Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Nyie mmejaa Majin kuliko dini yeyote maana mwenye mapepomnayapooza na kusema kiti kasema hivi na Hiv kama lin shetani akabembelezwa badala mumtoe, pia Kwa mwamposa waliojaa huko ni waislam na wanaanguka mapepo vibaya mnoo
 

Wajinga ndiyo waliwao.
 
Panapo mchawi, jini, pepo, tamka tu kwa jina la Yesu, Hakuna mchawi wala jini litabaki hapo wote lazima wasambaratike vibaya
Nyumba ya yesu siku hizi wanafungishwa ndoa za jinsia moja yaani wanaume wanaoa wanaume

Siku yesu akija kuwasalimu huku sijui mtamwambiaje,au labda kama na yeye alikua anafungisha hizi ndoa huko madhabahuni

Oooooh,I almost forgot,kumbe yesu alikua bachelor bhana
 
Hujielew ya biblia yanakuhus Nini, biblia tunaiamini mia mia na ndo maana tunaidoma na huwez kumkuta mkristo mwenye uelewa anasoma kuran maana sio kitabu Cha Mungu lakin huwez kutukuta tukibishana na nyie kuhus kuran yenu tunadili na yanayotuhusu, tunakushangaa unayetaka ukristo uwe sawa na uislam
Huu ni ukristo na protocol zake Baki na Iman Yako kama huutaki ukristo sio kutuletea propaganda zisizoeleweka,kwanza kabisa YESU kristo sio Issa sifa na matendo ya Yesu ni tofaut na ya hyo Isa wenu, msitake kufananisha A kuwa B
 
Biblia ipi unayoiamini? 100% ?

Kjv, Nkjv, queen James version, AV, Au maelfu ya biblia tofauti bila kusahau Satanic bible
 
Hata wewe mwenyewe hapo ukimwamini Yesu Kristo kwa dhati ya moyo wako na kumfanya awe ndiye kiongozi wako wa kiroho ukikemea majini, mapepo na mizimu itakimbia. Hapa suala kubwa ni imani yake na matendo yako matakatifu tu baasi. Hata wewe mwenye kama una majini au mapepo tamka jina la YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI JUU MBINGUNI AKETIYE UPANDE WA KUUME WA MUNGU uone majini yako na mapepo yako yatakavyopata tabu.

Kwa upande wa pili shetani naye anatenda miujiza tena ya kuwashangaza binadamu japokuwa miujiza yake ina mipaka. Hivyo kama kuna watu wanajiita watumishi wa Mungu lakini nyuma ya pazia wanatumia nguvu za ibilisi kutenda miujiza mbele ya wanadamu basi watu hao ndio wanaosemwa katika hayo mafungu ya maandiko matakatifu.
 
Labda huelewi kuwa hakuna anayemuamini Yesu zaidi ya Muislam.

Waislam tunamuamini Yesu kwa ukweli na siyo kwa kudanganywa na kanisa.

Kuambiwa mambo ya yesu ambayo si yake.

Labda huuelewi Uislam. Unajuwa kuwa Yesu katajwa mara nyingi kwenye Qur'an?


Unajuwa kuwa mama'ke Yesu kaenziwa kwenye Qur'an kuliko kwenye Biblia? Kapewa sura (kama biblia mngesema kitabu) nzima kwa jina lake?

Wapi Yesu alisema "Mimi Mungu"?
 
Allah anaabudiwa ingawa hajawahi tamka

"Mimi ni Mungu Niabuduni"

Ila wanaoshadadia Yesu aseme hivyo akiwa katika hali ya umbo bora kabisa, umbo la Binadamu hawajiulizi hili swali.
 
Mnatapeliwa na Wachungaji eti jina la Yesu , yaani hilo sio changa la uso ni mawe ya uso , Yesu mwenyewe kakataza jina lake lisitumiwe nyinyi mnampinga Yesu, ni haki yenu kutapeliwa, Wajinga ndiwo waliwao
 
Allah anaabudiwa ingawa hajawahi tamka

"Mimi ni Mungu Niabuduni"

Ila wanaoshadadia Yesu aseme hivyo akiwa katika hali ya umbo bora kabisa, umbo la Binadamu hawajiulizi holi swali.
Mwajifanya mnaijua Torati (Torah) ya Musa halafu unaandika uongo. Inawezekana ni kweli huyo Allah hajawahi kusema aabudiwe na wanadamu lakini MUNGU wa mbinguni amesema sana kuhusu yeye kuabudiwa na wanadamu. Kuanzia kwa Ibrahimu (baba wa imani) hadi kwenye Torati ya Musa, Manabii wake na Mitume wake. Au Mungu kusema mpaka watu wote wasikie sauti yake?
 
Sitaacha kulishujudia jina la Yesu. Kuandika sitamaliza, ila kisa kimoja tu labda kiwakilishe. Mwaka 2021 nilifunga siku 21 nikiwa na mambo tata sana katika maisha yangu, nikaliita jina la Yesu katika hizo siku zote, nilikuwa na maombi yangu 9, nilijibiwa 8, mbili kati yake zolihitaji financial resources, nilipata kwa muujiza sana mpaka mtaani wananiita usalama wa taifa maana kazi haihusiani na na kuiba cha mtu, within few months mambo yalibadilika sana, haukuisha mwaka kujibiwa, it was instantaneous, mengine yalishashindikana kwa muda wa miaka 9 yakafanikiwa within months. Suala moja lilishindikana ambalo najua kulikuwa na weakness ndani yake, nilihitaji Mungu aniondoe katika hali fulani, ndani yake kuna matendo yasiyompendeza Mungu ambayo kila mtu mzima anafanya anyways, most of us, nilifanya hayo maombi nikiwa sijadhamiria kuachana nayo mimi kama mimi ila nilitarajia Mungu afanye muujiza, imeshindikana hadi leo. Lakini prayers zote zilizokuwa 100% clean zilitiki mpaka nikaogopa, naogopa mpaka leo to be honest, ni financial na mostly personal issues. In addition, nina matukio mengi sana ikiwemo healing prayers, mfano, mama yangu alikuwa ameshikwa na matatizo fulani ya ngozi few years back, siku nimeenda kuwaona nikanotice how bad she was hata kuliko alivyokuwq anaelezea kwa simu, nilipoona nikajisikia huzuni sana, nikaingia ndani nililia kimya kimya, usiku kucha nawaza why and how, nikamwambia Mungu heal her ikikupendeza, the next day she was like 60% better, bila intervention ya ziada, mpaka naondoka akawa ameshapona, sikumwambia ila nilijua this cannot just be by chance. Huyu Yesu mwacheni tu, anasema mkiniita kwa nia nitawajibu kwa lolote mliombalo, He does, always, ni udhaifu wetu tu wa imani unatukosesha kunufaika naye ila kama ni miujiza ya mkate unaweza kufanya sana kupitia Yeye. Usilinganishe Yesu na vitu vya ajabu, yeye Mungu katikati yetu, wala hatofautishwi ukuu na Baba, maana wao ni kitu kimoja! Mungu mmoja katika Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Mtafuteni tu kwa dhati anajibu, wala humhitaji Mwamposa, padre au mchungaji, you can do it mwenyewe.
 
Mnatapeliwa na Wachungaji eti jina la Yesu , yaani hilo sio changa la uso ni mawe ya uso , Yesu mwenyewe kakataza jina lake lisitumiwe nyinyi mnampinga Yesu, ni haki yenu kutapeliwa, Wajinga ndiwo waliwao
Uwe unajitahidi kusoma na kuelewa kilichoandikwa. Usiendeshwe na mihemko. Rudia tena kusoma kisha futa komenti yako.
 
Allah anaabudiwa ingawa hajawahi tamka

"Mimi ni Mungu Niabuduni"

Ila wanaoshadadia Yesu aseme hivyo akiwa katika hali ya umbo bora kabisa, umbo la Binadamu hawajiulizi holi swali.
Sifahamu umeandika kwa kuelewa au kwa kukisia tu? Soma:


qur'an 20:14. Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi. 14

Uislam ni mwema sana, huwa hatukisii.
 
Sifahamu umeandika kwa kuelewa au kwa kukisia tu? Soma:


qur'an 20:14. Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi. 14

Uislam ni mwema sana, huwa hatukisii.
Hakuna jina la Allah hapo.
Wapi Allah anasema Mimi ni Mungu Niabuduni. ?

Angalia hapa Mungu flani anavyojitambulisha

Kutoka 6:2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;
3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.

Wapi Allah anajitambulisha kwa jina lake na kusema ndiye Mungu ?

Tutajuaje anayeongea hapo ni Allah au YEHOVA au BUDHA ?
Ni nani Huyo anayeongea hapo 20:14?
 
Wajinga ndiyo waliwao. Wacheni kudanganyana.

Mnapingana na biblia?

Mathayo 24:
24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.


Uislam ni mwema sana, hauna longolongo.
 
Saw his documentary, amazing sana
 
Nimekuwekea na kiarabu, orijino, ili usione kuwa Qur'an imechezewa kama biblia. Tafsiri ya neno Mwenyezi Mungu ndiyo jina Allah.

qur'an 20:14. Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi. 14

kwa sababu ahaufahamu kusoma Kiarabu, Kama tafsiri ya Kiswahili imekupiga chenga, soma ya Kingereza:

YUSUF ALI
qur'an 20:14.
“Verily, I am Allah: There is no god but I: So serve thou Me (only), and establish regular prayer for celebrating My praise.
 
Yesu ndio chanzo cha uzima wangu, nilishawahi kugongwa na treni, licha ya kwamba gari yangu iliharibiwa kabisa lakini mimi binafsi nilitoka nikiwa mzima kabisaaaaaaaaa
Ikiwa alishindwa kujiokowa mwenyee atakuokowa wewe?

Tujifikirie kidogo.
 
Kwahiyo 20:14 ya Kiswahili ni tofauti na 20:14 ya Kiingereza.
Kwanini hapakuandikwa Allah hapo pa Kishwahili?

Ushakimbilia chaka la Lugha ya Kiarabu.
Nitakujibu baadae ngoja nimalize kiporo.
Ninavyojua Allah ni mjanja mjanja fulani tu.
Na hajawahi kujitambulisha kwa jina lake halisi la Allah popote pale na kwa yeyote yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…