Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Kazi imeisha ndiyo njia gani hiyo aliyoileta Yesu ?
Yesu alileta ukombozi wa mwanadamu dhidi ya dhambi akiwa kama ndie njia ya ukweli na uzima yeyeto ajae kwake anao uzima wa milele.
 
Ndivyo älivyokuambia mchungaji wako?
Ishu sio mchungaji kwa mujibu wa maandiko na elimu ya jumla katika ulimwengu usioonekana.
Hata waliokuwa level ya mwisho ya uchawi wakiwemo wenye phd ya uchawi wanathibitisha hilo.
 
Ishu sio mchungaji kwa mujibu wa maandiko na elimu ya jumla katika ulimwengu usioonekana.
Hata waliokuwa level ya mwisho ya uchawi wakiwemo wenye phd ya uchawi wanathibitisha hilo.

Hebu tuiache Biblia itueleze:

Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akisema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana, unisaidie. akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani za bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
Mathayo 15.21-28

Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina.

Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu: Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."

Ikiwa ipo shaka yo yote katika akili ya mtu kuwa maana ya maneno hayo ni kuwa Yesu anasema kuwa hakutumwa kwa kabila nyengine zo zote ila Waisiraili tu na atazame mwenye shaka tafsiri kubwa kabisa ya Wakristo inayoeleza maana wazi maneno ya Biblia

, The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi: "Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Mathayo 7.6

Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili. Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi. Hayo ndiyo mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani mwa Yesu. Kama asemavyo Isaac Asimov katika kitabu chake Guide to the Bible (Uwongozi kwa Biblia):

"Suala liliopo ni nani hao mbwa na nguruwe wnaokusudiwa katika mstari huu?

Yaweza kuwa maana ya mstari huu ni kuwa haifai kufunza ukweli wa dini kwa wale wasiotubu katika kejeli zao, au wale waliozama katika madhambi, lakini hayo hayaelekei kabisa.

Basi mtu amfundishe nani? Wale waliokwisha amini? Yesu mwenyewe anakanya hayo, kwani aliposhutumiwa kuwa anachanganyika na wenye dhambi ananukuliwa kusema:
Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.

Mathayo 9.12

"Upande mwengine, huku kutaja mbwa na nguruwe huweza kuwa ni maneno aliyoyachagua Mathayo kulipa nguvu wazo lake kuwa isifanywe juhudi kubwa kueneza mafunzo ya Yesu miongoni mwa Mataifa mengine.

Labda ni nadhari ya Mathayo kuwa ipo khatari kubwa ya hayo Mataifa kuudhika na juhudi za kutaka kuwatanasarisha na kwa hivyo wakawatesa Wakristo; itakuwa ndio 'watageuka na kuwararua'

.Na hayo kwa hakika waliwahi kuyafanya. Yaweza kuwa aliona kuwa yale Mataifa yaliyoukubali Ukristo bila ya kuijua Sharia ya Musa yangeweza kuyavuruga mafunzo ya Yesu: 'na kuyakanyaga chini ya miguu yao.'"

Na juu ya kauli ya Yesu : "Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa," Asimov anasema:

"Hapa Mathayo kwa uwazi anatuletea Yesu ambaye kazi yake ni ndani ya mipaka ya uwananchi wa Kiyahudi tu."
 
Yohana 14.6-30,Matendo ya mitume 4.12
Yohana 3.18,
kwa uchache tu hizi.

Hakuna Aya hata moja katika hizo Aya inayosema maneno haya uliyoyaandika, nakunukuu hapa chini

Yesu alileta ukombozi wa mwanadamu dhidi ya dhambi akiwa kama ndie njia ya ukweli na uzima yeyeto ajae kwake anao uzima wa milele.
 
Kuna dini ina uhusiano wa karibu na mapepo na mashetani, wao ni wapinga Kristo, watapinga kila kitu, watasema Yesu hajawahi kuponya wala kutoa pepo, ili tu aonekane sana na yule karani wa mama mfanyabiashara ambaye alioa katoto ka miaka tisa
Wewe jamaa Ni mpumbavu aliyekubuhu...kushinda shetani mkuu kilaza wewe.......
 
Hili ni swali tu katika kujua uweza na uwezo wa nguvu za Jina la Yesu katika kutenda miujiza.

Yesu alipata kuishi yapata miaka 2019 iliyopita. Je inakuwaje jina lake leo lisemwe kwamba lina nguvu sana katika kutenda miujiza?

Kuna manabii wengi sana na mitume wengi wamepita, kina Krishna, Elisha , Elizabeth Mtishbi nk mbona hatusikii visa vya majina yao katika kutenda miujiza? Sanasana Wlisha ametajwa mara moja kwamba jamaaa walibeba maiti wakienda kuzika, walipofika katika kaburi la Elisha ikatokea vita, katika kujinusuru wakaibwaga maiti chini, maiti ikaangukia kaburi la Elisha, maiti ikafufuka, ikatoka nduki kichizi.

Ndugu mnaoelezea uweza wa jina la Yesu njooni hapa mshuhudie
Elizabeth Mtishbi??? Au ulimaannisha Eliya?
 
Kuthibitisha kama ni uongo au ukweli ni hadi uingie kwenye ulimwengu wa roho sio wa nyama
Imani hiyo ndiyo inayowatajirisha Wachungaji, We Mungu amekupa akili, kuweza kutambua mambo, leo eti kujua uwongo wa mchungaji, mpaka kiroho.

Kibwetele alikua na kila sababu za kuwaunguza moto wale jamaa.
 
Sikatai kwenye original na feki wapo.
Wapo wachungaji wa Mungu na wachungaji wa shetani pia,kuwapima ni hadi uyajue maandiko.
 
Majini viumbe vilivyomuasi Mwenyezi Mungu.Majini roho ni viumbe katika ulimwengu wa roho.
Ni vitendea Kazi vya shetani,utumika na wachawi na waganga wa kienyeji.
Bado sijakuelewa unavyosema tu majini ni viumbe vilivyomuasi Mwenyezi Mungu unakuwa bado haujaeleza hivyo viumbe ni viumbe gani, kwa maana hata Malaika mnasema wapo waliyomuasi Mungu na malaika wana sifa zao wanafahamika ila sasa hao majini ndio viumbe gani?
 
Rudia kusoma kwa utulivu utaelewa.
 
Rudia kusoma kwa utulivu utaelewa.
Haujaweka wazi hao viumbe ndio malaika au ni aina nyengine ya viumbe? Kumbuka nilisema kwamba majini sifa zao hufanana na binadamu tofauti na malaika.
 
Haujaweka wazi hao viumbe ndio malaika au ni aina nyengine ya viumbe? Kumbuka nilisema kwamba majini sifa zao hufanana na binadamu tofauti na malaika.
Labda lete ufafanuzi tuelimike tunatofautiana elimu
 
Labda lete ufafanuzi tuelimike tunatofautiana elimu
Ufafanuzi ni kwamba malaika majini na binaadamu, hivyo ni viumbe aina tatu tofauti. Sasa tatizo linakuja pale inaposemwa kwamba majini ni malaika(waliyoasi) wakati sifa za viumbe majini ni tofauti na malaika.

Hivi viumbe majini tuvijuavyo ni kwamba wanakula, wanajamiana na kuzaa. Sasa sidhani kama malaika wana sifa hizo?
 
Hili ni swali tu katika kujua uweza na uwezo wa nguvu za Jina la Yesu katika kutenda miujiza.

Yesu alipata kuishi yapata miaka 2019 iliyopita. Je inakuwaje jina lake leo lisemwe kwamba lina nguvu sana katika kutenda miujiza?

Kuna manabii wengi sana na mitume wengi wamepita, kina Krishna, Elisha , Elizabeth Mtishbi nk mbona hatusikii visa vya majina yao katika kutenda miujiza? Sanasana Wlisha ametajwa mara moja kwamba jamaaa walibeba maiti wakienda kuzika, walipofika katika kaburi la Elisha ikatokea vita, katika kujinusuru wakaibwaga maiti chini, maiti ikaangukia kaburi la Elisha, maiti ikafufuka, ikatoka nduki kichizi.

Ndugu mnaoelezea uweza wa jina la Yesu njooni hapa mshuhudie
Mambo ya dini tuwaachie wenyewe
 
Back
Top Bottom