Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Nimemtolea mfano, mchungaji Mwamposa, jinsi anavyotumia Shuhuda za uongo kuibia wakristo wenzake.

Wewe umejibu wewe siyo Muumini wake.
Ndiyo nimekuuliza wewe ni muuni wa mtu.
Sikunyingine uweke alama ya kuuliza iliueleweke unamaanisha nini.

Mimi sio muumini wa mtu.
 
Wacheni kudanganyana, someni Biblia...

Mathayo 7:
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Nani aliyeongea maneno haya?
 
Hata Dunia ipinduliwe vipi itabaki kuwa Yesu ni Mungu Mwenye Nguvu


. Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili?

Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika:
Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
1 Wakorintho 15.15


Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja hapa anasema:

"Tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo."

Ikiwa Mungu kamfufua Kristo, hawawezi kuwa wote wawili hao ni mtu mmoja.

Mmoja alikuwa ni mtenda, mfufuaji, na wa pili alikuwa ni mtendwa, mfufuliwa. Kama Kristo ni Mungu mwenye uwezo wa kufufua basi maelekeo ni kusema: "Kristo kajifufua", sio kafufuliwa. Mwenye kufufuliwa ni mfu asiyejiweza kitu.

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume inasimuliwa kuwa Mt Stefano alisema aliyoyaona yaliyo mbinguni. Alisema:

Tazama! naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
Matendo 7.56

Mwana wa Adamu ndiye Yesu, na kwa jina hilo ndio mwenyewe akipenda kujiita, sio Mwana wa Mungu. Hapo basi huko mbinguni Stefano anasema anamwona Yesu kakaa mkono wa kulia wa Mungu. Mwenye kukaa mkono wa kulia wa fulani hawezi kuwa ndiye yule yule fulani. Hayo ni maelezo ya mbinguni. Ni wazi basi kwa ushahidi wa Biblia kuwa Yesu hakuwa Mungu mbinguni kama alivyokuwa si Mungu duniani.

Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:

Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Luka 22.42-43

Hapa tunaona mambo matatu muhimu:

Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu.

Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.

Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: "uniondolee kikombe hiki" cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.

Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu."

Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:
Baba ni mkuu kuliko mimi.
Yohana 14.28

Na mwishoni naye yupo mslabani:
Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
Mathayo 27.46

Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema:

"Mungu wangu naye ni Mungu wenu"? Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake.

La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo. Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.

Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu.
 
Soma biblia inaitwa Red letter Bible. Humo utakuta maneno yote yanayodhaniwa aliyoyasema Yesu yako kwa wino mwekundu.
Mi najua,nataka aliyeweka hapa ndo aseme nani aliyeongea,Na atuambie inahusiana vipi na swali LA mtoa mada!
 
Hili ni swali tu katika kujua uweza na uwezo wa nguvu za Jina la Yesu katika kutenda miujiza.

Yesu alipata kuishi yapata miaka 2019 iliyopita. Je inakuwaje jina lake leo lisemwe kwamba lina nguvu sana katika kutenda miujiza?

Kuna manabii wengi sana na mitume wengi wamepita, kina Krishna, Elisha , Elizabeth Mtishbi nk mbona hatusikii visa vya majina yao katika kutenda miujiza? Sanasana Wlisha ametajwa mara moja kwamba jamaaa walibeba maiti wakienda kuzika, walipofika katika kaburi la Elisha ikatokea vita, katika kujinusuru wakaibwaga maiti chini, maiti ikaangukia kaburi la Elisha, maiti ikafufuka, ikatoka nduki kichizi.

Ndugu mnaoelezea uweza wa jina la Yesu njooni hapa mshuhudie
Jina lipitalo majina yote lina nguvu ya ajabu.
Hii nguvu ya Yesu inaogopwa na walio kuzimu na ambao ni wafuasi wa yule mwovu, Ibilisi.
Kwa Jina la Yesu watu wanapona
wanaokoka
wenye mapepo yanakimbia
Jina la Yesu lina nguvu iwezayo kuhamisha milima.
Mkuu kazi yako ni kuamini, kulikubali na kulitukuza.
 
Kuna dini ina uhusiano wa karibu na mapepo na mashetani, wao ni wapinga Kristo, watapinga kila kitu, watasema Yesu hajawahi kuponya wala kutoa pepo, ili tu aonekane sana na yule karani wa mama mfanyabiashara ambaye alioa katoto ka miaka tisa
Acha udini.
 
Kati ya wakristo na Waislamu, wafuasi wepi wanaongoza kuanguka mapepo kwenye nyumba zao za ibada Kama sio nyie wakristo?!!

Wakristo mna mapepo mengi Sana sababu mnaongoza kwa kila uchafu na kutembea nusu uchi pia, nyie mnamiliki majini maovu wengi kwenye majumba yenu ya ibada kuliko Waislamu, wamiliki madanguro mjini karibia wote wakristo, Sinza pale bar karibia zote na club Ni za wakristo, tabata pia alkadhalika,

Hakika nyie Ni wakala wa mambo yote ya kishetani,
Na ndio mnasababisha tusipate mvua aisee
Umemaliza mjadala.
 
Ndivyo älivyokuambia mchungaji wako?

Wakati wakristo wakipambana na mapepo
Uku Muhammad anasema kila muislamu ana jini kama companion na yeye Muhammad anakiri na yeye analo
Ila jina lake linamfundisha mema

Abdullah ibn Mas’ud reported: The Muhammad, said, “Each one of you has a devil-companion from the jinn over him.” They said, “Even you, O Messenger of Allah?” The Prophet said, “Even me, yet Allah helped me against him until he embraced Islam. He does not order me to do anything but good.”

Source: Ṣaḥīḥ Muslim 2814
 
Anayesema hayo maneno kwenye hizo sentensi ulizozinukuu ni nani ????
Swali halijibiwi kwa swali,toa majibu ya maswali niliyokuuliza acha kurukaruka.Inakuwaje Yesu anakuwa mwana wa Adam?Na kwenye kitabu cha Mathayo wanamweleza kama mwana wa Daudi,mwana wa Abrahimu kwanini wanamwiita hivyo na wakati tunajua alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu?Wewe si unaijua Biblia ,leta majibu acha kuruka?
 
soma vizuri bila jaziba


Hili neno Biblia ni neno la Kigiriki, na maana yake ni "vitabu".

Basi Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi ambavyo ndio vinafanya msingi wa imani ya Kikristo. Inakubaliwa kuwa vitabu hivi vimeandikwa na watu wengi mbali mbali, wajuulikanao na wasiojuulikana.

Lakini hao waandishi wanaaminiwa kuwa walipata ufunuo kutokana na Mwenyezi Mungu, na wameandika walivyoandika chini ya uangalizi na uwongozi wa Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Biblia inaambiwa kuwa ni Neno la Mungu. Biblia ya Wakatoliki, lakini, kidogo inakhitalifiana na ya Waprotestani. Ya Wakatoliki ina vitabu 73, na ya Waprotestani ina vitabu 66.

Kwa jumla Biblia imegawika sehemu mbili kubwa, Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la Kale ni vitabu vyote vilivyoandikwa kabla ya kutokea Yesu Kristo. Vitabu hivi vinaeleza tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, na Adamu na Hawa, historia (taarikh) ya wanaadamu na khasa ya Wana wa Israili, sharia alizopewa Musa na Mwenyezi Mungu, vita vya Mayahudi na jirani zao, mafunzo ya manabii kadhaa wa kadhaa katika Bani Israili yaliyotokana na Mwenyezi Mungu.

Isipokuwa kwa baadhi ya vitabu ambavyo hawavikubali hili liitwalo Agano la Kale, kwa jumla, ndio liliokuwa Biblia na mpaka hivi sasa ndio Biblia ya Mayahudi. Mayahudi hawaikubali kabisa sehemu ya pili iitwayo Agano Jipya inayokubaliwa na Wakristo.

Agano Jipya ni ile sehemu ya Biblia iliyoandikwa baada ya Yesu Kristo. Sehemu hiyo inakusanya Injili nne. Hizi ziitwazo Injili ziliomo katika Biblia ni vitabu vinavyosimulia maisha ya Yesu Kristo na mafunzo yake.

Katika Agano Jipya kipo kitabu kinachoitwa Matendo ya Mitume, kinachoeleza khabari za wanafunzi wake Yesu aliowatuma kwenda tangaza dini. Pia kipo kitabu kinacho itwa "Ufunuo" chenye kueleza mambo ya ajabu ajabu ambayo yasimuliwa kuwa Yohana alifunuliwa akayaona.

Hali kadhaalika zimo barua kadhaa wa kadhaa, nyingi zao ni za Paulo, walizopelekewa watu fulani fulani kuwafunza mambo ya dini. Hizi barua za Paulo, Myahudi aliyetanasari, zinategemewa sana na Wakristo, na ndio msingi wa imani na itikadi zao, hata wengi wapo wanaosema kuwa huu Ukristo tuuonao sasa kwa hakika uliasisiwa na Paulo.

Vitabu viliomo katika Agano la Kale kama vilivyo hivi sasa labda viliandikwa baada ya kurejea Mayahudi kutoka utumwani Babilionia, yaani baada ya mwaka 536 kabla ya Kristo.

Na vitabu vya Agano Jipya vilikusanywa na kukubaliwa na wakuu wa Kanisa katika karne ya nne baada ya Kristo (kiasi 367 A.D.)

Injili nne ziliomo katika Agano Jipya, yaani ya Mathayo, ya Marko, ya Luka na ya Yohana, ndizo zilizoteuliwa na kukubaliwa na wakuu wa Kanisa kutokana na Injili nyingi sana ambazo zimekataliwa.

Neno "Injili" ni neno la Kigiriki, na maana yake ni "Khabari Njema", kwa kuwa Yesu alikuwa akisema kuwa analeta Khabari Njema, yaani Bishara. Vitabu ambavyo vingeweza kuwa ni sehemu ya Biblia, na kwa hakika vikawa vinakubaliwa kwanza na pengine mpaka sasa na baadhi ya madhehebu za Kikristo, vinaitwa "Apokrifa", yaani "vilivyofichwa".
Tell me something I do not know.
 
Nini according , sikiliza clip hii


Kama nilivyosema mwanzo hoja zenu hazina nguvu,kwa hiyo hapo neno "according to " ndiyo limewaletea shida?Mpaka mkakusanya watu uongelee neno according tu?
 
Kama jina lake yeye mwenyewe Yesu halikumsaidia kwenye maombi yake Yesu ya kumuomba babaake alioko mbinguni kumuepusha na kikombe cha umauti kilichokuwa kinamkabili wakati anaenda kusulubiwa, na matokeo yake akasulubiwa na kufa msalabani, iweje jina lake hilo hilo liweze kukufanyia muujiza wewe mmatumbi wa TZ?
Huwezi kujua mpaka utenge muda usome Biblia na ukubali kufundishwa na waliokutangulia otherwise nabaki kuwa sahihi juu yenu,hoja zenu hazina nguvu.Ebu nisaidie kitu nyie huwa mnavaa pete za ndoa?Na kama mnavaa pete za ndoa huwa mnavaa zaidi ya pete moja?Sasa tafuta video za viongozi wako ,kisha uone ile mipete wanavaa utuletee jibu ni ya ndoa au ni ya nini?
 
82% of the words of Jesus are not his:

"The Five Gospels," is a 550 page book containing translations of the Gospels of Matthew, Mark, Luke, and John. It was the result of a six year study by 24 Christian scholars from a number of Western universities.

They decided to produce a translation of the Gospels which would be uncolored by the translator's personal faith. It was decided that this translation was to give the reader an honest picture of what Jesus truly said.

They scanned the text for the words of Jesus, and collect an index of over 1,500 such sayings. They then tested the validity of each of these sayings, one at a time, to see whether Jesus truly said each one.

They then produced a fresh translation, color-coded to show authentic Jesuit sayings and those of an unreliable nature. Their conclusion (page 5) was:

"Eighty-two percent of the words ascribed to Jesus in the gospels were not actually spoken by him."

They go on to reveal that:

"biblical scholars and theologians alike have learned to distinguish the Jesus of history from the Christ of faith. It has been a painful lesson for both the church and scholarship. The distinction between the two figures is the difference between a historical person who lived in a particular time and place...and a figure who has been assigned a mythical role, in which he descends from heaven to rescue humankind and, of course, eventually returns there."

Well then, if 82% of the "words of Jesus" found in the Bible were apparently never spoken by him then where did they come from? Some of the sources demonstrated by the authors are:

"The concept of plagiarism was unknown in the ancient world. Authors freely copied from predecessors without acknowledgment. Sages became the repository of free-floating proverbs and witticisms. For the first Christians, Jesus was a legendary sage: it was proper to attribute the world's wisdom to him. The proverb in Mark 2:17, for example, is attested in secular sources (Plutarch and Diogenes for example)...in the parallel to the Markan passage, Matthew adds a sentence taken from the prophet Hosea (Matt 9:13)."

Also:

"Hard sayings are frequently softened in the process of transmission to adapt them to the conditions of daily living...Variations in difficult saying often betray the struggle of the early Christian community to interpret or adapt sayings to its own situations... Matthew's version of the aphorism "The last will be first and the first last"(Matt 20:16) is softened in Mark 10:31 to "MANY of the first will be last, and of the last MANY will be first"."

And probably most revealing:

"Christian conviction eventually overwhelms Jesus: he is made to confess what Christians had come to believe...The contrast between Christian language or viewpoint and the language or viewpoint of Jesus is a very important clue to the real voice of Jesus, the language of Jesus was distinctive, as was his style and perspective."

The above is only a very small sampling of the very large cache of evidence clearly showing the Bible to have been seriously distorted and altered. To this day it is being continuously edited, corrected, and modified. This is not to say that Christians are not good and honest people in search of the truth. Quite the opposite. Among them are some of the most decent and moral people on this earth. The goal of this book is only to show that the Christian faith as it stands today is not the same one preached by Jesus peace be upon him to his followers nineteen hundred years ago. This is exactly what the Qur'an has been asserting for over fourteen hundred years now
Kuiamini bibilia hutaki ila kumwamini huyo aliyeandika hayo uko tayari?Why?Yanaendana na sumu ulizolishwa.
Mngekuwa mnatafakari mnayoelezwa ma walimu wenu mngekuwa mhamia huku kwani kuna muda huwa wanawalisha matango pori wazi wazi ila kwa kuwa ufahamu wenu umetiwa giza hamuamki.
Siku moja walimu wenu walisema Mtume Paulo aliruhusu uzinzi,hoja wanayoleta "eti Paulo alisema msinyimane ikiwa mmekubaliana".Hapo nilizidi kuchoka,nikawaona hawafai na wanafanya makusudi.Hawaelewi mazingia mabayo Paulo alisem na alikuwa anaongea na watu gani wanachukua neneo na kulitafasiri kwa wanavyotaka wao.
Endelea ila kuna siku utatuelewa hofu yangu usije ukatuelewa ukawa umechelewa.
 
Lingekua linaponya wangeenda hospital wakawaponye wagonjwa na siyo kusubiri sadaka kanisan.
Usanii mwingi hiyo ni biashara
Huo ni utoto ulio nao siku ukikua na kujua Mungu anavyotenda kazi utaacha tabia za utoto.Kwa Mungu kilicho cha muhimu ni uponyaji wa Roho kwanza na wala siyo mwili.Yesu akasema itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu wote na kuipoteza nafsi yake?
Kama ulikuwa hujui kabla Mungu hajamponya mtu huuchunguza moyo wake kujua je huyu mtu ananihitaji mimi niwe Mungu wake au anataka uponyaji tu?Kama Mungu ndiye anayeponya hapangiwi nani amponye,yeye anaamua.
Utoto wa kumjua Mungu kama ulio nao umewapeleka wengi kwenye mtego wa shetani kwa kutaka uponyaji bila kujali uponyaji huo au kutatuliwa kwa matatizo yao ni nguvu ya Mungu imetenda au ni nguvu za giza kupitia watumishi feki waliojaa katika nyakati hizi.
Kasome Biblia ,tatizo hamjui na hamtaki tuwafundishe,mtume Paulo aliponya wengi lakini ilikuja akaugua na Mungu hakumponya akmwambia Neema yangu yakutosha.Je ni lazima kila mgonjwa aponywe?Kasome,kuna wagonjwa wengine waliponywa kwa imani zao,kuna wengine waliponywa kwa kufanya walichoagizwa wakafanye,njia za Mungu hazichunguziki.Mnatuchosha ,mko chekechea mnauliza maswali ya advanced level na tukiwa pa majibu ni wabishi.Tutawasaidiaje?Subilini siku nafsi ikitengana na mwili,mtayakumbuka haya tunayowaeleza.
 
. Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili?

Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika:
Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
1 Wakorintho 15.15


Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja hapa anasema:

"Tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo."

Ikiwa Mungu kamfufua Kristo, hawawezi kuwa wote wawili hao ni mtu mmoja.

Mmoja alikuwa ni mtenda, mfufuaji, na wa pili alikuwa ni mtendwa, mfufuliwa. Kama Kristo ni Mungu mwenye uwezo wa kufufua basi maelekeo ni kusema: "Kristo kajifufua", sio kafufuliwa. Mwenye kufufuliwa ni mfu asiyejiweza kitu.

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume inasimuliwa kuwa Mt Stefano alisema aliyoyaona yaliyo mbinguni. Alisema:

Tazama! naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
Matendo 7.56

Mwana wa Adamu ndiye Yesu, na kwa jina hilo ndio mwenyewe akipenda kujiita, sio Mwana wa Mungu. Hapo basi huko mbinguni Stefano anasema anamwona Yesu kakaa mkono wa kulia wa Mungu. Mwenye kukaa mkono wa kulia wa fulani hawezi kuwa ndiye yule yule fulani. Hayo ni maelezo ya mbinguni. Ni wazi basi kwa ushahidi wa Biblia kuwa Yesu hakuwa Mungu mbinguni kama alivyokuwa si Mungu duniani.

Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:

Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Luka 22.42-43

Hapa tunaona mambo matatu muhimu:

Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu.

Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.

Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: "uniondolee kikombe hiki" cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.

Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu."

Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:
Baba ni mkuu kuliko mimi.
Yohana 14.28

Na mwishoni naye yupo mslabani:
Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
Mathayo 27.46

Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema:

"Mungu wangu naye ni Mungu wenu"? Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake.

La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo. Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.

Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu.
Ninaanzisha uzi wenye majibu
 
Hebu tuiache Biblia itueleze:

Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akisema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana, unisaidie. akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani za bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
Mathayo 15.21-28

Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina.

Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu: Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."

Ikiwa ipo shaka yo yote katika akili ya mtu kuwa maana ya maneno hayo ni kuwa Yesu anasema kuwa hakutumwa kwa kabila nyengine zo zote ila Waisiraili tu na atazame mwenye shaka tafsiri kubwa kabisa ya Wakristo inayoeleza maana wazi maneno ya Biblia

, The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi: "Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Mathayo 7.6

Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili. Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi. Hayo ndiyo mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani mwa Yesu. Kama asemavyo Isaac Asimov katika kitabu chake Guide to the Bible (Uwongozi kwa Biblia):

"Suala liliopo ni nani hao mbwa na nguruwe wnaokusudiwa katika mstari huu?

Yaweza kuwa maana ya mstari huu ni kuwa haifai kufunza ukweli wa dini kwa wale wasiotubu katika kejeli zao, au wale waliozama katika madhambi, lakini hayo hayaelekei kabisa.

Basi mtu amfundishe nani? Wale waliokwisha amini? Yesu mwenyewe anakanya hayo, kwani aliposhutumiwa kuwa anachanganyika na wenye dhambi ananukuliwa kusema:
Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.

Mathayo 9.12

"Upande mwengine, huku kutaja mbwa na nguruwe huweza kuwa ni maneno aliyoyachagua Mathayo kulipa nguvu wazo lake kuwa isifanywe juhudi kubwa kueneza mafunzo ya Yesu miongoni mwa Mataifa mengine.

Labda ni nadhari ya Mathayo kuwa ipo khatari kubwa ya hayo Mataifa kuudhika na juhudi za kutaka kuwatanasarisha na kwa hivyo wakawatesa Wakristo; itakuwa ndio 'watageuka na kuwararua'

.Na hayo kwa hakika waliwahi kuyafanya. Yaweza kuwa aliona kuwa yale Mataifa yaliyoukubali Ukristo bila ya kuijua Sharia ya Musa yangeweza kuyavuruga mafunzo ya Yesu: 'na kuyakanyaga chini ya miguu yao.'"

Na juu ya kauli ya Yesu : "Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa," Asimov anasema:

"Hapa Mathayo kwa uwazi anatuletea Yesu ambaye kazi yake ni ndani ya mipaka ya uwananchi wa Kiyahudi tu."
Unazidi kuprove nilichokisema juu yenu wapotoshaji wakubwa,mnatafuta maandiko mnayageuza mnavyotaka.Haya umesema Yesu alikuja kwa ajiliya ya wayahudi tu na hivyo ukristo haufai kufundishwa kwa watu wengine,wewe au huyo mwandishi wako una conclude haya ndiyo mawazo ya Yesu.Mtazamo wako au wa mwandishi unalazimisha yawe yalikuwa mawazo ya Yesu.Kwa hiyo Yesu baadaye alijipinga alivyowaambia wanafunzi wake" enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili kwa watu wote?Hapo alisema kwa wayahudi peke yake?
Vipi Yohana 3:16?Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila mtu amwaminie asipotee...(Hapo aliposema Kila mtu amwaminie inamaanisha Wayahudi peke yao?).Kama nilivyokuambia mimi technique zenu nazijua,maandiko haya mnayajua ila mnajua yatawaaibisha lakini mnaendelea kupoteza watu ambao mnajua hawayajui maandiko na hao mmewapata.Mngekuwa mko fair mlitakiwa mjifunze na mngegundua ya kwamba mna mambo mengi ya kujifunza.
Unapojenga hoja katika biblia ni muhimu kuwa na mstari na ikiwezekana mistari mingi kutetea hoja yako.Labda nikusaidie kitu,mpango wa Mungu mwanzoni ilikuwa ni kulifikia taifa la Israel kisha taifa la Israel litumike kueneza habari njema duniani.Lakini walipomkataa Yesu,kazi hiyo walipewa baadhi yao walioamnini na wenhgine ambao hata hawakuwa Wayahudi.
Chakula cha watoto kuwapa mbwa ni msemo wa kutoa kitu cha thamani kwa mtu asiyekitambua thamani yaKe.
Kwa mfano hapa kuna muda natoa chakula cha watoto nawapa mbwa na nguruwe hapa ila hawajui thamani yake ndiyo sababu wanarudi na maswali yasiyo na hoja za msingi na hawako tayari kujifunza bali kufanya ubishi.
Kama unatakakujifunza na kuacha ushabiki tafuta kuna biblia ya King James Version ni ya Kiingereza maneno aliyoyasema Yesu wameyaandika kwa rangi nyekundu kutofautisha na mengine.Hapo utajua kipi kilitoka kinywani mwa Uesu na kipi walielezea wanafunzi wake.
Sielewi shida yenu ni nini wanafunzi wa Yesu wakiandika yale Yesu aliyoyatenda au kusema,naamini wewe unaweza ukawaelezea wazazi wako kwa kuwa umeishi nao inakuwa ngumu kwenu kuamini kile walichoandika wanafunzi wa Yesu kumhusu Yesu na wakati walikuwa naye wakifanya naye huduma huku na kule?
Mko tayari kuamini wanachoandika wapotoshaji ambao hata hawakuwepo na Yesu hicho mnakiamini,hii ni nini?
Hoja zenu hazina support ushahidi mwingine wa Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote utaupata kwenye kitabu cha ufunuo?Labda nikupe shule itakusaidia siku moja ukimpokea Yesu,ufunuo unaweza ukawa wa mambo yaliyopita au mambo yajayo.Sasa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana(hata hapa huwa mnamaswali yasiyio na msingi) haya niseme ni Ufuno wa Yesu aliompa Yohana ndiyo huwa mnapenda tuseme hivyo.

Ufunuo 21​

1.Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu(siyo na Wayahudi peke yao), naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao
Yohana 3:17-19
17.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe (Siyo Wayahudi imesema ulimwengu)katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni(Yesu amekuja ulimwenguni), na watu(siyo Wayahudi imesema watu) wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Kwa hiyo ukizingatia hayo maandiko hapo juu Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote,shida unachukua mstari mmoja unafanya conclusion bila kuangali amziungira au maneno hayo alikuwa anasema na nani na katika mazingira gani.Hapo tu mnapotea na tukiwaita mrudi hamtaki,taratibu tutaelewana.
 
Back
Top Bottom