabaki kuwa viumbe.

Roho ni Ukamilifu, Ni Nguvu, ndio Asili yenyewe. Anayeiita Mungu, ni saw a na anayeiita Shetani, au mzimu. Hata ukiita nyuki, ni saw a tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…