Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie


Unakimbia swali? Hivi mbona makanisani mumeweka picha ya yesu Mzungu? Na masanamu ya Yesu Mzungu ?
 


Hujaleta ushahidi wowote kuthibitisha kuwa Luka alikuwa ni mwanafunzi wa Yesu. Hizo ngonjera ulizoandika ndizo mbinu Za mwachungaji makanisani Za kuwadanganya watu.

Luka 1 1 Kasema mwenyewe kuwa baada kuona watu wengi wameandika Na yeye akaona ni bora Na yeye aandike baada ya kufanya uchunguzi

1Kwa kuwa watu wengi wamekaa ili kuandika habari za mambo yaliyotukia katikati yetu,

2kama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale waliokuwa mashahidi walioyaona na watumishi wa Bwana,

3mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo hayo, ewe mtukufu Theofilo,

4ili upate kujua ukweli kuhusu yale uliyofundishwa.

Soma bila jaziba
 
Hafs aliewandikia Koran mnayosoma leo aliwahi ata kumuona Muhammad?
 
Sorry thread inasema nini? Fungua uzi tutakujibu
Punguza ku copy na ku paste
Wewe umehoji uhalali wa Luka kuandika ,

Nimekupa swali rahisi sana
Hafs aliewandikia Koran mnayosoma soma leo , aliwahi kumuona Muhammad , jibu kirahisi tu ndio au hapana acha kuleta janjajanja
 
Punguza ku copy na ku paste
Wewe umehoji uhalali wa Luka kuandika ,

Nimekupa swali rahisi sana
Hafs aliewandikia Koran mnayosoma soma leo , aliwahi kumuona Muhammad , jibu kirahisi tu ndio au hapana acha kuleta janjajanja
kwani aliyeandika quran ndiye kaandika biblia ??? lete wewe hayo maandiko kutoka vitabu vya kanisa lako hajakukataza mtu, ndiyo kupeana elimu
 
Limenitendea mengi.
Itoshe kusema jina la Yesu , Yesu jina lenye nguvu[emoji120]
 

Busara ya Mwenyezi Mungu kukataza mafunzo ya Yesu yasikiuke mipaka ya Israili ni kuwa isije dini ya haki ikaharibiwa na ushirikina wa makafiri ulioenea pande zote katika zama zile. Ulimwengu ulikuwa bado haujawa tayari kupokea ujumbe wa ulimwengu mzima, na huyo mwenye kuweza kubeba ujumbe ule hajazaliwa, na umma wa kutimiza jambo hilo na kulieneza bado haujapikika ukawa tayari. Yaliyotokea tumeyaona.

Ukristo tuuonao na ulioenea ulimwenguni sio Ukristo aliofundisha Yesu. Wa Yesu ulitoweka na mwenyewe na wafuasi wake wa mwanzo wa kabila la Kiyahudi. Paulo kaufuja Ukristo.

Kauli zinazonukuliwa kwa kudai kuwa ni ushahidi kuwa Yesu mwenyewe alitaka mafunzo yake yakafundishwe kwa ulimwengu wote yamo katika Injili ya Mathayo 28.19-20, Injili ya Luka 24.46-49 na Marko 16.15. Mathayo inasema:


Basi, enendeni, mkwafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 28.19-20

Luka anatwambia:

(Yesu) akwaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, naweletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kueni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Luka 24.46-49

Na Injili ya Marko inasema:

(Yesu) akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Marko 16.15

Je, imekuwaje?
Yesu ni kigeugeu?

Mbona huku anawakataza wanafunzi wake wasende kuwahubiria ila kabila kumi na mbili za Israili, na huku anawaambia nendeni kuwahubiria Injili ulimwengu mzima. La, Yesu si mbabaishi, wala si kigeugeu. Hebu natuziangalie vilivyo hizo amri mbili, moja ya kuwa mafunzo yake wasifunzwe ila wana wa Israili tu, na ya pili ni hii ya kuwa watu wote wafunzwe dini.

Vipande vyote vitatu tulivyonukulu mwishoni havitaji mambo ya Yesu alipokuwa na maisha yake ya uhai wa kidunia, lakini vyaeleza mambo yaliyotukia baada ya "kufufuka kutoka wafu" kama inavyosimuliwa na Injili zote tatu. Yajuulikana kuwa Injili ya mwanzo kuandikwa ni Injili ya Marko. Hizo nyingine ziliandikwa baadae, na labda ujuzi wao ulitegemea hiyo hiyo Injili ya Marko.

Yajuulikana vile vile kuwa maneno yote yaliyohusu kufufuka Yesu kutokana na wafu, pamoja na hayo maamrisho ya kwenda kuihubiri Injili "kwa kila kiumbe", kinyume na maamrisho yake yote ya kuwa asihubiriwe ila Muisraeli tu - maneno hayo yote hayakuwamo katik Marko ya asli, bali yaliongezwa baadae.
Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.

William Neil akiandika katika tafsiri ya Biblia iitwayo Harper's Bible Commentary anasema:

"Kama lipo jambo lolote katika uchunguzi wa Injili ambalo juu yake wataalamu wamekubaliana, ni kuwa kufika hapa (yaani Marko 16.8) Injili ya Marko inakoma. Sehemu iliyobaki ya sura (yaani 16.9-20) ndio hiyo iitwayo "Kimalizio kirefu" cha Injili.

Kimalizio hicho hakionekani katika nakla za miswada ya zamani, na ambacho ni nyongeza iliyopachikwa katika karne ya pili kutokana na maongezo ya Mathayo, Luka na Matendo...

ushahidi wa kale kabisa ulioandikwa juu ya Kufufuka (Yesu) haumo katika Injili bali katika barua ya kwanza ya Paulo kuwapelekea Wakorintho 15.3-8."
 
Punguza copy paste , soma unaposoma andika kwa ufupi sio unachukua desa kama lilivyo unapachika humu
 
jibu hoja kuwa sio , au copy vitabu vya mchungaji wako utupe elimu usilalamike
Koran iliyonayo imeandikwa kutoka kwa hafs na hafs alikuwepo miaka zaidi ya 200 baada ya Muhammad , hajawahi kumuona Muhammad , hafs na yeye anasema aliadithiwa Koran na mjomba ake, Yani ni mlolongo wente utata na janja janja nyingi

Hafs waislamu pia wanamuita ni muongo na aaminiki kabisa , ni mwizi wa kazi za kiuandishi za watu
 
Koran iliyonayo imeandikwa kutoka kwa hafs na hafs alikuwepo miaka zaidi ya 200 baada ya Muhammad , hajawahi kumuona Muhammad , hafs na yeye anasema aliadithiwa Koran na mjomba ake, Yani ni mlolongo wente utata na janja janja nyingi

Petro akasimama pamoja na wale wanafunzi kumi na moja, akawaambia umati:

“Enyi watu wa Israeli, sikilizeni neno hili: Yesu wa Nazareti alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kati yenu kwa yeye, kama ninyi wenyewe mjuavyo.” (Matendo 2:22).

Kwa hiyo, Mungu ndiye aliyefanya miujiza hiyo kupitia Yesu ili kuwasadikisha watu kwamba Yesu aliungwa mkono na Mungu. Petro hakuona miujiza hiyo kuwa uthibitisho wa kwamba Yesu ni Mungu.

Kwa kweli, jinsi Petro anavyomtaja Mungu na Yesu huonyesha wazi kwamba Yesu sio Mungu. Kwa maana daima anageuza jina la Mungu kutoka kwa Yesu. Chukua marejeleo yafuatayo kwa mfano:

“Mungu amemfufua huyu Yesu…” (Matendo 2:32).

"Mungu amemfanya huyu Yesu mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo." (Matendo 2:36)

Katika vifungu vyote viwili, jina la Mungu limegeuzwa kutoka kwa Yesu. Basi kwa nini alifanya hivi, ikiwa Yesu alikuwa Mungu?
Kwa Petro, Yesu alikuwa mtumishi wa Mungu. Petro alisema:

“Mungu alimfufua mtumishi wake…” (Matendo 3:26).

Cheo cha mtumishi kinarejelea Yesu. Hili liko wazi kutokana na kifungu kilichotangulia ambapo Petro alisema:

"Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu." (Matendo 3:13).

Lazima Petro alijua kwamba Ibrahimu, Isaka, na Yakobo hawakuzungumza kamwe juu ya Mungu wa Utatu. Siku zote walizungumza juu ya Mungu kama Mungu pekee. Hapa, kama katika Mathayo 12:18, Yesu ni mtumishi wa Mungu.

Mathayo anatuambia kwamba Yesu alikuwa mtumishi yule yule wa Mungu aliyetajwa katika Isaya 42:1. Kwa hiyo, kulingana na Mathayo na Petro, Yesu sio Mungu, bali mtumishi wa Mungu. Agano la Kale linasema tena na tena kwamba Mungu yuko peke yake (kama vile Isaya 45:5).
Wanafunzi wote wa Yesu walikuwa na maoni haya. Katika Matendo 4:24 tunaambiwa kwamba waumini walimwomba Mungu wakisema:
“...wakapaza sauti zao pamoja katika kumwomba Mungu. Wakasema, ‘Bwana Mwenye Enzi Kuu, wewe ndiye uliyeziumba mbingu na dunia na bahari na vyote vilivyomo.’”
Ni wazi kwamba yule waliyekuwa wakimuomba hakuwa Yesu, kwa sababu, mistari miwili baadaye, walimtaja Yesu kuwa
"...mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta." (Matendo 4:27).
Ikiwa Yesu alikuwa Mungu, wanafunzi wake walipaswa kusema hivyo waziwazi. Badala yake, waliendelea kuhubiri kwamba Yesu alikuwa Kristo wa Mungu. Tunaambiwa katika Matendo::
“Siku baada ya siku, katika hekalu kutoka nyumba kwa nyumba, hawakuacha kamwe kufundisha na kutangaza habari njema kwamba Yesu ndiye Kristo.” (Matendo 5:42).

Neno la Kigiriki “Kristo” ni cheo cha kibinadamu. Inamaanisha “Mtiwa-Mafuta.” Ikiwa Yesu alikuwa Mungu, kwa nini daima wanafunzi wangemrejelea kwa vyeo vya kibinadamu kama vile mtumishi na Kristo wa Mungu, na mara kwa mara watumie jina la cheo Mungu kwa yule aliyemfufua Yesu?

Je, waliogopa wanadamu? Hapana! Walihubiri kweli kwa ujasiri bila kuogopa kufungwa au kuuawa. Walipokabiliwa na upinzani kutoka kwa wenye mamlaka, Petro alisema:

“Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu! Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu...” (Matendo 5:29-30).

Je, walikuwa wamepungukiwa na Roho Mtakatifu? Hapana! Waliungwa mkono na Roho Mtakatifu (angalia Matendo 2:3, 4:8, na 5:32).

Walikuwa wakifundisha tu yale waliyokuwa wamejifunza kutoka kwa Yesu—kwamba Yesu hakuwa Mungu bali, mtumishi wa Mungu na Kristo.

Quran inathibitisha kwamba Yesu alikuwa Masihi (Kristo), na kwamba alikuwa mtumishi wa Mungu (angalia Quran Tukufu 3:45 na 19:30).















 
Waislamu huwa mnachekesha , Yani hafs mnamuita muongo alafu Koran mnasema ndio kasema kweli ,ila Hadith zake zote mmezikataa
 
Punguza copy paste , soma unaposoma andika kwa ufupi sio unachukua desa kama lilivyo unapachika humu

ndiyo ushahidi wako huo wa kuruhusiwa ukristo kuenea ulimwenguni ???
 
takbiriii allah wakubhal ,faidha ameokoka anampenda Yesu
 
Waislamu huwa mnachekesha , Yani hafs mnamuita muongo alafu Koran mnasema ndio kasema kweli ,ila Hadith zake zote mmezikataa
Ushahidi wako huo kuwa luka ni mwanafunzi wa Yesu ??
 
Hallelujah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…