Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Mkuu ni imani tu, si kweli kama Yesu anaponya.
 

Kwa mujibu wa Wakristo wengi, Yesu amekuwa ni Mungu-mtu, mtu kamili na Mungu kamili. Je, kitu chenye mwisho na kile kisicho na mwisho vinaweza kuwa ni kimoja? Kuwa “Mungu kamili” maana yake ni kutokuwa na mwisho na kutohitajia msaada, na kuwa “mtu kamili” maana yake ni kutokuwa na uungu.

Kuwa mtoto ni kuwa chini ya daraja ya uungu na kuwa na uungu ni kutokuwa mtoto wa yoyote. Vipi Yesu atakuwa na sifa ya utoto na uungu kwa wakati mmoja?

Wakristo mnadai kwamba Yesu alidai kuwa yeye ni Mungu wakati ulipomnukuu katika Yohana 14:9: “…Aliyeniona mimi amemwona Baba…”

Swali :

Je, Yesu hakusema wazi wazi kwamba: kamwe watu hawakumuuona Mungu, kama inavyosema Yohana 5:37:

“Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona”?
 

YESU SI MUNGU:


KWA SABABU MUNGU YUPO NDANI NA PAMOJA NA WENGINE PIA


Baadhi ya Wakristo wanadhani kwamba Yesu ni Mungu kwa sababu ya baadhi ya maandiko ya Biblia yanayosema kwamba Yesu yupo pamoja na Mungu, bali Mungu yupo ndani ya Yesu na Yesu yupo ndani ya Mungu.

Maandishi ya aina hii yote hayamaanishi kwamba Yesu ni Mungu bali yanaonesha kwamba Mungu na Yesu ni tofauti tofauti wala siyo kitu kimoja.

Vile vile Biblia haisemi kwamba mtu ambaye anatajwa kuwa ndani ya Mungu au Mungu yumo ndani yake ni mungu.

Kinyume chake Biblia inatutajia watu kadhaa wale ambao wako pamoja na Mungu na Mungu yupo ndani yao na hawa wapo ndani ya Mungu.

Tena hakuna Mchungaji yeyote ambaye anawaita watu hawa miungu.

Wakati watu wengine kwa sifa zile zile hawaitwi miungu, kwa msingi na kwa uzuri gani, Yesu aitwe Mungu? Biblia inasema kwamba:

1. “Wote wawe na umoja, kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; Hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujuwe ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. (Yohana 17:21-23).

2. Mungu mmoja, naye ni baba wa wote aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. (Waefeso 4:6)

3. Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya baba yangu, nanyi ndani yangu, mimi ndani yenu. (Yohana 14:20).

4. Nabii Suleimani anasema kwamba: Mimi nilikuwepo pamoja na Mungu hata kabla ya kuumbwa ardhi na mbingu, (Mithali 8:22-30).

5. ....Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawambie, ninapaa kwenda kwa baba yangu naye ni baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. (Yohana 20:17).

6. Kama Wakristo waseme kwamba Yesu ni mungu kwa sababu alizaliwa bila baba. Najibu kwamba aya gani inasema kuwa azaliwaye bila baba ni Mungu? Na malaki ya wadudu wanaozaliwa bila baba watakuwa na uhusiano gani na Bwana Yesu?

Katika Biblia mfano mzuri zaidi kuliko Yesu unapatikana kwamba: Melkizedeki mfalme wa Salem hana wazazi, hana mwanzo na mwisho, (Waebrania 7:3). Sasa kama Yesu anaitwa mungu kwa sababu ya kuzaliwa bila baba, Melkezedeki atakuwa mungu mkuu kwa sababu hana wazazi, hana mwanzo hana mwisho.

Wakristo wanasemaje hapa?
 

YESU SI MUNGU


Exodus 33:20


But He said, “You cannot see My face, for no man can see Me and live!”


John 1:18


No one has seen God at any time;


1 John 4:12


No one has seen God at any time; if we love one another, God abides in us, and His love is perfected in us


John 5:37


And the Father who sent Me, He has testified of Me. You have neither heard His voice at any time nor seen His form.


1 Timothy 6:16

who alone possesses immortality and dwells in unapproachable light, whom no man has seen or can see. To Him be honor and eternal dominion! Amen.
 


Neno KRISTO linatokana na neno Messiah la Kiebrania.

Kwa Kiarabu ni Masih.

Shina la neno ni m-a-s-a-h-a, maana yake ni kuchuwa, kusinga, kupaka.

Makuhani na wafalme walisingwa (walipakwa mafuta) kabla ya kusimikwa katika katika nyadhifa zao. Lakini kwa haiba yake ya tafsiri ya Kigiriki, neno hili linaonekana kuwa mahususi, likiswihi kwa Yesu tu.

Mkristo ana mazoweya ya kubadilisha metali kuwa dhahabu ing’arayo. Walichoweza kukifanya ni kuyabadili kabisa maneno katika lugha yake kama vile “Cephus” kuwa Peter, “Messiah” kuwa Christ.

Anawezaje kufanya hivyo? Rahisi sana. Neno MASSIAH la Kiebrania, kwa Kiingereza, maana yake ni Anointed (aliyepakwa, aliyetiwa au aliyesingwa mafuta). Neno la Kigiriki la kutafsiri neno hilo ni “christos”.

Inyofowe ‘os’ katika neno christos, hapo unabakiwa na christ. Sasa geuza “c” ndogo kuwa “C” kubwa, yebo! Hapo sasa keshaunda jina jingine!
Christos maana yake ni ALIYETIWA (ALIYEPAKWA) MAFUTA, na mpakwa mafuta, kwa maana yake ya kidini ni MTEULE (ALIYETEULIWA). Yesu (as), baada ya ubatizo wake kwa Yohana, aliteuliwa kuwa nabii wa Mungu. Kila nabii wa Mungu huteuliwa hivyo (anointed or appointed).

Biblia imejaa “wapakwa mafuta” kibao. Yaani kwa lugha asiliya ya Kiebrania-waliofanywa kuwa “messiah”.

Hebu tubakiye na tafsiri hiyo ya Kiingereza- “anointed.”

Siyo tu manabii makuhani na wafalme waliotiwa mafuta (christos-ed- waliofanywa kristo) bali pembe, kerubi na nguzo nazo piya zilitiwa mafuta (zilifanywa kristo)

Kama Kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi... (mambo ya walawi 4:3)

Kisha Musa akatwaa hayo mafuta matakatifu ya kutia, akatia mafuta maskani, na vyote vilivyokuwamo, na kuvitakasa...(mambo ya walawi 8:10)

Bwana.... Na kuitukuza pembe ya masihi wake (1Samweli 2:10)

Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake...(Isaya 45:1)

Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta.... (Ezekieli 28:14)

Kuna zaidi ya mifano mia kama hiyo katika Biblia. Kila ukutanapo na neno anointed katika lugha ya Kiingereza (iliyotumika kutafsiri Biblia kwa Kiswahili), uchukuliye kuwa neno hilo ni christos kwa tafsiri ya Kigiriki.

Na ukilichukuwa neno christ ambalo wakristo wameliunda, utakuwa na Christ Cherub (Kerubi Kristo), Christ Cyrus (Koreshi Kristo), Christ Priest (Kuhani Kristo), Christ Pillar (Nguzo Kristo) n.k.
 
mimi sio mtu wa kanisa wala kuzingatia mambo ya dini ila nakumbuka ijumaa kuu ya mwaka 2019 usiku wa saa sita nilipata ajari ya gari liligongwa na lori la mchanga, gari ilipigwa ikawa inabilingika yani pombe yote ilikata ghafla ninachokumbuka nilimwambia Mungu inamaana umekubari leo nife kweli? ni kama nilikua naongea na mtu na gari ilisimama hapohapo na nikatoka na majeraha kidogo sana mashuhuda wa ajari hawakuamini kama nimepona, kifupi jina la Yesu/Mungu kweli linaponya, bado sijaokoka ila naamini uweza wake.
 
Reactions: _ly

Kama nilivyosema mwanzo w a l e j a m a a (Yahaya mpe MIC) wamewapoteza sana,na inaonekana mna program maalum yakufanya upotoshaji.Nimegundua uwezo wenu sasa naomba uniruhusu nikufundishe kama mtoto wa darasa la kwanza,nimeona jinsi ninavyokuelezea huelewi una lengo lako,najua kabisa unajua unachokifanya na unawajua na ndugu zako mnaoshirikiana nao kuweka sumu,ndiyo sababu,huna vitu vyako wewe kama wewe,mambo mengi unayoyaandika tukiyatafuta tunayakuta mitandaoni yanafanana.Hii inaonyesha umekalilishwa au umepewa maswali fulani ndiyo sababu hutoki na haujibu maswali yangu ila unaendelea kuleta maswali yako.Unashindwa kujibu maswali yangu kwa sababu haya ninayoukuuliza huna desa.

Sasa nirudi nikufundishe kwa technique nyingine kama hii nayo hautailewe basi tutaendelea kukuombea

Mfano wa kwanza:Wewe ni mfanya kazi, mnafanya kazi ya kusambaza mboga mikoa ya Tanzania,boss anatoa maelekezo mwezi huu wa nne,tutapeleka mboga Arusha peke yake ,msipeleke maeneo mengine.Sawa ?Sawa boss.Maagizo haya yanarekodiwa kwenye vitabu ya kwamba boss alisema tutapeleka mboga Arusha peke yake.
Mnafanya kazi ya kupelaka mboga Arusha,baadaye siku za mbele boss anawaagiza pelekeni mboga miko yote ya Tanzania.Taarifa hii pia inarekodiwa ya kwamba boss aliagiza tupeleke mboga Tanzania yote.
Hapa shida yenu kwa kuwa boss alisema mwanzoni tutapeleka Arusha tu,mnapinga maagizo yake ya kuepeleka mikoa mingine.Pia hamtaki kukubali kwamba katika kujifunza kuna formal way na informal.Hamuwaamini wanafunzi wa Yesu ya kwamba walichokiandika ni kweli Yesu alisema?Kwa lugha zingine mimi leo nije nikubishia wewe juu ya somo mlilofundishwa Ijumma iliyopita pale ulipoenda kuswali.Nikatae ya kwamba mlichofundishwa siyo hicho,yaani mtu amabaye hakuwepo anabisha na na watu waliokuwepo?Huyu mtu akili yake iko sawa?
Biblia huwa haijipingi isipokuwa sisi ndiyo tunashindwa kuelewa ,sasa ukisema Paulo ameleta mafundisho mapya?
Nokusaidie katika ukristo wa kweli hatufanynhudumamkwa akili zeti wenyewe yupo anayetuonhgoza katika huduma hiyo.Paulo alichaguliwa na Mungu kwa kazi maalum,kwa hiyo hakuna sehemu alienda kufanya kazi kwa matakwa yake mwenyewe.

Mfano wa pili:Baba yako ametoa maelekezo kwamba nataka mfanye usafi wa ndani ya nyumba tu ndicho nilichopanga,sawa?Sawa baba.Alichokisema kikaandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu.Baada ya mwezi anawaagiza enendeni mtaani,mpite kila nyumba mfanye usafi nje ya nyumba hizo.Hili agizo la pili linachelewa kutekelezwa,linakuja kufanyiwa kazi baadaye.Je ni sahihi mtu akikubishia akakuambia wewe Baba alisema tufanye usafi nyumbani kwetu na siyo kwingine?Mtu huyu anyebisha pasipo kuwa na hoja za msingi ni wewe na hao ndugu zako.Hoja zenu ni dhaifu sana hazina ushadhidi zaidi ya kutumia technique za ujanjaujanja kuwachanganya watu,kisha unawafanya waone unachosema wewe ni sahihi.

Soma Matendo 13:2
"Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu aliwaambia, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi maalumu niliyowaitia.”
Sasa Mungu mwenyewe anasema atengewe Sauli(Paulo) amemwita kwa kazi maalum,wewe huna hata umri wa miaka 120 unabisha kwa sababu ya document na vitabu vilivyojaa mawazo ya wanadamu vinavyopotosha kweli?
Mathayo 28:19 Yesu anawaagiza waende wakawafundishe mataifa wote...Wewe na wenzako mnataka wabaki na maelekezo ya mwanzo ya kufanya kazi kwa Wayahudi?Unachokifanya ni kama mfanyakazi anakataa maagizo mapya anayopewa na boss wake na kung'ang'ania alichoambiwa jana?Samahani umeajiliwa au umejiajili?Nisije niaka naongea na kukupa mifano ambayo ni giza kwako?Amacho hamjuini kwamba Yesu alikuwa na kazi anaifanya hivyo alikuwa anatoa maelekezo,leo atatoa maelekezo haya na kesho mengine ili lengo la kuja kwake litimie.Sasa kitendo chenu cha kung'ang'ania tu amelekezo fulani ili mtimize agenda yenu ya siri hatuwezi kunyamaza,taratibu watu wataujua ukweli na nitaendelea kuweka wazi technique zenu mpaka ndugu zako watampokea Yesu awe Bwana na mwokozi wao.
Kitu kingine nikusaidia ukawaambie na jamaa zako wale wanafunzi hawakujiita wao Wakristo bali waliitwa kwa mara ya kwanza kwenye mji unaitwa Antiokia(uko Uturuki ya sasa) kwa hiyo jamaa walipeleka injili mpaka Turkey wewe unasema kwa Wayahudi peke yao?Unapingana na Biblia na unapingana na historia.Hivi na Damscas ni Isarel?Jamaa walifika huko,tatizo humjui Mungu wetu na jinsi anavyofanya kazi.Kama ingekuwa siyo mapango wake injili iende kwa watu wengine angewazuia.Na kama ulikuwa hujui hata hayo makanisa 7 ya kwenye ufunuo yako Uturuki ,sasa mnapojadili muwe na hoja zenye nguvu.

,kama ambavyo mnang'ang'ani tuwape ushahidi wa wapi Yesu alijiita mwenyewe mwana wa Mungu?Mmekuwa kama mmejitoa ufahamu,unajua watu wana majina ,mara nyingi mtu anaitwa jina lake na watu wengine mara chache anajiita mwenyewe.
Biblia ni kitabu kizuri ,naamini unajua maana ya a.k.a (inawezekana hujui,nikifupi cha "also known as") ingekuwa leo yamkini Yesu angeiwa Mwana wa Mungu ak.a Mwana wa Adam.ak.a Mwana wa Daudi, kumbe kwa lugha nyingine a.k.a ilianza siku nyingi Sauli a.ka. Paulo.Sasa nyie shida yenu siielewi inaonekana kuna kitu mnataka mkifikie lakini ni kuambie hamtaweza kwa sababu Mungu wa Israel ni mkuu.Kama ambavyo taifa la Israel limeendelea kuwepo( pamoja na Iran kusem ni uvimbee ambao unaweza ukatumbuka muda wowote )ili uwe ushahidi wa habari zake zilizojaa kwenye biblia pamoja na chuki za mataifa wanayomzunguka ingawa siku hizi wamegundua wanaanza kushirikiana naye ,wewe tu bado umekomaa na madesa yako.
Je Yesu ni kigeugeu?Yesu siyo ,hajawahi na hatawahi ,shida ni nyie mnaolazimisha mambo yawe mnavyotaka nyie kwa makusudi yenu ambayo hamuwezi kuyaweka hadhalani,lakini najua unayajua au unatumiwa ila huyajui .
Nikuulize kitu,wewe unaamini nini katika Biblia ?Kipi kiko sahihi ambacho kiko ndani ya Biblia?
Naomba pia urudi shule ujifunze nini maana ya "passive na active speech" inaonekana katika Biblia hamtaki kutambua "passive speech".Ila mnaposoma magazeti yanaandika "mwanzo wa kunukuuu..." mwisho wa kunuuu" au mkiangalia TV mtangazaji akisema "namnukuu" hayo mnayakubali ila ya Kwenye biblia yamepotoshwa.Waandishi wakiandika Rais alisema "......." Mnakubali ila Biblia ikiandika "Yesu alisema..."Mnakataa.Kazi kwelikweli

Kuna maswali niliuliza usidhani nimesaahau nahitaji jibu,
1.Je huwa mnavaa pete za ndoa?Na kama huwa mnavaa,mnavaa zaidi ya pete moja?Kama huwa hamvai zile pete wanavaa wakubwa wenu zinakazi gani?
2.Ulisema Yesu siyo mwana wa Mungu yeye mwenyewe alijiita mwana wa Adam,nilikuuliza Yesu anakuwaje ni mwana wa Adam wakati tunajua alizaliwa na bikra Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu?Naamini mnaijua Biblia vizuri kuliko sisi ndiyo sababu nataka jibu kutoka kwako mwananzuoni.lakini pia pita Mathayo moja,juu ya ukooo wa Yesu ameitwa tena Yesu mwana wa Daudi,mwana wa Abraham,tusaidie majibu mwananzuoni wetu ila usikimbie,taratibu tutaelewana.
 
Only sometimes it is better to be quite than to speak or write cause by talking or writing we give information about us.
 
Yesu yupi mzungu au yule mweusi ?
Mkuu utajishusha status yako kuna ndugu zako wanakutegemea hapa kwa majibu yako na maswali yako,na hapa pia huwa mnakosea "kujifanya hamjui na kuuliza maswali yasiyo na msingi".Naamini unasoma biblia otherwise hausomi Biblia ila una access na website/Vitabu za jamaa zako walioweka maswali yenye utata au ya kuwauliza wakristo.kwa hiyo naamini unajua sura halisi ya Yesu Kristo haijulikani.Hayo mambo ya Yesu mweupe au mweusi ni for educational purpose lakini sura halisi ya Yesu haijulikani.Sanasana kama unaitaka sura yake kama alivyoonyeshwa Yohana utaipata kwenye ufunuo lakini hiyo ni sura akiwa mbinguni siyo duniani.Unashindwaje kuyajua haya masomo ya elementary katika ukristo?
 
Una mikwala ,unaleta maneno ya Kigiriki,sijui kilatinji ili watu wadhani uko deep kumbe unachukua sehemu unapaste kama yalivyo hata "font" na "style" zinaonekana hujazibadilisha umechukua sehemu umeleta zigo kama lilivyo.Kuna muda unaleta tu vitu haviendani kabisa na kinachojadiliwa.Vipi unataka tujadili mafuta au?🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hoja1:Wewe kutokuwa na Biblia original au kutokujua ipi ni original hakufanyi isiwepo,nyie ndiyo huwa mnatabia za kuseama pesa hazipo?Usiseme pesa hazipo sema sina pesa kwa nini unajumuisha na wengine?

Hoja2:Umesema hakuna uthibitisho ya kwamba wanafunzi wa Yesu waliandika injili?Wewe tupe uthibitisho ya kwamba hawakuandik injili?Kuna tofauti ya kutokuwepo na uthitisho na uthibitisho kuwepo ila mtu anaamua kuukataa.Nyie mmeamua wenyewe kukataa uthibitisho.
Hoja 3:Umeandika Luka hakuwa mwanafunzi wa Yesu?(Hapa umeonyesha hujui kabisa sasa tulia upate shule)Kujua hamjui darasani hamtaki kuja?Tunawasaidiaje?Unatakaniedelee kutoa chakula cha watoto niwape mbwa?

Je mwanafunzi ni nani?Je Yesu alikuwa na wanafunzi wangapi?Je mitume wa Yesu na wanafunzi wa Yesu maneno haya yanamanisha kitu kimoja au tofauti?Au moja limebeba jingine?
Definition
Desciple:
one who accepts and assists in spreading the doctrines of another
Apostle: one sent on a mission:
Yesu alikuwa na wanafunzi wengi,kati ya hao wanafunzi wengi aliwaita akachagua mitume(apostles) kumi na mbili.Kwa hiyo Luka(Dr.Luka) alikuwa ni mwanafunzi wa Yesu,angali maana ya neno Desciple hapo juu,Luka alikuwa pamoja na Yesu alijifunza kutoka kwake na alishiriki kwenda kueneza injili.Kwa hiyo kusema Luka hakuwa mwanfunzi wa Yesu nashukuru umejionyesha kiasi gani hujui tofauti ya Disciples and Apostles na hujui kama kulikuwa kuna makundi katika hao wanafunzi wa Yesu.Yesu alikuwa na wanfunzi wengi lakini siyo wote waliandikwa majina yao ili wewe ujifunze.Lakini mitume walikuwa 12 na mitume aliwapata kutoka kwa wanafunzi wake.

Tena Katika wale mitume kumi na mbili,kuna watatu alikuwa nao karibu zaidi ,hao ndiyo alienda nao mlimani.Kwa hiyo yaliyotokea kule mlimani yalishuhudiwa na wale wanafunzi watatu.
Kwa hiyo wanafunzi wa Yersu walikuwa wengi,sasa Kusema Luka hakuwa mwanafunzi wa Yesu siyo sahihi .Hata kama Luka hakuwepo wakati Yesu yupo na labda alijiunga baadaye bado ni mwanafunzi wa Yesu kwani si ni Yesu aliagiza "enendeni ulimwenguni kote mkawawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu?Hapa nyie mnakuwa mnafail wapi kuelewa mbona mambo yako wazi?

Kwa hiyo kama ulivyoandika "vitu kama hivi vinakuwa taabu kuthibitisha " uko sahihi kwani huwezi kuthibitisha kitu ambacho hukijui,hayo tuachie sisi tutathibitisha wewe huwezi.
Kuhusu jina Theophilus soma hapo chini

Luke was written to be read aloud to a group of Jesus-followers gathered in a house to share the Lord's supper. The author assumes an educated Greek-speaking audience, but directs his attention to specifically Christian concerns rather than to the Greco-Roman world at large.He begins his gospel with a preface addressed to "Theophilus": the name means "Lover of God," and could mean any Christian though most interpreters consider it a reference to a Christian convert and Luke's literary patron.

Kitu ambacho umekosa ni kwamba nyakati zile barua ilitumwa kwa mtu na kama ilitakiwa isomwe kwa jamii husika au kanisa basi ilisomwa.Kwa hiyo kitabu cha Luka kwa kuwa kimeanza na kutaja hilo jina Theophilus ambalo linamanisha Mtu wa Mungu au Mtumishi wa Mungu hii haimanishi kilikusudiwa kwa ajili ya huyo mtu mmoja.Chochote unachokiona kimeandikwa kwenye biblia maana yake siyo siri kinafaa kwa ajili ya waamini kukifahamu au kujifunza.Kwa hiyo kama kitabu cha Luka kilimhusu mtu mmoja tu na hakutakiwa kuisoma barua hiyo kwa kanisa basi isinge andikwa .Lakini hata kama barua hiyo ilikusudiwa kwa mtu mmoja na baada ya kuisoma akaona yaliyomo yanafaa na wengine wayafahamu au yatawasaidia katika imani,shida iko wapi wengine wakijua mpaka iwe ni topic inawasumbua mpaka mnasema kitabu hicho ni barua ilikuwa inaenda kwa mtu mmoja?Shida hapo ni nini?Hoja yenu hapa haina nguvu kama ambavyo nimekuwa nasema.
Regards
Aqua
 
Kwani muhimu Si elimu au vipi ? Kwani hizo Aya Za biblia huwa wewe unaziandika ,Si unazi copy kutoka kwenye vitabu ? Kwani Nani kakukataza kutuwekea elimu kutoka kwenye vitabu vya Kanisa lako ?

Lete majibu ya hoja kama unayo ,usilalamike Na kukasirika

Tuambie maana ya Neno kristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…