Ni kwa mtazamo wake yeye na si kwa mtazamo wa waamini.
Ni SAwa na wanazuoni wasemao uislamu ulianzishwa na mapadre watano walioasi ukatoliki wakipinga suala la kutooa.
Aramai ilikuwa ndio lugha iliyokuwa ikitumiwa na Mayahudi huko Palestina. Kwa hiyo, inaaminika kuwa Yesu na wanafunzi wake walizungumza na kufundisha kwa Kiaramai. “Simulizi za kwanza ya mdomo za matendo ya Yesu na kauli zake bila shaka zilisambaa kwa Kiaramai.
Hata hivyo, Injili nne ziliandikwa kwa ukamilifu wake kwa maneno mengine, Kiyunani ya kawaida, lugha iliyokuwa ikitumika katika dunia ya Kistaarabu ya Mediterania, ili kutumikia wengi katika Kanisa, ambayo ilikuwa ni ya Kiyunani (wenye kuzungumza Kigriki) badala ya Kipalestina.
Mabaki ya Kiaramai yalikuwepo katika Anaajiyl za Kiyunani.
Kwa mfano, katika Marko 5: 41, “Kisha akamshika mkono, akamwambia, ‘Tal’itha cu’mi’, maana yake, ‘Msichana mdogo, nakuambia amka’”.
Pia Marko 15: 34: “Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, ‘Eloi, Eloi, lama sabachthani?’ maana yake, ‘Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?’” (Encyclopedia Americana, Mj. 3, uk. 654).
Injili ya Marko katika Agano Jipya, japokuwa inachukuliwa na wanazuoni wa Kanisa kuwa ndio kongwe kabisa kati ya Anaajiyl, haikuandikwa na mwanafunzi wa Yesu. Wamehitimisha wanazuoni wa Biblia, kutegemea na dalili zinazopatikana katika Injili, kuwa Marko mwenyewe hakuwa mwanafunzi wa Yesu. Zaidi ya hayo, kulingana na wao, haijulikani kamwe huyu Marko alikuwa nani kwa uhakika.
Mwandishi wa kale wa Kikristo, Eusebius (325 BI), alipokea kuwa mtunzi mwengine wa zamani, Papias (130 BI), alikuwa wa kwanza kuinasibisha Injili kwa John Mark (Yohana Marko), mwandani na mfuasi wa Paul (Paulo).
Wengine wametoa rai kuwa huenda alikuwa mwandishi wa Petro na ilhali wengine wanaona kuwa huenda alikuwa mtu mwengine kabisa.
Hiyo ndiyo hali ya Injili nyingine.
Japokuwa Mathayo, Luka na Yohana yalikuwa majina ya wanafunzi wa Yesu, waandishi wa Injili hizo waliokuwa na majina ya wanafunzi hao mashuhuri, lakini ni watu wengine ndio waliotumia majina yao ili maelezo yao yapate kusadikika.
Kwa hakika, Injili zote zilisambaa hapo awali bila majina.
Baadaye majina yenye kuaminika yalipatiwa kama watunzi wa Injili hizo na watu wasiojulikana katika kanisa za awali.
Vitabu
Watunzi
Gospel of Matthew (Injili ya Mathayo)
Hajulikani (“Japokuwa yupo Mathayo aliyetajwa katika orodha tofauti za wanafunzi wa Yesu… mwandishi Mathayo kwa kiasi kikubwa hana jina” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 824).
Gospel of Mark (Injili ya Marko)
Hajulikani (“Japokuwa mtunzi wa Marko huenda akawa hajulikani…” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 826).
Gospel of Luke (Injili ya Luka)
Hajulikani (“Sheria ya Muratori inamtaja Luka, tabibu, mwandani na mfuasi wa Paulo; Irenaeus anamuonyesha Luka kuwa ni mfuasi wa Injili ya Paulo. Eusebius anamuweka Luka kuwa ni tabibu wa Antiocha, ambaye alikuwa na Paulo ili kuipatia Injili mamlaka ya kiutume” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 827).
Gospel of John (Injili ya Yohana)
Hajulikani (“Kutokana na dalili za ndani, Injili hii iliandikwa na mwanafunzi mpenzi ambaye jina lake halijulikani” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 828).
Acts (Matendo)
Mtuzi wa Luka (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 830.)
I, II, III John (1, 2, 3 Yohana)
Mtunzi wa Yohana (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 830).